You are on page 1of 13

KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB

SAID RUBEYA, SWALEHE MADJAPA, USTADH M. HASSAN,

JACKSON J. SAGONGE & VALENTINE NYALU....
Waweka Pingamizi

DHIDI
MICHAEL RICHARD
WAMBURA..Muwekewa Pingamizi

MAAMUZI

Waweka Pingamizi waliotajwa hapo juu, ambao ni wanachama wa Simba Sports Club
wamemwekea pingamizi Mwekewa Pingamizi hapo juu kwa hoja zifuatazo:

i. Mwekewa Pingamizi aliipeleka Simba Sports Club mahakamani katika kesi
Namba 100/2010 iliyofunguliwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es
salaam, Kinyume na Ibara ya 11 (1) (e), (2), 12(3), na 55 ya Katiba ya Simba Sports
Club ya Mwaka 2010.
ii. Mwekewa Pingamizi alisimamishwa Uanachama na Kamati ya Utendaji ya
Simba Sports Club iliyokutana tarehe 5 Mei 2010 na barua ya tarehe 6 Mei 2010,
(Kumb. Na. SSC/MMKT/163/VOL.40/11) na hivyo basi anapoteza haki za kuwa
mwanachama wa Simba Sports Club
iii. Mwekewa Pingamizi amekiuka Katiba ya Simba, TFF na FIFA kwa
kuipeleka Simba Sports Club Mahakamani katika kesi Namba 100/2010.
iv. Mwekewa Pingamizi ameanza kampeni kabla ya muda wa Kampeni
v. Mwekewa Pingamizi amekiuka katiba ya Simba kwa kukubali uteuzi batili
kuwa mjumbe kamati ya uchaguzi.
vi. Mwekewa pingamizi hana maadili ya Uongozi kwasababu alikiuka maadili
akiwa kiongozi wa FAT/TFF.
vii. Mwekewa Pingamizi sio mwajibikaji.

Nakala ya mapingamizi hayo na mwaliko wa kikao cha kusikiliza pingamizi
valikabidhiwa kwa mwekewa pingamizi tarehe 23 Mei 2014. Siku ya kusikiliza
Pingamizi, tarehe 25 Mei 2014, Mwekewa pingamizi aliwasilisha mbele ya kamati ya
uchaguzi preliminary objections mbili kama ifuatavyo:

i. Dhidi ya waweka pingamizi wote watano(ona kiambatanisho A)
ii. Dhidi ya Kamati ya Uchaguzi ya Simba (ona kiambatanisho B)

Kabla ya kuanza kusikiliza mapingamizi ya waweka pingamizi, kamati ilisikiliza
preliminary objections na kutoa maamuzi kama ifuatavyo.

Mosi, preliminary objections dhidi ya wagombea watano (5), kimsingi ni majibu ya
pingamizi toka kwa ya wakewa pingamizi, hivyo basi, hoja hizo zitapata fursa wakati
mwekewa pingamizi anajibu hoja za waweka pingamizi.

Pili, preliminary objections dhidi ya kamati zinatupiliwa mbali kwa misingi
ifuatavyo;
a. Uteuzi wa katibu wa kamati ya uchaguzi samba sports club ulifanywa na
kamati ya utendaji ambayo mweka prelimary objections alihudhuria.
b. Kamati imeamua kuazima na kutumia kanuni za uchaguzi za TFF
kwasababu Kamati ya utendaji Simba haijaandaa kanuni hizo.
c. Unapoazima na kutumia kanuni za Mamlaka nyingine sio lazima uzitumie
kama zilivyo, una uhuru wa kufanya maboresha ili kuzingatia hali halisi ya Simba
Sports Club.
d. Pingamizi dhidi ya Bw. Evans Aveva ni malalamiko ya kawaida ambayo
Kamati inabidi iyazingatie kwa wakati wake na sio sehemu ya mapingamizi
kwasababu muda wa pingamizi umekwisha.
e. Kanuni hazielezi haki ya kuweka preliminary objections, lakini kamati
ilitumia busara kuzisikiliza.

Hivyo basi kamati ilitupilia mbali prelimary objections na kusikiliza pingamizi
katika mfumo wa kawaida.

Kamati, awali ya yote, ilichambua masuala ya kimaadili na kuamua kuwa mambo
hayo ya kimaadili, yapelekwe katika kamati ya maadili ya TFF na waweka pingamizi
wenyewe. Mambo ya kupelekwa kamati ya maadili ni:

i. Mwekewa Pingamizi amekiuka katiba ya Simba kwa kukubali uteuzi batili
kuwa mjumbe kamati ya uchaguzi.
ii. Mwekewa pingamizi hana maadili ya Uongozi kwasababu alikiuka maadili
akiwa kiongozi wa FAT/TFF.
iii. Mwekewa Pingamizi sio mwajibikaji.

Kamati ilijadili na kuyatolea maamuzi mapingamizi yafuatayo:

i. Mwekewa Pingamizi ameanza kampeni kabla ya muda wa Kampeni.

Kamati ilikwisha toa adhabu ya ONYO KALI dhidi ya Mwekewa Pingamizi kuhusu
kuanza kampeni kabla ya wakati, hivyo basi hawezi kuadhibiwa mara mbili kwa kosa
ambalo ameshaadhibiwa.

ii. Mwekewa Pingamizi aliipeleka Simba Sports Club katika kesi Namba
100/2010 iliyofunguliwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam,
Kinyume na Ibara ya 11 (1) (e), (2), 12(3), na 55 ya Katiba ya Simba Sports Club ya
Mwaka 2010.

Ushahidi uliotolewa mbele ya kamati unaonyesha kuwa Mwekewa pingamizi
alifungua kesi No. 100/2010 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya
Simba Sports Club katika masuala ambayo hayapaswi kwenda mahakamani. Kitendo
hicho ni ukiukwaji wa Ibara ya 11 (1) (e), (2), 12(3), na 55 ya Katiba ya Simba ya
Mwaka 2010.

iii. Mwekewa Pingamizi alisimamishwa Uanachama na Kamati ya
Utendaji ya Simba Sports Club iliyokutana tarehe 5 Mei 2010 na hivyo basi anapoteza
haki za kuwa mwanachama wa Simba Sports Club.

Kamati imepokea ushahidi na kuridhika kuwa tarehe 5 Mei 2010, kupitia kikao halali
kamati ya utendaji ya Simba Sports Club ilimsimamisha Uanachama Mwekewa
Pingamizi kwa tuhuma za kuipeleka Simba Mahakamani katika kesi tajwa. Baada ya
kusimaishwa uanachama na kamati ya utendaji kwa mujibu wa Ibara 12(1),(2) & (3)
ya katiba ya Simba mwaka 2010, jambo hilo lilipaswa kupelekwa katika mkutano
mkuu ili mkutano mkuu, utoe adhabu au utoe msamaha. Kwa mujibu wa Katiba ya
Simba, Ibara ya 55, adhabu ya kosa hilo ni kufukuzwa uanachama. Si kamati ya
utendaji wala Mwekewa Pingamizi aliyepeleka suala hili katika mkutano mkuu ili
litolewe uamuzi.

Kamati imepokea barua tatu, toka kwa Mwekewa Pingamizi, kuhusu uanachama wake
Simba Sports Club. Barua ya kwanza iliandikwa tarehe 6 Novemba 2012 toka kwa
Bw. Michael Wambura kwenda kwa Mwenyekiti wa Simba. Barua hiyo inakiri kosa
la kuipeleka Simba makahamani na kuahidi kuwa hatarudia tena. Barua ya pili toka
kwa Mwenyekiti wa Simba ya tarehe 15/09/2012, Ref. No. SSL/20/9/12, kukiri
kupokea barua toka kwa Bw. Michael Wambura na kuahidi kuwa suala hilo
litafanyiwa kazi, ingawa kamati ilibaini kuwa barua ya kujibu imeandikwa takribani
miezi miwili kabla ya ile ya awali jambo ambalo haliwezekani. Barua ya tatu ni ya
tarehe 25/9/1012, kumb. SSC 28/9/12 ambayo inasema samba haina tatizo na Bw.
Michael Wambura, lakini Uhalali wa Barua hiyo unashaka kubwa sana kiasi cha
kamati kuamua ipelekwe kwenye mamlaka husika kwa hatua zaidi.

Hivyo basi kamati imejiridhisha kuwa maamuzi ya Kamati ya utendaji ya tarehe 5
Mei 2010 ya kumsimamisha Mwekewa Pingamizi bado yanaendelea na yana nguvu
za kisheria kwasababu hakuna maamuzi yoyote ya Mkutano Mkuu kubatilisha hatua
hiyo.

Mwananchama ambaye amesimamishwa uananchama hana haki ya kushiriki katika
shughuli za simba kwa mujibu wa Ibara ya 12 (3) ya Katiba ya Simba ya Mwaka
2010 na Ibara ya 12 (3) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2014.

iv. Mwekewa Pingamizi amekiuka Katiba ya Simba, TFF na FIFA kwa
kuipeleka Simba Sports Club Mahakamani katika kesi Namba 100/2010.

Kamati inapenda kurejea maamuzi yake hapo juu katika suala ka kwenda
mahakamani kwa masuala ya Soka.

Hivyo basi Muwekewa Pingamizi, Bw. Michael Richard Wambura ameondolewa
katika mchakato wa Uchaguzi, kwa sababu zilizotajwa hapo juu.

Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki ya kukata rufaa
katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.

Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.

.
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club

KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB

ARTHUR MWAMBETA ..... Muweka
Pingamizi

DHIDI
GEOFREY NYANGE (KABURU) ..Muwekewa
Pingamizi

MAAMUZI

Awali, kamati ilipokea mapingamizi mawili dhidi ya Muwekewa Pingamizi toka kwa
Bw. Hafidh Bashir na Bw. Arthur Mwambeta, lakini katika mchakato wa kusikiliza,
Bw. Hafidh Bashir, aliamua kuondoa pingamizi hilo. Kwa mujibu wa maamuzi hayo
tuna Muweka Pingamizi mmoja, tajwa hapo juu. Hoja za Muweka Pingamizi ni Kama
ifuatavyo:
i. Muwekewa Pingamizi, akiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba kati
ya Mwaka 2010-2013 alishindwa kuwasilisha Audited Accounts kwenye Mkutano
Mkuu wa Simba, kwa mujibu wa ibara ya 19 (6), (7), 30 (1) (f) na 33 (5) ya katiba ya
Simba ya Mwaka 2010.
ii. Muwekewa Pingamizi, akiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba kati
ya Mwaka 2010-2013 alishindwa kujaza nafasi ya Mjumbe wa kamati ya Utendaji
(Mwanamke) iliyowazi kwa mujibu wa Ibara ya 28(1)(c) na 29 (3) ya Katiba ya
Simba ya Mwaka 2010.
iii. Muwekewa Pingamizi, akiwa sehemu ya Kamati ya Muda ya Simba Sports
Club ya Mwaka 2005, aliuza gari la Simba Sports Club kinyume na maagizo ya
Baraza la Wazee na Ibara ya 11(1) (b) na (c) na Ibara ya 6 (1) (iii) ya Simba.

Kamati ilisikiliza pande zote mbili na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na
hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:

Hoja zote tatu za pingamizi hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya kamati ya utendaji ya
Simba Sports Club na Kamati ya Muda ya Simba ya Mwaka 2005. Hakuna Ushahidi
wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili
na kuitolea maamuzi dhidi ya kamati ya utendaji kwasababu zifuatazo.

Mosi, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha juu kuliko kamati ya
Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea, hivyo ipo nje ya
Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, hakuna Ushahidi wowote dhidi ya Muwekewa Pingamizi binafsi na kama
Ungekuwepo, basi suala hilo lingefikishwa katika kamati husika na sio kamati ya
uchaguzi.

Hivyo basi Pingamizi, dhidi ya Muwekewa Pingamizi Bw. Geofrey Nyange (Kaburu)
limetupiliwa Mbali.

Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki ya kukata rufaa
katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.

Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.

.
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club

KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB

SAID ALI MANERO .....
Muweka Pingamizi

DHIDI
EVANS ELIEZA AVEVA
...Muwekewa Pingamizi

MAAMUZI

Kamati ilipokea mapingamizi dhidi ya Muwekewa Pingamizi, toka kwa Muweka
Pingamizi hapo juu. Hoja za Muweka Pingamizi ni Kama ifuatavyo:
i. Muwekewa Pingamizi, aliwahi kugombea uchaguzi wa DRFA mwaka
2013 kwa jina la Evans Aveva lakini katika vyeti vyake anatumia jina la Evans
Eliyeza, hivyo anaweza kuwa mtu tofauti, elimu ikwa haikidhi matakwa ya Katiba na
uraia wake kutiliwa shaka, hivyo kuiuka ibara ya 26 (1) (2) ya Katiba ya Simba ya
Mwaka 2010.
ii. Muwekewa Pingamizi, akiwa sehemu ya Kamati ya Muda ya Simba Sports
Club ya Mwaka 2005, aliuza gari la Simba Sports Club kinyume na maagizo ya
Baraza la Wazee na Ibara ya 11(1) (b) na (c) na Ibara ya 6 (1) (iii) ya Simba.

Kamati ilisikiliza pande zote mbili na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na
hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:

Hati ya kusafiria ya Muwekewa Pingamizi namba AB 047458 iliyotolewa tarehe
26/08/2006 inamajina: Evans Elieza Aveva, hivyo hakuna utata wowote dhidi ya jina
la mgombea. Muweka Pingamizi ameshindwa kuleta Ushahidi wowote kuhusu
mashaka yake katika elimu, uanachama au uraia wa muwekewa pingamizi, hivyo basi
hoja yake ya awali katika pingamizi hili inakosa miguu ya kikanuni na kutupiliwa
mbali.

Hoja ya pili ya pingamizi hapo juu inahusu tuhuma dhidi ya Kamati ya Muda ya
Simba ya Mwaka 2005. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati
ya Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kutoa maamuzi dhidi ya kamati ya muda
ya Simba ya Mwaka 2005 kwasababu zifuatazo.

Mosi, Kamati ya Muda ya Simba ya Mwaka 2005, ambayo hivi sasa haipo, sio
Mgombea, hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Pili, hakuna Ushahidi wowote dhidi ya Muwekewa Pingamizi Binafsi na kama
Ungekuwepo, basi suala hilo lingefikishwa katika kamati husika na sio kamati ya
uchaguzi.

Hivyo basi Pingamizi, dhidi ya Muwekewa Pingamizi Bw. Evans Elieza Aveva
limetupiliwa Mbali.

Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki ya kukata rufaa
katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.

Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.

.
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club

KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB

MWINYI SHARIFF DOSSI..... Muweka
Pingamizi

DHIDI
SWEDI MKWABI, JOSEPH ITANGARE (KINESI)
SAIDI PAMBA, IBRAHIM MASOUD &
DANIEL MANEMBE
..Muwekewa Pingamizi

MAAMUZI

Kamati ilipokea pingamizi dhidi ya Wawekewa Pingamizi toka kwa Muweka
Pingamizi tajwa hapo juu. Hoja za Muweka Pingamizi ni Kama ifuatavyo:

i. Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba
walifanya maamuzi ya kumpindua Mwenyekiti wa Simba Sports Club kinyume na
ibara ya 33 (3) (a) (b) (c) na (d) ya katiba ya Simba ya Mwaka 2010.
ii. Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba
walishindwa kujaza nafasi zilizowazi ndani ya siku 90 kwa mujibu wa Ibara ya
28(1)(c) na 29 (3) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2010.

Muweka Pingamizi hakutokea bila sababu yoyote, hata hivyo, Kamati ilisikiliza
utetezi wa wawekewa pingamizi na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na
hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:

Hoja zote tatu za pingamizi hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya kamati ya utendaji ya
Simba Sports Club. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya
Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kutoa maamuzi dhidi ya kamati ya utendaji
kwasababu zifuatazo.

Mosi, Kamati ya Utandaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha juu kuliko kamati ya
Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea, hivyo ipo nje ya
Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, Suala hilo linapaswa kupelekwa katika kamati husika ya maadili na sio kamati
ya uchaguzi.

Hivyo basi Pingamizi, dhidi ya wawekewa Pingamizi wote hapo juu; SWEDI
MKWABI, JOSEPH ITANGARE (KINESI), SAIDI PAMBA, IBRAHIM MASOUD
&
DANIEL MANEMBE limetupiliwa Mbali.

Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki ya kukata rufaa
katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.

Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.

.
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club

KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB

JAMHURI MUSSA KIHWELO.....
Muweka Pingamizi

DHIDI
SWEDI MKWABI, JOSEPH ITANGARE (KINESI)
SAIDI PAMBA, IBRAHIM MASOUD &
DANIEL MANEMBE
..Muwekewa Pingamizi

MAAMUZI

Kamati ilipokea pingamizi dhidi ya Wawekewa Pingamizi toka kwa Muweka
Pingamizi tajwa hapo juu. Hoja za Muweka Pingamizi ni kama ifuatavyo:

i. Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba
walifanya kikao haramu kinyume na ibara ya 33 (4) ya katiba ya Simba ya Mwaka
2010 na kufanya mapinduzi dhidi ya Mwenyekiti.
ii. Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba
walipitisha maamuzi batili ya kuwafukuza walimu wa mpira bila malipo na mamlaka
hivyo kusababisha usumbufu mkubwa hadi leo.

Muweka Pingamizi alitoa maelezo yake na wawekewa pingamizi walijibu hoja hizo.
Kamati ilisikiliza hoja na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na hatimaye
kutoa maamuzi yafuatayo:

Hoja za pingamizi hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya kamati ya utendaji ya Simba
Sports Club. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya
Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kuitolea maamuzi dhidi ya kamati ya utendaji
kwasababu zifuatazo.

Mosi, Kamati ya Utandaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha juu kuliko kamati ya
Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea, hivyo ipo nje ya
Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, Suala hilo linapaswa kupelekwa katika kamati husika ya maadili na sio kamati
ya uchaguzi.

Aidha kuhusu hoja ya Kufukuzwa Walimu wa mpira, kamati inamshauri muweka
pingamizi apeleke shauri hilo katika Kamati ya Sheria ya TFF au Mahakama ya kazi
kwasababu ni suala la mwajiri na mwajiriwa.

Hivyo basi Pingamizi, dhidi ya wawekewa Pingamizi wote hapo juu; SWEDI
MKWABI, JOSEPH ITANGARE (KINESI), SAIDI PAMBA, IBRAHIM MASOUD
&
DANIEL MANEMBE limetupiliwa Mbali na yale yanayohusu maadili yaenda katika
kamati husika.

Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki ya kukata rufaa
katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.

Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.

.
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club

KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB

ARTHUR MWAMBETA ..... Muweka
Pingamizi

DHIDI
SWEDI MKWABIMuwekewa
Pingamizi

MAAMUZI

Muweka Pingamizi aliondoa pingamizi lake. Hivyo kamati haikusikiliza pingamizi
hilo.

Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.

.
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club

KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB

LUKA NGWAKO MBAPILA.....}
Waweka Pingamizi
OMAR JUMA MUNGA }
SALIM R. SIMBA ...}
ABDALLAH MKOVA }

DHIDI
SWEDI MKWABIMuwekewa
Pingamizi

MAAMUZI

Waweka Pingamizi wote walileta hoja zifuatazo.
i. Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba
walishindwa kujaza nafasi zilizowazi ndani ya siku 90 kwa mujibu wa Ibara ya
28(1)(c) na 29 (3) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2010.
ii. Taarifa za mahesabu kwenye mkutano mkuu ziliwasilishwa kwa lugha ya
kiingereza hivyo kumnyima haki ya kujua mapato ya klabu kwa miaka minne.

Waweka Pingamizi hawakutokea bila sababu yoyote, hata hivyo, Kamati ilisikiliza
utetezi wa wawekewa pingamizi na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na
hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:

Hoja zote tatu za pingamizi hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya kamati ya utendaji ya
Simba Sports Club. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya
Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kuitolea maamuzi dhidi ya kamati ya utendaji
kwasababu zifuatazo.

Mosi, Kamati ya Utandaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha juu kuliko kamati ya
Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea, hivyo ipo nje ya
Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, Suala hilo linapaswa kupelekwa katika kamati husika ya maadili na sio kamati
ya uchaguzi.

Hivyo basi pingamizi linatupiliwa mbali.

Kwakuwa hawakuja kutetea pingamizi lao hawana haki ya kukata rufaa.

Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.

.
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club

KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB

MWINYI SHARIFF DOSSI.....}
Waweka Pingamizi
SWALEHE MADJAPA .}

DHIDI
KARAHA HASSAN CHANO
(ALMAS)Muwekewa Pingamizi

MAAMUZI

Waweka Pingamizi wote walileta hoja zifuatazo.
i. Muwekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba
(Mhasibu Msaidizi) hakuleta taarifa za fedha katika Mkutano Mkuu ambayo
ilisababisha kuondolewa katika uchaguzi wa 2010 baada ya kuwekewa pingamizi na
Asha Kigundula na hajawahi kusamehewa na mkutano mkuu wowote.

Waweka Pingamizi hakutokea bila sababu yoyote, hata hivyo, Kamati ilisikiliza
utetezi wa wawekewa pingamizi na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na
hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:

Hoja zote tatu za pingamizi hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya kamati ya utendaji ya
Simba Sports Club. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya
Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kuitolea maamuzi dhidi ya kamati ya utendaji
kwasababu zifuatazo.

Mosi, Kamati ya Utandaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha juu kuliko kamati ya
Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea, hivyo ipo nje ya
Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, Suala hilo linapaswa kupelekwa katika kamati husika ya maadili na sio kamati
ya uchaguzi.

Hivyo basi pingamizi linatupiliwa mbali.

Kwakuwa hawakuja kutetea pingamizi lao hawana haki ya kukata rufaa.

Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.

.
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club

You might also like