You are on page 1of 72

www.vitabutanzania.

com

Vitabutanzania Project
LULU ZA KISWAHILI

METHALI MIA SITA NA KUMI (610)
1. Aanguaye huanguliwa.
2. Asiye sikia la mkuu, huvunjika guu.
3. Abebwaye hujikaza.
4. Adhabu ya kaburi aijuae maiti.
5. Adui aangukapo, mnyanyue.
6. Adui mpende.
7. Adui wa mtu ni mtu.
8. Afadhali ya Musa kuliko ya Firauna.
9. Ahadi ni deni.
10. Ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke.
11. Akiba haiozi.
12. Akili ni mali.
13. Akili ni nywele kila mtu ana zake.
14. Akili nyingi huondowa maarifa.
15. Akutukanae hakuchagulii tusi.
16. Akipenda chongo huita kengeza.
17. Akufaae kwa dhiki, ndiye rafiki.
18. Akufanyiaye ubaya, mlipe wema.
www.vitabutanzania.com
19. Akupaye kisogo si mwenzio.
20. Akutendaye mtende, mche asiyekutenda.
21. Alisifuye jua, limeuangaza.
22. Aliye juu msubiri chini.
23. Aliye kando, haangukiwi na mti.
24. Aliye kupa wewe kiti (kibao) ndiye aliye nipa mimi kumbi.
25. Aliye kutwika, ndiye atakaye kutua.
26. Akufukuzae hakwambii toka.
27. Aliyekupa mkeka ndiye aliyenipa kumbesa.
28. Amani haipatikani mpaka kwa ncha ya upanga.
29. Ana hasira za mkizi.
30. Anayekuja pasi na hodi, huondoka bila ya kuaga.
31. Angurumapo simba, mcheza ni nani?
32. Aninyimaye mbazi kanipunguzia mashuzi.
33. Apewaye ndiye aongezwaye.
34. Anaejipiga mwenyewe, halii.
35. Asifuye mvuwa imemnyea.
36. Asiye kubali kushindwa si mshindani.
37. Asiye kujua, hakuthamini.
38. Asiye kuwapo na lake halipo.
39. Asiye lelewa na mamae hulelewa na ulimwengu.
40. Asiye na mengi, ana machache.
41. Asiye uliza, hanalo ajifunzalo.
42. Asiyejua maana, haambiwi maana.
43. Atangaye na jua hujuwa.
44. Atangazaye mirimo, si mwana wa ruwari (Liwali).
45. Atekaye maji mtoni hatukani mamba.
46. Avumaye baharini papa kumbe wengi wapo.
47. Baada ya dhiki faraja.
www.vitabutanzania.com
48. Bahari hailindwi.
49. Bamba na waume ni bamba, hakuna bamba la mume.
50. Bandu bandu huisha gogo.
51. Baniani mbaya, kiatu chake dawa.
52. Bendera hufuata upepo.
53. Biashara asubuhi.
54. Bilisi wa mtu ni mtu.
55. Bora kinga kuliko tiba.
56. Bora lawama kuliko fedheha.
57. Bora mchawi kuliko fitina.
58. Biashara asubuhi.
59. Bora nusu shari kuliko shari kamili.
60. Bwawa limeingia ruba.
61. Cha mtu mavi.
62. Chaka la samba, halilali nguruwe.
63. Chamlevi huliwa na mgema.
64. Chanda chema huvikwa pete.
65. Chelewa chelewa, utakuta mtoto si wako.
66. Choko mchokoe pweza, binaadamu hutomuweza.
67. Chombo cha kuzama hakina usukani.
68. Chovya - chovya yamaliza buyu la asali.
69. Chui hakumbatiwi.
70. Chururu si ndo ndo ndo.
71. Dalili ya mvua mawingu.
72. Damu nzito kuliko maji.
73. Daraja livuke ulifikapo.
74. Dawa ya moto ni moto.
75. Daraja ukilibomoa, ujue kuogelea.
76. Dau la mnyonge haliendi joshi, likienda joshi ni matakwa ya Mungu.
www.vitabutanzania.com
77. Dawa ya moto ni moto.
78. Donda ndugu halina dawa.
79. Dua ya kuku haimpati mwewe.
80. Fadhila huna, hata hisani hukumbuki?
81. Fadhila ya nyuki ni moto.
82. Fadhila ya punda ni mateke (mashuz)
83. Fahari ya macho haifilisi duka.
84. Farasi hamuwawezi, tembo mtawalishani?
85. Fata nyuki ule asali.
86. Fimbo ya mbali haiui nyoka.
87. Fumbo mfumbe mjinga, mwerevu huligangua.
88. Funika kombe mwanakharamu apite.
89. Ganda la mua la jana, chungu kaona kivuno.
90. Gome la udi, si la mnuka uvundo.
91. Haba na haba, hujaza kibaba.
92. Haki ya mtu hailiki.
93. Hakuna masika yaso mbu.
94. Hakuna msiba usio na mwenziwe.
95. Hakuna siri ya watu wawili.
96. Hakuna ziada mbovu.
97. Hala hala mti na macho.
98. Hamadi ni ilio kibindoni, na silaha ni iliyo mkononi.
99. Hapana marefu yasio na mwisho.
100. Haraka haraka haina baraka.
101. haraka haraka haina baraka.
102. Haramu yako halali kwa mwenzio.
103. Hasidi hasada.
104. Hasidi mbaya.
105. Hasira, hasara.
www.vitabutanzania.com
106. Hatua ndefu hufupisha mwendo.
107. Hauchi hauchi, unakucha.
108. Hayawi hayawi, mara huwa.
109. Heri kufa macho kuliko kufa moyo.
110. Heri kujikwa kidole kuliko ulimi.
111. Heri nitakula na nini?, kuliko nitakula nini?
112. Heri ya marama kuliko kuzama.
113. Hiari ya shinda utumwa.
114. Hogo halihogoki mpaka kwa hogo jenziwe.
115. Hucheka kovu asiye kuwa na jeraha.
116. Ila ya kikwapa, kunuka pasipo kidonda.
117. Yaliyoopita si ndwele, ganga yajayo.
118. Iliyo jaa ndiyo ipunguzwayo.
119. Imara ya jembe kaingojee shambani.
120. Jambo usilolijua, usiku wa giza.
121. Jina jema hungara gizani.
122. Jini likujualo halikuli likakwisha.
123. Jino la pembe si dawa ya pengo.
124. Jitihada haiondoi kudura.
125. Jitihadi haiondoi kudura.
126. Jogoo la shamba haliwiki mjini.
127. Jungu kuu, halikosi ukoko.
128. Jununu fununu.
129. Kafiri akufaaye, si muislamu asiye kufaa
130. Kafiri akufaye si Isilamu asiyekufa.
131. Kama hujui kufa,tazama kaburi.
132. Kama wewe wasema cha nini, mwezio asema nitakipata lini.
133. Kamba hukatika pabovu.
134. Kanga hazai ugenini.
www.vitabutanzania.com
135. Kawaida ni kama sheria.
136. Kawia ufike.
137. Kazi mbaya siyo mchezo mwema.
138. Kelele za chura hazimzuwii ng'ombe kunywa maji.
139. Kelele za mlango haziniwasi usingizi (Kelele za mlango hazimuudhi mwenye nyumba)
140. Kenda karibu na kumi.
141. Kesho kesho, kesho kiama.
142. Kiburi si maungwana.
143. Kibuzi na kibuzi hununua jahazi.
144. Kichango kuchangizana.
145. Kidole kimoja hakivunji chawa.
146. Kikulacho ki nguoni mwako.
147. Kikushindacho kukila usikitie ila.
148. Kila chombo kwa wimblile.
149. Kila mbwa hubwekea mlangoni kwao.
150. Kila mlango na ufunguwo wake.
151. Kila mtoto na koja lake.
152. Kila mtu huzikwa na kaburi lake.
153. Kila mtu na bahati yake.
154. Kila mwamba ngoma ,ngozi huivuta kwake.
155. Kila mtu hulilia mamae.
156. Kila ndege huruka kwa ubawa wake.
157. Kila shetani na mbuyu wake.
158. Kilimia kikizama kwa jua, huzuka kwa mvua, na kikizama kwa mvua, huzuka kwa jua.
159. Kilio huanza mfiwa ndipo wa mbali wakaingia.
160. Kimya kingi kina mshindo mkubwa.
161. Kinga na kinga ndipo moto uwakapo.
162. Kingiacho mjini si haramu.
163. Kinyozi hajinyoi.
www.vitabutanzania.com
164. Kinywa ni jumba la maneno.
165. Kipendacho moyo dawa.
166. Kipofu hasahau mkongojo wake.
167. Kipya kinyemi ingawa kidonda.
168. Kisebusebu na kiroho papo.
169. Kisokula mlimwengu, sera nale.
170. Kisokula mlimwengu,sera nale.
171. Kisu kimenifika mfupani.
172. Kitanda usicho kilalia hukijui kunguni wake.
173. Kitumbua kimeingia mchanga.
174. Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua.
175. Kiwi cha yule ni chema cha; hata ulimwengu uwishe.
176. Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.
177. Konzi ya maji, haifumbatiki.
178. Konzo ya maji haifumbatiki.
179. Kosa moja haliachi mke.
180. Kozi mwandada, kulala na njaa kupenda.
181. Kuagiza kufyekeza.
182. Kuambizana kuko kusikilizana hapana.
183. Kucha M'ngu si kilemba cheupe.
184. Kuchamba kwingi, kuondoka na mavi.
185. Kufa kufaana.
186. Kufa kwa jamaa, harusi.
187. Kufa kwa mdomo,mate hutawanyika.
188. Kufanaya kosa sio kosa, kosa ni kurudia kosa.
189. Kuishi kwingi, kuona mengi.
190. Kujikwa si kuanguka,bali ni kwenda mbele.
191. Kujikwaa si kuanguka, bali ni kwenda mbele.
192. Kukopa harusi kulipa matanga.
www.vitabutanzania.com
193. Kukopa harusi, kulipa matanga.
194. Kuku havunji yai lake.
195. Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
196. Kula kutamu ,kulima mavune.
197. Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana.
198. Kukopa harusi, kulipa matanga.
199. Kumuashia taa kipofu ni kuharibu mafuta.
200. Kunako matanga kume kufa mtu.
201. Kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake.
202. Kupanda mchongoma, kushuka ndio ngoma.
203. Kupata si werevu, na kukosa si ujinga.
204. Kupoteya njia ndiyo kujua njia.
205. Kurambaramba ndio kula, kunenepa kwake Mola.
206. Kusikia si kuona.
207. Kutangulia si kufika.
208. Kutoa ni moyo usambe ni utajiri.
209. Kutu kuu ni la mgeni.
210. Kuugua sio kufa.
211. Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi.
212. Kuzima koleo si mwisho wa uhunzi.
213. Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaa huenda kilio.
214. Kweli ilio chungu, si uongo ulio mtamu.
215. Kwenda mbio siyo kufika.
216. Kwenye miti hakuna wajenzi.
217. La kuvunda halina rubani.
218. La kuvunda halina ubani.
219. Lake mtu halimtapishi bali humchefua.
220. Leo kwako, kesho kwa mwenzio.
221. Leo ni leo asemayo kesho ni mwongo.
www.vitabutanzania.com
222. Liandikwalo ndiyo liwalo.
223. Lila na fila hazitangamani.
224. Lipitalo, hupishwa .
225. Lisemwalo lipo,ikiwa halipo laja.
226. Lisilo na mkoma, hujikoma lilo.
227. Lisilokuwapo moyoni, halipo machoni.
228. Maafuu hapatilizwi.
229. Macho hayana pazia.
230. Mafahali wawili hawakai zizi moja.
231. Maiti haulizwi sanda.
232. Maji hayapandi mlima.
233. Maji hufuata mkondo.
234. Maji ukiyavuliya nguo huna budi kuyaoga.
235. Maji usiyoyafika hujui wingi wake.
236. Maji ya kifuu, bahari ya chungu.
237. Maji yakijaa hupwa.
238. Maji yakimwagika hayazoleki.
239. Maji yamenifika shingoni.
240. Majuto ni mjukuu.
241. Mali ya bahili huliwa na wadudu.
242. Mama ni mama, hata kama ni rikwama.
243. Mama nipe radhi kuishi na watu kazi.
244. Mambo kunga.
245. Manahodha wengi chombo huenda mrama.
246. Maneno makali hayavunji mfupa.
247. Maneno mazuri humtowa nyoka pangoni.
248. Maneno si mkuki.
249. Mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichika.
250. Masikini akipata matako hulia mbwata.
www.vitabutanzania.com
251. Masikini haokoti,akiokota huambiwa kaiba.
252. Masikini na mwanawe tajiri na mali yake.
253. Maskini hana kinyongo.
254. Mavi usioyala, wayawingiani kuku?
255. Mavi ya kale hayanuki.
256. Mbinu hufuata mwendo.
257. Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
258. Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo.
259. Mchagua jembe si mkulima.
260. Mchagua nazi hupata koroma.
261. Mchagua nazi si mfuaji.
262. Mchakacho ujao,halulengwi na jiwe.
263. Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo.
264. Mchamba kwingi mara ujitia dole.
265. Mcheka kilema hafi bila kumpata.
266. Mchele mmoja mapishi mengi.
267. Mchelea mwana kulia hulia yeye..
268. Mcheza hawi kiwete, ngoma yataka matao.
269. Mcheza kwao hutuzwa.
270. Mcheza na tope humrukia.
271. Mchezea mavi, hayaachi kumnuka.
272. Mchezea zuri, baya humfika.
273. Mchimba kisima hungia mwenyewe.
274. Mchonga mwiko hukimbiza mkono wake.
275. Mchuma janga hula na wakwao.
276. Mchumia juani,hulia kivulini.
277. Mdharau biu, hubiuka yeye.
278. Mdharau mwiba humchoma.
279. Meno ya mbwa hayaumani.
www.vitabutanzania.com
280. Mfa maji haachi kutapatapa.
281. Mfa maji hukamata maji.
282. Mficha uchi hazai.
283. Mfinyazi hulia gaeni.
284. Mfuata nyuki hakosi asali.
285. Mfukuzwa kwao hana pakwenda.
286. Mgaagaa na upwa hali ugari kande.
287. Mganga hajigangi.
288. Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.
289. Mgeni ni kuku mweupe.
290. Mgeni njoo mwenyeji apone.
291. Mgomba haushindwi na mkunguwe.
292. Mgonjwa haulizwi uji.
293. Miye nyumba ya udongo, sihimili vishindo.
294. Mjinga akierevuka mwerevu yupo mashakani.
295. Mjinga mpe kilemba utamuona mwendowe.
296. Mjumbe hauawi.
297. Mkaidi hafaidi mpaka siku ya idi.
298. Mkamatwa na ngozi ndiye mwizi.
299. Mkamia maji hayanywi.
300. Mkamia maji hayanywi.
301. Mkataa la mkuu huvunjika guu.
302. Mkataa wengi ni mchawi.
303. Mkataa ya Musa hupata ya Firauna.
304. Mke ni nguo, mgomba kupalilia.
305. Mkono moja hauchinji ng'ombe.
306. Mkono moja haulei mwana.
307. Mkono mtupu haulambwi.
308. Mkono usioweza kuukata,ubusu.
www.vitabutanzania.com
309. Mkosa kitoweo humangiria.
310. Mkuki kwa nguruwe, kwa mwanadamu uchungu.
311. Mkulima ni mmoja walaji ni wengi.
312. Mla cha mwenziwe na chake huliwa.
313. Mla cha uchungu na tamu hakosi.
314. Mla kuku wa mwenziwe miguu humwelekea.
315. Mla mbuzi hulipa ngombe.
316. Mla mla leo mla jana kala nini?
317. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
318. Mlala na maiti haachi kulia lia.
319. Mlenga jiwe kundini hajui limpataye.
320. Mlimbua nchi ni mwananchi.
321. Mnyamaa kadumbu.
322. Mnywa maji kwa mkono mmoja,Kiu yake i pale pale.
323. Moja shika, si kumi nenda urudi.
324. Moto hauzai moto.
325. Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
326. Mpanda ngazi hushuka.
327. Mpanda ovyo hula ovyo.
328. Mpemba akipata gogo hanyii chini.
329. Mpemba hakimbii mvua ndogo.
330. Mpende akupendae asiyekupenda achana naye.
331. Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe.
332. Mpofuka ukongweni,hapotewi na njia.
333. Msafiri kafiri.
334. Msafiri masikini ajapokuwa sultani.
335. Msasi haogopi mwiba.
336. Msema kweli hukimbiwa na rafiki zake.
337. Msema pweke hakosi.
www.vitabutanzania.com
338. Mshika kisu, hashiki makalini.
339. Mshale kwenda msituni haukupotea.
340. Mshoni hachagui nguo.
341. Msi bahati, habahatishi.
342. Msi mbele, hana nyuma.
343. Msishukuru mja, hamshukuru Molawe.
344. Msitukane wagema na ulevi ungalipo.
345. Msitukane wakunga na uzazi ungalipo.
346. Mstahimilivu hula mbivu.
347. Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
348. Mtaka lake hasindwi.
349. Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba.
350. Mtaka unda haneni.
351. Mtaka uzuri hudhurika.
352. Mtaka yote hukosa yote.
353. Mtegemea nundu haachi kunona.
354. mtegemea nundu, haachi konona.
355. Mtego bila ya chambo, haunasi.
356. Mtembezi hula miguu yake.
357. Mteuzi heshi tamaa.
358. Mti hauwendi ila kwa nyenzo.
359. Mtondoo haufi maji.
360. Mtoto akililia wembe mpe.
361. Mtoto umleyavyo ndivyo akuavyo.
362. Mtoto wa nyoka ni nyoka.
363. Mtu hakatai mwito,hukata aitwalo.
364. Mtu hujikuna ajipatapo.
365. Mtu huulizwa amevaani ,haulizwi amekulani.
366. Mtumai cha ndugu hufa masikini.
www.vitabutanzania.com
367. Mtumi wa kunga haambiwi maana.
368. Mtumikie kafiri upate mradi wako.
369. Mtupa jongoo hutupa na mti wake.
370. Muhitaji khanithi walau kana rijaali.
371. Muiba yai leo kesho hua mwizi wa ng'ombe.
372. Mume wa mama ni baba.
373. Mungu hamfichi mnafiki.
374. Mungu si asumani.
375. Muonja asali haonji mara moja.
376. Muuza sanda, mauti kwake harusi.
377. Mvua nguo, huchutama.
378. Mvumbika changa hula mbovu.
379. Mvumbika pevu hula mbivu na mvumbika changa hula mbovu.
380. Mvungu mkeka.
381. Mvunja nchi ni mwananchi.
382. Mvuvi ajuwa pweza alipo.
383. Mwacha asili ni mtumwa.
384. Mwamba na wako hukutuma umwambiye.
385. Mwamini Mungu si mtovu.
386. Mwana maji wa kwale kufa maji mazowea.
387. Mwana mkuwa nawe ni mwenzio kama wewe.
388. Mwana simba ni simba.The child of lion is a lion.
389. Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura.
390. Mwana wa mtu ni kizushi, akizuka, zuka naye.
391. Mwanga mpe mtoto kulea.
392. Mwangaza mbili moja humponyoka.
393. Mwanzo kokochi mwisho nazi.
394. Mwanzo wa chanzo ni chane mbili.
395. Mwanzo wa ngoma ni lele.
www.vitabutanzania.com
396. Mwapiza la nje hupata la ndani.
397. Mwekaji kisasi haambiwi mwerevu.
398. Mwenda bure si mkaa bure,huenda akaokota.
399. Mwenda mbio hujikwa kidole.
400. Mwenda omo na tezi marejeo ni ngamani.
401. Mwenda pole hajikwai.
402. Mwenda wazimu hapewi panga.
403. Mwenda wazimu hapoi, bali hupata nafuu.
404. Mwenye haja hwenda chooni.
405. Mwenye kelele hana neno.
406. Mwenye kovu usidhani kapowa.
407. Mwenye kubebwa hujikaza.
408. Mwenye kuchinja hachelei kuchuna.
409. Mwenye kuumwa na nyoka akiona jani hushtuka.
410. Mwenye macho haambiwi tazama.
411. Mwenye mdomo hapotei.
412. Mwenye nguvu mpishe.
413. Mwenye njaa hana miko.
414. Mwenye pupa hadiriki kula tamu.
415. Mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
416. Mwenye shoka hakosi kuni.
417. Mwenye tumbo ni tumbole, angafunga mkaja.
418. Mwenzako akinyolewa wewe tia maji.
419. Mwibaji na watwana, mlifi ni mwungwana.
420. Mwili wa mwenzio ni kando ya mwilio.
421. Mwizi hushikwa na mwizi mwenziwe.
422. Mwomba chumvi huombea chunguche.
423. Mwosha hadhuru maiti.
424. Mwosha huoshwa.
www.vitabutanzania.com
425. Mwosha husitiri maiti.
426. Mzaha,mzaha, mara hutumbuka usaha.
427. Mzazi haachi ujusi.
428. Mzigo usiouweza unaubebea nini?
429. Mzigo Wa mwenzio ni kanda Ia usufi.
430. Mzika pembe ndiye mzua pembe.
431. Mzowea kutwaa, kutoa ni vita.
432. Mzowea vya kunyonga, vya kuchinja haviwezi.
433. Mzungu Wa kula hafundishwi mwana.
434. Nahodha wengi, chombo huenda mrama.
435. Nani kama mama?
436. Natuone ndipo twambe, kusikia Si kuona.
437. Nazi haishindani na jiwe.
438. Nazi mbovu harabu ya nzima.
439. Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu.
440. Ndege mwigo hana mazowea.
441. Ndevu sio shani, hata beberu anazo.
442. Ndugu chungu, jirani mkungu.
443. Ndugu mwui afadhali kuwa naye.
444. Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime, wakipatana chukua kikapu ukavune.
445. Ngoja! ngoja? huumiza matumbo.
446. Ngoma ivumayo haidumu.
447. Ngoma ivumayo haikawii kupasuka.
448. Ngoma ya kitoto, haikeshi.
449. Ng'ombe avunjikapo guu hurejea zizini.
450. Ng'ombe haelemewi na nunduye.
451. Ngombe wa Maskini hazai.
452. Ngozi ivute ili maji. ( Udongo upate uli maji )
453. Nguo ya kuazima, Haistiri matako.
www.vitabutanzania.com
454. Nia njema ni tabibu, nia mbaya huharibu.
455. Nifae na mvua nikufae na jua.
456. Nimekula asali udogoni, utamu ungali gegoni.
457. Nimekupaka wanja, wewe wanipaka pilipili.
458. Nimerejesha kikombe na kisahani chake.
459. Njia ya muongo fupi.
460. Njia ya mwongo ni fupi.
461. Njia ya siku zote haina alama.
462. Nta Si asali; nalikuwa nazo Si uchunga.
463. Nyani haoni kundule, huliona la mwenziwe.
464. Nyani haoni kundule.
465. Nyimbo mbaya haibembelezewi mtoto.
466. Nyimbo ya kufunzwa haikeshi ngoma.
467. Nyongeza huenda kwenye chungu.
468. Nyota njema huonekana asubuhi.
469. Nyumba usiyolala ndani huijui ila yake.
470. Nyumba ya udongo haihimili vishindo.
471. Nzi kufa juu ya kidonda Si haramu. (Jihadi ya nzi, kufa kidondani)
472. Ondoa dari uwezeke paa.
473. Pabaya pako Si pema pa mwenzako.
474. Padogo pako Si pakubwa pa mwenzako.
475. Painamapo ndipo painukapo.
476. Paka akiondoka, panya hutawala.
477. Paka hakubali kulala chali.
478. Paka hashibi kwa wali, matilabaye ni panya.
479. Paka wa nyumba haingwa.
480. Panapo wengi hapaharibiki neno.
481. Papo kwa papo kamba hukata jiwe.
482. Pele hupewa msi kucha.
www.vitabutanzania.com
483. Pema usijapo pema; ukipema Si pema tena.
484. Penye kuku wengi usimwage mtama.
485. Penye mafundi, hapakosi wanafunzi.
486. Penye mbaya wako, hapakosi mwema wako/na mwema wako hakosi.
487. Penye miti hakuna wajenzi.
488. Penye nia pana njia.
489. Penye urembo ndipo penye urimbo.
490. Penye wazee haliharibiki neno.
491. Penye wengi pana mengi.
492. Penye wengi pana Mungu.
493. Pilipili usoila, wewe inakuwashia nini?
494. Pole pole ndio mwendo.
495. Pwagu hupata pwaguzi.
496. Radhi ni bora kuliko mali .
497. Radhi za wazee, ni fimbo.
498. Sahani iliyofunikwa, kilichomo kimesitirika.
499. Sahau ni dawa ya Waja.
500. Samaki mmoja akioza, huoza wote.
501. Samaki mpinde angali mbichi.
502. Shida haina hodi.
503. Shida huzaa maarifa.
504. Shika! Shika! na mwenyewe uwe nyuma.
505. Shimo Ia ulimi mkono haufutiki.
506. Shoka lisilo mpini halichanji kuni.
507. Si kila king'aacho ni dhahabu.
508. Si kila mwenye makucha huwa simba.
509. Si Mungu mtupu na mkono wa mtu.
510. Sikio halilali na njaa.
511. Sikio halipwani kichwa. (Sikio halipiti kichwa).
www.vitabutanzania.com
512. Sikio Ia kufa halisikii dawa.
513. Siri ya mtungi aijuaye ni kata.
514. Sitaacha kula mkate kwa kuogopa kiungulia.
515. Siku njema huonekana asubuhi.
516. Siku utakayokwenda uchi, ndiyo siku utakayokutana na mkweo.
517. Siku ya kufa nyani, miti yote huteleza.
518. Siku za mwizi, arubaini.
519. Simba mwenda kimya (pole) ndiye mla nyama.
520. Simbiko haisimbuki ila kwa msukosuko.
521. Sio shehe bali ni shehena.
522. Siri ya maiti aijuaye muosha.
523. Sitafuga ndwele na waganga tele.
524. Sitapiki nyongo harudi haramba.
525. Subira ni ufunguo Wa faraja.
526. Sumu mpe paka, mbuzi utamdhulumu.
527. Sumu ya neno ni neno.
528. Tabia ni ngozi ya mwili.
529. Tamaa mbele, mauti nyuma.
530. Taratibu ndio mwendo.
531. Tawi kavu kuanguka si ajabu.
532. Teke Ia kuku halimuumizi mwanawe
533. Tonga si tuwi
534. Tunda jema halikawii mtini.
535. Ucheshi wa mtoto ni anga Ia nyumba.
536. Ujuzi hauzeeki.
537. Uchungu wa mwana, aujue mzazi.
538. Udongo uwahi ungali maji (Udongo upate uli maji)
539. Udugu wa nazi hukutania chunguni (Udugu wa nazi hukutana pakachani)
540. Uji hajauonja, tayari ushamuunguza
www.vitabutanzania.com
541. Ukenda kwa wenye chongo, fumba lako jicho.
542. Ukimpa shubiri huchukua pima.
543. Ukimuiga tembo kunya, utapasuka mkundu.
544. Ukimwamsha alolala utalala weye.
545. Ukinyofoa mnofu, ukumbuke kuguguna mfupa.
546. Ukiona kwako kunaungua kwa mwenzako kunateketea.
547. Ukiona moshi, chini kuna moto.
548. Ukiona neno, usiposema neno, hutapatikana na neno.
549. Ukiona vinaelea, vimeundwa.
550. Ukiona zinduna, na ambari iko nyuma.
551. Ukistahi mke ndugu, huzai nae.
552. Ukitaja nyoka, shika fimbo mkononi.
553. Ukitaka kula nguruwe, chagua aliye nona.
554. Ukitaka salama ya dunia, zuia ulimi wako.
555. Ukiujua wa mbele, nina ujua wa nyuma.
556. Ukupigao ndio ukufunzao.
557. Ukuukuu wa kamba Si upya wa ukambaa.
558. Ulimi hauna mfupa.
559. Ulimi unauma kuliko meno.
560. Ulipendalo hupati, hupata ujaaliwalo.
561. Ulivyoligema, utalinywa.
562. Umeadimika kama la jogoo.
563. Umegeuka mung'unye waharibika ukubwani.
564. Umejigeuza pweza, unajipalia makaa?
565. Umekuwa bata akili kwa watoto?
566. Umekuwa nguva, huhimili kishindo?
567. Umeruka mkojo unakanyaga mavi.
568. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
569. Unajenga kwa mwenzio na kwako kunaporomoka!!
www.vitabutanzania.com
570. Unakuja juu kama moto wa kifuu.
571. Unamlaumu mwewe, kipanga yuwesha kuku.
572. Ungalijua alacho nyuki, usingalionja asali.
573. Ushikwapo shikamana (Ukibebwa usijiachie).
574. Usiache kunanua kwa kutega.
575. Usiache mbachao kwa msala upitao.
576. Usiache tawi kabla ya kushika tawi.
577. Usiandikie mate na wino ungalipo
578. Usicheze na simba, ukamtia mkono kinywani.
579. Usijifanye kuku mweupe.
580. Usikaange mbuyu ukawaachia wenye meno
581. Usile na kipofu ukamgusa rnkono.
582. Usimgombe mkwezi, nazi imeliwa na mwezi.
583. Usiniache njia panda.
584. Usinikumbushe kilio matangani.
585. Usinipake mafuta kwa nyuma ya chupa.
586. Usinivishe kilemba cha ukoka.
587. Usione simba kapigwa na mvua.
588. Usipoziba ufa utajenga ukuta.
589. Usisafirie nyota ya mwenzio.
590. Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha.
591. Usishindane na Kari; Kari ni mja wa Mungu.
592. Usitukane wagema na ulevi ungalipo.
593. Usitukane wakunga na uzazi 'ungalipo.
594. Utakosa mtoto na maji ya moto.
595. Usiyavuke maji usiyoweza kuyaoga.
596. Utaula na chua kwa uvivu wa kuchagua.
597. Vita havina macho.
598. Vita si lele mama.
www.vitabutanzania.com
599. Vita vya panzi, neema ya kunguru
600. Waarabu wa pemba, hujuana kwa vilemba
601. Wache waseme.
602. Wafadhilaka wapundaka.
603. Wagombanao ndio wapatanao.
604. Watu wanahisabu nazi, wewe unahisabu makoroma.
605. Wapiganapo tembo wawili ziumiazo ni nyasi.
606. Watetea ndizi, mgomba si wao.
607. Wazuri haweshi.
608. Wema hauozi..
609. wengi wape.
610. Zinguo la mtukufu, ni ufito.















www.vitabutanzania.com
NAHAU MIA TATU THEMANINI NA NNE(384)

1.Adhabu ya kaburi aijua maiti,
2.Akiba haiozi,
3.Asifuye mvuwa imemnyea.
4.Akili nyingi huondowa maarifa.
5.Asiye kubali kushindwa si mshindani.
6.Atangaye na jua hujuwa.
7.Asiye kuwapo na lake halipo.
8.Avumaye baharini papa kumbe wengi wapo.
9.Baada ya dhiki faraja.
10.Baniani mbaya kiatu chake dawa.
11.Bendera hufuata upepo.
12.Bilisi wa mtu nimtu.
13.Chamlevi huliwa na mgema.
14.Chanda chema huvikwa pete.
15.Chombo cha kuzama hakina usukani
16.Chovya - chovya yamaliza buyu la asali.
17.Dalili ya mvua mawingu.
18.Damu nzito kuliko maji.
19.Dawa ya moto ni moto
20.Dua la kuku halimpati mwewe.
21.Fadhila ya punda ni mateke
22.Fimbo ya mbali hayiuwi nyoka
23.Fuata nyuki ule asali.
24.Fumbo mfumbe mjinga mwerevu huligangua.
25.Ganda la mua la jana chungu kaona kivuno.
26.Haba na haba hujaza kibaba.
27.Hapana marefu yasio na mwisho.
28.Hakuna siri ya watu wawili.
www.vitabutanzania.com
29.Haraka haraka haina baraka.
30.Hasira, hasara.
31.Heri kufa macho kuliko kufa moyo.
32.Heri kujikwa kidole kuliko ulimi.
33.Hiari ya shinda utumwa.
34.Hucheka kovu asiye kuwa na jeraha.
35.Ihsani (hisani)haiozi.
36.Ikiwa hujui kufa,tazama kaburi.
37.Jina jema hungara gizani.
38.Jino la pembe si dawa ya pengo.
39.Jitihadi haiondoi kudura.
40.Jogoo la shamba haliwiki mjini
41.Kafiri akufaye si Isilamu asiyekufa.
42.Kamba hukatika pabovu.
43.Kanga hazai ugenini.
44.Kawaida ni kama sheria.
45.Kawia ufike.
46.Kazi mbaya siyo mchezo mwema.
47.Kelele za mlango haziniwasi usingizi.
48.Kenda karibu na kumi.
49.Kiburi si maungwana.
50.Kichango kuchangizana.
51.Kidole kimoja hakivunji chawa.
52.Kingiacho mjini si haramu.
53.Kikulacho ki nguoni mwako.
54.Kila chombo kwa wimblile.
55.Kila mlango na ufunguwo wake.
56.Kila mtoto na koja lake.
57.Kila mwamba ngoma ,ngozi huivutakwake.
www.vitabutanzania.com
58.Kila ndege huruka na mbawa zake.
59.Kilio huanza mfiwa ndipo wa mbaliwakainga
60.Kimya kingi kina mshindo mkubwa.
61.Kinga na kinga ndipo moto uwakapo.
62.Kinyozi hajinyoi.
63.Kinywa ni jumba la maneno.
64.Kipendacho moyo ni dawa.
65.Kipya kinyemi ingawa kidonda.
66.Kisebusebu na roho kipapo.
67.Kisokula mlimwengu,sera nale.
68.Kitanda usicho kilala hujui kunguni wake.
69.Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua.
70.Kiwi cha yule ni chema cha;hata ulimwenguuwishe.
71.Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.
72.Konzo ya maji haifumbatiki.
73.Kosa moja haliachi mke.
74.Kozi mwandada ,kulala na njaa kupenda.
75.Kuagiza kufyekeza
76.Kuambizana kuko kusikilizana hapana.
77.Kumcha M'ngu si kilemba cheupe.
78.Kuchamba kwingi,kuondoka na mavi.
79.Kufa kufaana.
80.Kufa kwa jamaa, harusi.
81.Kufa kwa mdomo,mate hutawanyika.
82.Kuishi kwingi ni kuona mengi.
83.Kujikwa si kuanguka,bali ni kwenda mbele.
84.Kukopa harusi kulipa matanga.
85.Kuku havunji yai lake.
86.Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
www.vitabutanzania.com
87.Kula kutamu ,kulima mavune.
88.Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana.
89.Kunako matanga kume kufa mtu.
90.Kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake.
91.Kupanda mchongoma ,kushuka ngoma.
92.Kupoteya njia ndiyo kujua njia.
93.Kutoa ni moyo usambe ni utajiri.
94.Kutu kuu ni la mgeni.
95.Kuharibika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.
96.Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaahuenda kilio.
97.Kwenda mbio siyo kufika.
98.Kwenye miti mingi hakuna wajenzi.
99.La kuvunda(kuvunja) halina rubani.
100.La kuvunda (kuvunja)halina ubani.
101.Lake mtu halimtapishi bali humchefusha.
102.Leo ni leo asemaye kesho ni mwongo.
103.Liandikwalo ndiyo liwalo.
104.Lila na fila hazitangamani.
105.Lipitalo ,hupishwa .
106.Lisemwalo lipo,ikiwa halipo laja.
107.Lisilokuwapo moyoni,halipo machoni.
108.Maafuu hapatilizwi.
109.Macho hayana pazia.
110.Mafahali wawili hawakai zizi moja.
111.Maiti haulizwi sanda.
112.Maji hufuata mkondo.
113.Maji huteremka bondeni,hayapandi mlima.
114.Maji ukiyavuliya nguo huna budi kuyaogelea.
115.Maji usiyoyafika hujui wingi wake.
www.vitabutanzania.com
116.Maji ya kifufu ni bahari ya chungu.
117.Maji yakija hupwa.
118.Mpanda ngazi hushuka.
119.Maji yakimwagika hayazoleki.
120.Majumba makubwa husitiri mambo.
121.Majuto ni mjukuu.
122.Manahodha wengi chombo huenda mrama.
123.Maneno makali hayavunji mfupa.
124.Maneno mema hutowa nyoka pangoni.
125.Masikini akipata matako hulia mbwata.
126.Masikini haokoti,akiokota huambiwa kaiba.
127.Masikini na mwanawe tajiri na mali yake. 128.Mavi usioyala,wayawingiani kuku
129.Mavi ya kale hayanuki.
130.Mbinu hufuata mwendo.
131.Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
132.Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo.
133.Mchagua jembe si mkulima.
134.Mchagua nazi hupata koroma.
135.Mchakacho ujao,haulengwi na jiwe.
136.Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo.
137.Mchelea mwana kulia hulia yeye..
138.Mchele moja mapishi mengi.
139.Mcheka kilema hafi bila kumpata.
140.Mcheza hawi kiwete,ngoma yataka matao.
141.Mcheza kwao hutuzwa.
142.Mcheza na tope humrukia.
143.Mchezea zuri ,baya humfika.
144.Mchimba kisima hungia mwenyewe.
145.Mchonga mwiko hukimbiza mkono wake.
www.vitabutanzania.com
146.Mchovya asali hachovi mara moja.
147.Mchuma janga hula na wakwao.
148.Mchumia juani,hula kivulini.
149.Mdharau biu,hubiuka yeye.
150.Meno ya mbwa hayaumani.
151.Mfa maji hukamata maji.
152.Mficha uchi hazai.
153.Mfinyazi hulia gaeni.
154.Mfuata nyuki hakosi asali.
155.Mfukuzwa kwao hana pakwenda.
156.Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
157.Mganga hajigangui.
158.Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.
159.Mgeni ni kuku mweupe.
160.Mgeni njoo mwenyeji apone.
161.Mgonjwa haulizwi uji.
162.Miye nyumba ya udongo ,sihimili vishindo
163.Mjinga akierevuka mwerevu yupomashakani.
164.Mjumbe hauawi.
165.Mkamatwa na ngozi ndiye mwizi.
166.Mkamia maji hayanywi.
167.Mkata (masikini) hana kinyongo.
168.Mke ni nguo ,mgomba kupalilia.
169.Mkono moja hauchinji ngombe.
170.Mkono moja haulei mwana.
171.Mkono mtupu haulambwi.
172.Mkono usioweza kuukata,ubusu.
173.Mkosa kitoweo humangiria.
174.Mkuki kwa nguruwe mtamu,kwa mwanadamumchungu.
www.vitabutanzania.com
175.Mkulima ni mmoja walaji ni wengi.
176.Mla cha mwenziwe na chake huliwa.
177.Mla cha uchungu na tamu hakosi.
178.Mla kuku wa mwenziwe miguu humwelekeya.
179.Mla mbuzi hulipa ngombe.
180.Mla mla leo mla jana kala nini?
181.Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
182.Mlenga jiwe kundini hajui limpataye.
183.Mlimbua nchi ni mwananchi.
184.Mnyamaa kadumbu.
185.mnywa maji kwa mkono moja,Kiu yake i palepale.
186.Moja shika,si kumi nenda urudi.
187.Moto hauzai moto.
188.Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
189.Mpanda ovyo hula ovyo.
190.Mpemba akipata gogo hanyii chini.
191.Mpemba hakimbii mvua ndogo.
192.Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe
193.Mpofuka ukongweni,hapotewi na njia.
194.Msafiri masikini ajapokuwa sultani.
195.Mwindaji haogopi mwiba.
196.Msema pweke hakosi.
197.Mshale kwenda msituni haukupotea.
198.Mshoni hachagui nguo.
199.Msitukane wagema na ulevi ungalipo.
200.Msitukane wakunga na uzazi ungalipo.
201.Mstahimilivu hula mbivu.
202.Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
203.Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba.
www.vitabutanzania.com
204.Mtaka unda haneni.
205.Mtaka yote hukosa yote.
206.Mtegemea nundu haachi kunona.
207.Mtembezi hula miguu yake.
208.mteuzi hashi tamaa.
209.Mti hauwendi ila kwa nyenzo.
210.Mtondoo haufi maji.
211.Mtoto akililia wembe mpe.
212.Mtoto umleyavyo ndivyo akuavyo.
213.Mtoto wa nyoka ni nyoka.
214.Mtu hakatai mwito,hukata aitwalo.
215.Mtu hujikuna ajipatiapo.
216.Mtu huulizwa amevaanini ,haulizwi amekulanini.
217.Mtumai cha ndugu hufa masikini.
218.Mtumi wa kunga haambiwi maana.
219.Mtumikie kafiri upate mradi wako.
220.Mtupa jongoo hutupa na mti wake.
221.Mume wa mama ni baba.
222.Mungu hamfichi mnafiki.
223.Mvumbika changa hula mbovu.
224.Mvungu mkeka.
225.Mvunja nchi ni mwananchi.
226.Mvuvi ajuwa pweza alipo.
227.Mwacha asili ni mtumwa.
228.Mwamba na wako hukutuma umwambiye.
229.Mwamini Mungu si mtovu.
230.Mwana mkaidi hafaidi mpaka siku ya idi.
231.Mwana maji wa kwale kufa maji mazowea.
232.Mwana mkuwa nawe ni mwenzio kamawewe.
www.vitabutanzania.com
233.Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura.
234.Mwana simba ni simba.
235.Mwanga mpe mtoto kulea.
236.Mshika mawili mbili moja humponyoka.
237.Mwanzo kokochi mwisho nazi.
238.Mwanzo wa chanzo ni chane mbili.
239.Mwanzo wa ngoma ni lele.
240.Mwapiza la nje hupata la ndani.
241.Mwekaji kisasi haambiwi mwerevu.
242.Mwenda bure si mkaa bure,huendaakaokota.
243.Mwenda mbio hujikwa kidole.
244.Mwenda tezi na omo marejeo ngamani.
245.Mwenye kelele hana neno.
246.Mwenye kovu usidhani kapowa.
247.Mwenye kubebwa hujikaza(Hujishikilia).
248.Mwenye kuchinja hachelei kuchuna.
249.Mwenye kuumwa na nyoka akiona janihushtuka.
250.Mwenye macho haambiwi tazama.
251.Mwenye nguvu mpishe.
252.Mwenye njaa hana miiko
253.Mwenye pupa hadiriki kula tamu.
254.Mwenye shibe hamjui mwenye njaa
255.Mwenye shoka hakosi kuni.
256.Mwenye tumbo ni tumbole, angafunga mkaja.
257.Mwenzako akinyolewa wewe tia maji.
258.Mwibaji na watwana, mlifi ni mwungwana
259.Mwili wa mwenzio ni kando ya mwilio.
260.Mwizi hushikwa na mwizi mwenziwe
261.Mwomba chumvi huombea chunguche.
www.vitabutanzania.com
262.Mwosha hadhuru maiti.
263.Mwosha huoshwa.
264.Mwosha husitiri maiti.
265.Mzaha,mzaha, hutumbuka usaha
266.Mzazi haachi ujusi.
267.Mzigo Wa mwenzio ni kanda Ia usufi.
268.Mzika pembe ndiye mzua pembe.
269.Mzowea kutwaa, kutoa ni vita.
270.Mzowea kunyonga, kuchinja hawezi
271.Mzungu Wa kula hafundishwi mwana.
272.Nahodha wengi, chombo huenda mrama.
273.Natuone ndipo twambe, kusikia Si kuona
274.Nazi mbovu harabu ya nzima.
275.Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu
276.Ndege mwigo hana mazowea.
277.Ndugu chungu, jirani mkungu
278.Ndugu mwui afadhali kuwa naye.
279.Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime,wakipatana chukua kikapu ukavune.
280.Ngoja! ngoja? huumiza matumbo.
281.Ngoma ivumayo haidumu.
282.Ngoma ivumayo haikawii kupasuka.
283.Ngozi ivute ili maji.
284.Nia njema ni tabibu, nia mbaya huharibu
285.Nifae na mvua nikufae na jua
286.Nimekula asali udogoni, utamu ungali gegoni
287.Nimekupaka wanja, wewe wanipaka pilipili.
288.Njia ya mwongo fupi.
289.Njia ya siku zote haina alama.
290.Ng'ombe avunjikapo guu hurejea zizini.
www.vitabutanzania.com
291.Ng'ombe haelemewi na nunduye.
292.Nta Si asali; nalikuwa nazo Si uchunga
293.Nyani haoni kundule, huliona la mwenziwe
294.Nyimbo ya kufunzwa haikeshi ngoma.
295.Nyumba usiyolala ndani huijui ila yake.
296.Nyumba ya udongo haihimili vishindo
297.Nzi kufa juu ya kidonda Si haramu
298.Pabaya pako Si pema pa mwenzako
299.Padogo pako Si pakubwa pa mwenzako
300.Painamapo ndipo painukapo.
301.Paka akiondoka, panya hutawala.
302.Paka hakubali kulala chali
303.Paka wa nyumba Hawindwi.
304.Panapo wengi hapaharibiki neno.
305.Papo kwa papo kamba hukata jiwe.
306.Pele hupewa asiye na kucha
307.Pema usijapo pema; ukipema Si pema tena.
308.Penye kuku wengi hapamwagwi mtama.
309.Penye mafundi, hapakosi wanafunzi.
310.Penye mbaya wako, hapakosi mwema wako/namwema wako hakosi.
311.Penye miti hakuna wajenzi.
312.Penye nia pana njia.
313.Penye urembo ndipo penye urimbo.
314.Penye wazee haliharibiki neon
315.Penye wengi pana mengi.
316.Penye wengi pana Mungu.
317.Pilipili usozila zakuwashiani?
318.Pofu hasahau mkongoja wake.
319.Pwagu hupata pwaguzi.
www.vitabutanzania.com
320.Radhi ni bora kuliko mali
321.Sahani iliyofunikwa, kilichomo kimesitirika.
322.Samaki mmoja akioza, huoza wote
323.Shika! Shika! na mwenyewe nyuma
324.Shimo Ia ulimi mkono haufutiki.
325.Shoka lisilo na mpini halichanji kuni.
326.Si kila mwenye makucha huwa samba
327.Sikio halilali na njaa
328.Sikio halipiti kichwa.
329.Sikio Ia kufa halisikii dawa.
330.Siku njema huonekana asubuhi.
331.Siku utakayokwenda uchi, ndiyo sikuutakayokutana na mkweo.
332.Simba mwenda kimya(pole) ndiye mla nyama.
333.Simbiko haisimbuki ila kwa msukosuko.
334.Sitafuga ndwele na waganga tele.
335.Subira ni ufunguo Wa faraja.
336.Subira yavuta heri, huleta kilicho mbali.
337.Sumu ya neno ni neno.
338.Tamaa mbele, mauti nyuma.
339.Taratibu ndiyo mwendo.
340.Teke Ia kuku halimwumizi mwanawe
341.Tonga si tuwi
342.Ucheshi wa mtoto ni anga Ia nyumba
343.Uchungu wa mwana, aujua mzazi.
344.Udongo uwahi ungali maji
345.Udugu wa nazi hukutania chunguni
346.Ukenda kwa wenye chongo, vunja lako jicho.
347.Ukiona kwako kunaungua kwa mwenzakokunateketea.
348.Ukiona neno, usiposema neno, hutapatikana naneno
www.vitabutanzania.com
349.Ukiona vinaelea, vimeundwa.
350.Ukiona zinduna, ambari iko nyuma
351.Ukipewa shibiri usichukue pima.
352.Ukupigao ndio ukufunzao.
353.Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni.
354.Ukitaja nyoka, shika fimbo mkononi.
355.. Ukitaka kula nguruwe, chagua aliyeno,na
356.Ukitaka uzuri sharti udhurike.
357.Ukuukuu wa kamba Si upya wa ukambaa
358.Ulimi hauna mfupa.
359.Ulimi unauma kuliko meno.
360.Ulipendalo hupati, hupata ujaliwalo.
361.Ulivyoligema utalinywa.
362.Umejigeuza pweza, unajipalia makaa?
363.Umekuwa bata akili kwa watoto?
364.Umekuwa jeta hubanduki?
365.Umekuwa nguva, huhimili kishindo?
366.Unamlaumu mwewe, kipanga yuwesha kuku.
367.Ungalijua alacho nyuki, usingalionja asali
368.Ushikwapo shikamana.
369.Usiache kunanua kwa kutega.
370.Usiache mbachao kwa msala upitao
371.Usicheze na simba, ukamtia mkono kinywani.
372.Usigombanee na mkwezi, nazi imeliwa na mwezi.
373.Usijifanye kuku mweupe.
374.Usikaange mbuyu ukawaachia wenye menowatafune.
375.Usile na kipofu ukamgusa rnkono.
376.Usimwamshe aliyelala utalala wewe.
377.Usinivishe kilemba cha ukoka.
www.vitabutanzania.com
378.Usipoziba ufa utajenga ukuta
379.Usisafiriye nyota ya mwenzio.
380.Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha.
381.Usishindane na Kari; Kari ni mja wa Mungu
382.Usitukane wagema na ulevi ungalipo.
383.Usitukane wakunga na uzazi 'ungalipo.
384.Usiyavuke maji usiyoweza kuyaoga.






















www.vitabutanzania.com
VITENDAWILI
1.Adui lakini po pote uendako yuko nawe.
2.Afahamu kuchora lakini hajui achoracho.
3.Afuma hana mshale.
4.Ajenga ingawa hana mikono.
5.Ajifungua na kujifunika.
6.Akitokea watu wote humwona.
7.Akitokea watu wote hunungunika na kuwa na huzuni.
8.Akivaa nguo hapendezi, akiwa uchi apendeza.
9.Alipita mtu ana bunda la mshale.
10.Alipita mtu mwenye kibandiko cha nguo.
11.Aliwa, yuala; ala, aliwa.
12.Amchukuapo hamrudishi.
13.Amefunika kote kwa blanketi lake jeusi.
14.Amefunua jicho jekundu.
15.Ameingia shimoni akiwa uchi, akatoka amevaa nguo nzuri.
16.Amejitwika mzigo mkubwa kuliko yeye mwenyewe.
17.Amekaa kimya na watoto wamemzunguka pande zote.
18.Amekula ncha mbili.
19.Amevaa joho kubwa kuliko yeye mwenyewe.
20.Anakuangalia tu wala halali au kutembea.
21.Anakula kila siku lakini hashibi na hatashiba.
22.Anakula lakini hajashiba na hatashiba milele.
23.Anakula lakini hashibi.
www.vitabutanzania.com
24.Anapendwa sana ingawaje ni mkali sana.
25.Anatoka kutembea, anakuja nyumbani anamwambia mama,"Nieleke".
26.Ashona mikeka wala hailali.
27.Askari wangu wote wamevaa kofia upande.
28.Askari wangu wote wamevaa mavazi meusi.
29.Asubuhi atembea kwa miguu mine, adhuhuri kwa miwili.
30.Atapanya mbegu nyingi sana lakini hazioti.
31.Atolewapo nje hufa.

B
32.Baba alinipa mfupa, nikautunza ukawa fahali.
33.Baba ameweka mkuki nje nikashindwa kuukwea, mdogo wangu akaukwea.
34.Babako akojoapo hunung'unika.
35.Babu amefunga ushanga shingoni.
36.Babu anakula ng'ombe, analea fupa linakuwa ng'ombe.
37.Babu hupiga kelele akojoapo.
38.Babu mkubwa ameangushwa na babu mdogo.
39.Babu, nyanya, mjomba, mama, baba na watoto, mna safari ya wapi?
40.Bak bandika, bak bandua.
41.Bawabu mmoja tu asiyeogopa chochote duniani.
42.Bibi kikongwe apepesa ufuta.
43.Bibi yake hutandikwa kila siku, lakini hatoroki.

C
www.vitabutanzania.com
44.Chakula kikuu cha mtoto.
45.Cha ndani hakitoki nje, cha nje hakiingii ndani.
46.Chang'aa chapendeza, lakini hakifikiwi.
47.Chatembea na hakijapata kupumzika hata nukta moja.
48.Cheupe chavunjika manjano yatokea.
49.Chumba change kina ukuta niondoa na kuusimika nitakapo.
50.Chungu change cha udongo hakipasuki kikianguka.
51.Chungu kikubwa sana chenye kifuniko kikubwa sana.

D
52.Dada yangu akitoka kwao harudi kamwe.
53.Dada yangu kaoga nusu.
54.Drrrrrh1 Ng'ambo.
55.Dume wangu amelilia machungani.

F
56. Fahali wa ng'ombe na mbuzi wadogo machungani.
57. Fika umwone umpendaye.
58. Fuko kajifukia, mkia kaacha nje.
59. Funga mizigo twende Kongo.

H
60.Hachelewi wala hakosei safari zake.
61.Haina miguu wala mikono, lakini, yabeba magogo.
www.vitabutanzania.com
62.Hakihitaji maji, wala udongo, wala chakula; lakini chamea.
63.Hakionekani wala hakishikiki.
64.Hakisimami, na kikisimama msiba.
65.Hakuchi wala hakuchwi.
66.Halemewi wala hachoki kubeba.
67.Hamwogopi mtu yeyote.
68.Hana mizizi, nimemkata mara nyingi lakini haachi kukua.
69.Haoni kinyaa.
70.Hapo nje panapita mtu mwenye miguu mirefu.
71.Hasemi, na akisema hatasahaulika.
72.Hasimamishwi akiwa na ghadhabu.
73.Hata inyeshe namna gani haifiki humu.
74.Hata jua likiwaka namna gani hakauki wala kupata joto.
75.Hata Mzungu ameshindwa.
76.Hauchagui chifu wala jumbe.
77.Hausimiki hausimami.
78.Hawa wanaingia hawa wanatoka.
79.Hesabu haihesabiki.
80.Huitumia kila siku lakini haiishi.
81.Huku kutamu, huku kutamu, katikati uchungu.
82.Huku unasikia "pa" Huku unasikia "pa!
83.Hula lakini hashibi.
84.Hulala tulalapo, huamka tuamkapo.
85.Humu mwetu tuko wanne tu, ukimwona wa tano mwue.
www.vitabutanzania.com
86.Huna macho lakini wakamata wanyama.
87.Hupanda mtini na mwenye kichaa wake.
88.Hutembea watatu.
89.Hutoka upesi sana lakini hasalimu.
90.Huwafanya watu wote walie.
91.Huwezi kukalia alipokalia msichana wangu mweusi.
92.Huzikwa mmoja, hufufuka mmoja, huzeeka wengi.

I
93.Inaonekana mara mbili katika dakika moja na mara moja tu katika mwaka.
94.Ini la ng'ombe huliwa hata na walioko mbali.

J
95.Jembe la Wangoni haliishi.
96.Je, unaweza, kukua ukampita mzee wako?
97.Jiwe litoalo maji.

K
98. Kaburi la mfalme lina milango miwili.
99. Kaka yangu anapanda darini na fimbo nyuma.
100.Kama kingekuwa mkuki, ungekuta kimekwisha kuua wote.
101.Kama unapenda, mbona usile?
102.Kanipa ngozi nikapikia, kanipa nyama nikala, kanipa mchuzi nikanywa, kanipa mfupa
nikautumia.
www.vitabutanzania.com
103.Kapanda mti pamoja na uchawi wake.
104.Kidimbwi kimezungukwa na majani.
105.Kikioza hutumiwa, kikiwa kichungu hakitumiwa.
106.Kila linapofika kwetu hutanguliza makelele.
107.Kila mtu atapitia malango huo.
108.Kila mtu hata mfalme huheshimu akipita.
109.Kila siku hupita njia hiyo hiyo bali arudipo hatumwoni.
110.Kileee! Hiki hapa.
111.Kilimsimamisha chifu njiani.
112.Kina mikono na uso lakini hakina uhai.
113.Kinaniita lakini sikioni.
114.Kisima cha Bimpai kina nyoka muwai, ndiye fisadi wa maji.
115.Kisima kidogo kimejaa changarawe.
116.Kitendawili change ukikitambua nitakupa hirizi.
117.Kiti cha dhahabu hakikaliwi na watu.
118.Kiti cha Sulatni hukaliwa na mwenyewe.
119.Kiti nyikani.
120.Kitu change asubuhi chatembea kwa miguu mine, saa sita kwa miguu miwili, jioni kwa
miguu mitatu.
121.Kiwanja kizuri lakini hakifai kuweka mguu.
122.Kombe ya Sultani I wazi.
123.Kondoo wangu amezaa kwa paja.
124.Kondoo wangu mnene kachafua njia nzima.
125.Kondoo za mtoto zamaliza mavuno.
www.vitabutanzania.com
126.Kufanya kwa ridhaa mojamoja.
127.Kuku wangu aliangua mayai jana, lakini si kuku wala ndege.
128.Kuku wangu amezalia miibani.
129.Kuku wetu hutagia mayai mikiani.
130.Kuna mlima mmoja usio pandika
131.Kuna mtu mwenye tumbo kubwa aliyesimama nje.
132.Kuna ziwa kubwa ambalo limekauka na limebakiza mizizi.
133.Kunguru akilia hulilia mirambo.
134.Kwenye msitu mkubwa Napata mti mmoja tu, lakini kwenye msitu mdogo naweza
kupata miwili.
135.Kwetu mishale na kwenu mishale.
136.Kwetu twalala tumesimama.

L
137.La mgambo limelia wakatoka weusi tu.
138.Likienda hulia, likirudi halilii.
139.Likitoka halirudi.
140.Liwali amekonda lakini hana mgaga.

M
141.Mama ametengeneza chakula lakini hakula.
142.Mbona kinakumeza lakini hakikuli?
143.Mbona mwakunjiana ngumi bila kupigana?
144.Mbona mwasimama na mikuki, mwapigana na nani?
www.vitabutanzania.com
145.Mchana "ti" usiku "ti".
146.Mdogo lakini humaliza gogo.
147.Mfalme amesimika mkuki wake hapa name nikausimika wangu kando yake, baadaye
hatukuitambulisha tena.
148.Mfalme hushuka kwa kelele.
149.Mfalme katikati lakini watumishi pembeni.
150.Mfalme wetu hupendwa sana, lakini wakati wa kumwona lazima umtoe nguo zote
kwanza.
151.Mhuni wa ulimwengu.
152.Mkanda mrefu wafka mpaka pwani.
153.Mke wangu mfupi, lakini huvaa nguo nyingi.
154.Mlango wa nyumba yangu uko juu.
155.Mlima mkubwa wapandwa kuanzia juu.
156.Mlimani sipandi.
157.Mlima umezuia kutazama kwa mjomba.
158.Mlima wa kupanda kwa mikono.
159.Mlima wa kwetu hupandwa na mfalme.
160.Mlima wa mwenyewe hupandwa na mwenyewe.
161.Mpini mmoja tu lakini majembe hayahesabiki.
162.Msitu ambao haulii hondohondo.
163.Mti mkubwa, lakini una matawi mawili tu.
164.Mti mnyanya mti kerekeche mti ah mti ah!.
165.Mti wangu una matawi kumi na mawili na kila tawi lina majani kadiri ya thelathini.
166.Mtoto asemea pangoni.
www.vitabutanzania.com
167.Mtu mdogo mwenye miguu mirefu ambaye aweza kutembea dunia nzima kwa dakika
tano.
168.Mvua hema na jua hema.
169.Mvua kidogo ng'ombe kaoga kichwa.
170.Mwadhani naenda lakini siendi.
171.Mwalimu analala na mwanafunzi wanamsomea.
172.Mwanamke mfupi hupiga kelele njiani.
173.Mwanamke mfupi hutengeneza pombe nzuri.
174.Mwanang'ang'a hulia mwituni.
175.Mwepesi, lakini aweza kuvunja nyumba za mji wote.
176.Mwezi wangu umepasuka.
177.Mzee Kombe akitoa machozi wote hufurahi.
178.Mzee Kombe akilia watu hufurahi.
179.Mzizi wa miti hutokea mbali.
180.Mzungu yuko ndani na ndevu ziko nje.

N
181.Naitumia ngazi hiyo kwa kupandia na kushukia.
182.Nakikimbilia lakini sikikuti.
183.Nakupa lakini mbona huachi kudai.
184.Nakwenda msituni na mdogo wangu, lakini yeye namwacha huko.
185.Nameza lakini sishibi.
186.Namkimbiza lakini simkuti.
187.Namlalia lakini halii.
www.vitabutanzania.com
188.Namwomba atangulie lakini hukataa kabisa.
189.Nanywa supu na nyama naitupa.
190.Napigwa na mvua na nyumba ipo.
191.Natembea juu ya miiba lakini hainichomi.
192.Natembea juu ya miiba lakini sichomwi.
193.Natembea na wenzangu lakini tukifika kwenye nyumba mimi hukaa mlangoni.
194.Natengeneza mafuta lakini nimepauka sana.
195.Natengeneza mbono lakini alama hazionekani.
196.Ndege wengi baharini.
197.Ndugu wawili wafanana sana, lakini hawatembeleani.
198.Ngoja nikumbuke.
199.Ng'ombe wa baba watelemka mtoni.
200.Ng'ombe wa babu huchezea miambani.
201.Ng'ombe za babu zikienda machungani hulia, zikirudi hazilii.
202.Ng'ombe za babu zinalala na mkia nje.
203.Ng'ombe wamechanganyika nikakosa wa kwangu.
204.Ng'ombe wangu ni weupe kwatoni.
205.Ng'ombe wangu wote hunywa maji isipokuwa mmoja.
206.Ngozi ndani nyama juu.
207.Nguo ivaliwayo kila siku isiyoingiwa na chawa.
208.Nikicheka kinacheka, nikinuna kinanuna.
209.Nikienda arudi, nikirudi aenda.
210.Niiita "baba" huitika "baba".
211.Nikija kwenye ndege wananifukuza, na nikienda kwenye wanyama hawanitaki.
www.vitabutanzania.com
212.Nikimpiga huyu huyu alia.
213.Nikimpiga mambusu.
214.Nikimwita hunijibu nani.
215.Nikipewa chakula nala bali natema.
216.Nikitembea walio wafu huniamkia na walio hai hukaa kimya.
217.Nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayupo.
218.Ni kitu gani ambacho kutoa ni kuongeza?
219.Nikitupa mshale wangu mchana huenda mbali sana, lakini niutupapo usiku hauendi
mbali.
220.Nikiwaambia ondokeni hukataa, lakini mjomba akitokea wote hukimbia.
221.Nilijenga nyumba yangu nikaiacha bila kuiezeka majani;lakini niliporudi nilikuta
imekwisha ezekwa majani.
222.Nilijenga nyumba yangu yenye mlango mmoja.
223.Nilimkata alafu nikamridhia.
224.Nilimtuma askari vitani akaniletea kondoo mweusi.
225.Nilipandia majanini nikashukia majanini.
226.Nilipigwa na tonge la ugali la moto nilipopita msituni.
227.Nilipitisha mkono wangu chini la ardhi, nikamshika beberu mkubwa sana.
228.Nilipoangalia kwenye magereza ya Wazungu, nikaona wameketi juu ya mabati.
229.Nilipofika msituni nilikuta chungu cha pure kinachemka.
230.Nilipoingia Rumi, alitoka mtu na wake kumi; kila mke na tundu kumi, kila tundu na
kuku
kumi; kila kuku na mayai kumi. Mayai, kuku, tundu, wake,
kumi kumi kumi. Wangapi walikwenda Rumi?
www.vitabutanzania.com
231.Nilipo, juu kuna miiba na chini vivyo hivyo; lakini sichomwi.
232.Nilipokuwa mchanga nilikuwa na kijikia lakini sasa sinacho.
233.Nilitembea na mwezangu naye hupita vichakani.
234.Nimechoma fimbo yangu pakabaki pa kushikia tu.
235.Nimefyeka mitende yote kiungani isipokuwa minazi miwili tu.
236.Nimejenga nyumba babu akaihamia kabla mimi sijahamia.
237.Nimekata mti, akaja samba mwekundu akaukalia.
238.Nimekata mti bara ukaangusha matawi pwani.
239.Nimekwenda na rafiki yangu kwa jirani, yeye akafika kabla yangu.
240.Nimemtahiri binti wangu akatoa damu mchana kutwa.
241.Nimempeleka kondoo wangu akatoa damu mchana kutwa.
242.Nimemtuma mtu kumwamkua mtu, yeye amekuja, Yule aliyetumwa hajaja.
243.Nimemwacha mzee kikongwe mtoni anangojea mgeni kulaki.
244.Nimempandikiza mti wangu ukapeleka matawi ng'ambo ya mto.
245.Nimesimama mbali nyikani lakini naonekani.
246.Nimetembea kitambo, kukumbuka sikufunga nyumba.
247.Nimetoka kutembea kutembea, nikashika ng'ombe mkia.
248.Nimetupa mshale angani wala sitambui utateremsha ndege wa namna gani.
249.Nimeweka ndizi yangu, asubuhi siioni.
250.Nimezaliwa na mguu mmoja.
251.Nimezungukwa na adui wengi, lakini siumizwi.
252.Nina kijiti change, nizidivyo kukikata ndivyo kizidivyo kuwa kirefu.
253.Nina kitu change kitumiwacho na wengine kuliko mimi.
254.Nina kitu kizuri sana nyumbani, lakini siwezi kukichukua.
www.vitabutanzania.com
255.Nina kitu nipendacho ambacho hata baba, mama, dada, kaka hata na mgeni
nimpendaye sana siwezi kumwazima.
256.Nina mwezi ndani ya bakuli.
257.Nina ng'ombe wangu nisipomshika mkia hali majani.
258.Nina nyumba yangu imezungukwa na mifupa.
259.Nina pango langu lilojaa mawe.
260.Nina watoto wangu hamsini na wote nimewavisha visibau vyeupe.
261.Nina watoto watatu, mmoja akitoka kazi haifanyiki.
262.Nina badilika umbo langu baada ya kila muda mfupi.
263.Ninachimba mizizi ya mti usio na mizizi.
264.Ninacho, nakitumia, lakini kila nikitumiapo, sikiharibu ila nakipa rangi.
265.Ninakula vitu vyote vinono lakini sikui wala sinenepi.
266.Ninakwenda naye na kurudi naye.
267.Ninao mlima ambao una msitu kileleleni tu.
268.Nitokeapo kila mmoja asema namtazama yeye tu.
269.Njia yapitwa siku zote lakini haina alama.
270.Njoo hapa nije hapo.
271.Nne nne mapaka pwani.
272.Nusu mfu nusu hai.
273.Nyama ndogo imewashibisha wengi wala isiishe.
274.Nyama ya Reale haijai kikombe.
275.Nyanya yako ana huruma kukubeba ulalapo.
276.Nyumba yangu ina makuti tele, lakini mvua ikinyesha huvuja.
277.Nyumba yangu ina milango mimgi.
www.vitabutanzania.com
278.Nyumba yangu ina nguzo moja.
279.Nyumba yangu kubwa, haina mlango.
280.Nyumba yangu kubwa, haina taa.
281.Nyumba yangu kubwa hutembelewa mgongoni.

O
282.Oh!
283.Ondoka nikae.

P
284.Paa alipenga hata pua ikapasuka.
285.Palikuwepo watu watatu wakivuka mto. Mmoja alivuka pasipo kukanyaga maji wala
kuyaona; wa pili aliyaona maji
lakini alivuka bila kuyakanyaga; wa tatu aliyaona na
kuyakanyaga alipovuka. Ni nani hawa?
286.Panda ngazi polepole.
287.Para hata Maka.
288.Pete ya mfalme ina tundu katikati.
289.Poopoo mbili zavuka mto.
290.Po pote niendako anifuata.

R
291.Rafiki yangu ana mguu mmoja.
292.Reli yangu hutandika ardhini.
www.vitabutanzania.com
293.Ruka Riba.

S
294.Shamba langu kubwa lakini mavuno hayajazi kiganja.
295.Shamba langu miti mitano tu.
296.Shangazi yangu ni mrefu sana lakini hafikii tumbo la kondoo.
297.Sijui aendako wala atokako.
298.Sijui afanyavyo.
299.Sina dada wala kaka, lakini baba wa huyu jamaa ni mtoto wa babangu. Ni nani huyo?
300.Subiri kidogo!
301.Sultani alipiga mbiu watu waje kufanya kazi yake lakini wakashindwa.

T
302.Taa ya bure.
303.Taa ya Mwarabu inapepea.
304.Tajiri aniweka mfukoni na maskini anitupa.
305.Tandika kitanga tule kunazi.
306.Tangu kuzaliwa kwake sijamwona asimame wala kukimbia.
307.Tatarata mpaka ng'ambo yam to.
308.Tatu tatu mpaka pwani.
309.Tega nikutegue.
310.Teke teke huzaa gumugumu, na gumugumu huzaa teke teke.
311.Tengeneza kiwanja kikubwa kabila Fulani lije kupigania.
312. Tonge la ugali lanifikisha pwani.
www.vitabutanzania.com
313. Tukate kwa visu ambacho hakitakatika.
314. Tulikaribishwa mahali na mdogo wangu, yeye akaanza kushiba kabla yangu.
315. Tuliua ng'ombe na babu, kila ajaye hukata.
316. Tuliua ng'ombe wawili ngozi ni sawasawa.
317. Tumvike mwanamke huyu nguo.
318. Tunajengajenga matiti juu.
319. Twamsikia lakini hatumwoni.

U
320. Ukimcheka atakucheka, ukimwomba atakuomba.
321. Ukimwita kwa nguvu hasikii, lakini ukimwita polepole husikia.
322. Ukimwona anakuona.
323. Ukitaka kufahamu ana mbio, mwonyeshe moto.
324. Ukitembea ulimwengu wote utakosa nyayo.
325. Ukiukata haukatiki, ukiushika haushikiki.
326. Ukiwa mbali waweza kumwona Fulani umatini.
327. Ukoo wa liwali hauna haya.
328. Ule usile mamoja.
329. Umempiga sungurra akatoa unga.
330. Unatembea naye wote umjiao atakuona.
331. Upande wote umjiao atakuona.
332. Ushuru wa njia wa asili.
333. Utahesabu mchana na usiku na hutamaliza kuhesabu.

www.vitabutanzania.com
V
334. Viti kumi nyumbani, tisa vyakalika lakini kimoja hakikaliki.

W
335. Wake wa mjomba kimo kimoja.
336. Wako karibu lakini hawasalimiani.
337. Wanakuja mmoja mmoja na kujiunga kuwa kitu kimoja.
338. Wanameza watu jua linapokuchwa.
339. Wanamwua nyoka.
340. Wanangu wawili hugombana mchana, usiku hupatana.
341. Wanao wakati wao wa kuringa, nao ni weupe kama barafu.
342. Wanapanda mlima kwa makoti mazuri meusi na meupe.
343. Wanastarehe darini.
344. Wanatembea lakini hawatembelewi.
345. Watoto wa mtu mmoja hulala chini kila mwaka.
346. Watoto wangu wana vilemba, asio kilemba si mwanangu.
347. Watoto wangu wote nimewavika kofia nyekundu.
348. Watoto wangu wote wamebeba vifurushi.
349. Watu ishirini walipanda juu ya mti, wawili wakaona chungwa, watano wakalichuma,
kumi
wakalimenya, wote wakaridhirika mtu mmoja alile.Je, ni watu gani hao?
350. Watu waliokaa na kuvaa kofia nyekundu.
351. Watu wamehama askari wekundu wakazidi nyikani.
352. Watu wawili hupendana sana; kati ya mchana hufuatana ingawa mmoja ni dhaifu.
www.vitabutanzania.com
Usiku mdhaifu haonekani tena.
353. Watu wote ketini tumfinye mchawi.
354. Wewe kipofu unaenda wapi huko juu?

Y
355. Yaenda mbali lakini haiondoki ilipo.

Z
356. Zilitazamana na mpaka sasa hazijakutana.
357. Ziwa dogo linarusha mchanga.
358. Ziwa kubwa, lakini naogelea ukingoni tu.












www.vitabutanzania.com
MAJIBU YA VITENDAWILI
A
1.Inzi
2.Konokono
3.Nungunungu (Kufuma ni kuchoma. Nungunungu huchoma kwa miiba yake ingawa si
sawa na mishale ya mwindaji)
4.Ndege
5.Mwavuli
6.Jua
7.Ugonjwa
8.Mgomba (Migomba katika kiunga hupendeza baada ya kukwanyua majani makavu)
9.Mkindu
10.Inzi
11.Papa
12.Kaburi
13.Giza
14.Jua
15.Mbegu
16.Konokono au Koa
17.Mgomba (Shina la mgomba huzungukwa na machipukizi)
18.Wali
19.Kaburi ( KAburi ni kama joho la mauti)
20.Picha
21.Mchanga
www.vitabutanzania.com
22.Ardhi
23.Mauti
24.Moto
25.Kitanda (Kueleka ni kuchukua mgomgoni)
26.Maboga (Tunda la mboga hukaa chini ya majani yake)
27.Mahindi
28.Chunguchungu
29.Fedha
30.Mvua (Matone yake ni kama mbegu azitapanyazo mkulima)
31.Samaki

B
32.Muwa (Kipande cha muwa kikipandwa hutokea muwa mkubwa)
33.Sisimizi
34.Mawingu (Baba mawingu huleta mvua na ngurumo)
35.Mtama au Nazi
36.Muwa (Taz. 32 juu)
37.Mvua (Taz 34 juu)
38.Mti na Shoka
39.Siafu
40.Nyayo
41.Mlango (BAwabu ni mngoja mlango)
42.Kope za macho
43.Kinu cha kutwangia
www.vitabutanzania.com

C
44.Usingizi
45.Nyama na mfupa
46.Jua
47.Mwezi au Jua
48.Yai
49.Pazia
50.Mjusi au panya
51.Dunia na mbingu

D
52.Jani likwanyukapo
53.Jiwe mtoni
54.Daraja la buibui
55.Radi

F
56.Mwezi na nyota angani
57.Kioo
58.Kata mtungini
59.Mikia ya mbwa

H
www.vitabutanzania.com
60.Jua
61.Maji
62.Nywele
63.Hewa
64.Moyo
65.Kula
66.Ardhi
67.Njaa
68.Ukucha
69.Mvua
70.Mvua
71.Kalamu
72.Upepo au Mvua
73.Kwapani
74.Pua ya Mbwa
75.Mauti
76.Utelezi
77.Mkufu
78.Nyuki mzingani
79.Nyota
80.Miguu
81.Jua (Jua ni kali zaidi wakati wa mchana kuliko asubuhi au jioni)
82.Mkia wa kondoo
83.Sindano
www.vitabutanzania.com
84.Jua
85.Matendegu ya Kitanda
86.Ndoana
87.Kivuli
88.Mafiga
89.Kuku (Kuku akifunguliwa asubuhi hukimbia nje upesi bila kusalimu)
90.Moshi
91.Chungu jikoni
92.Mbegu na matunda

I
93.Herufi "K";
94.Kifo

J
95.Miguu (yaani Nyayo)
96.Nywele kichwani
97.Macho

K
98.Kata ya kuchukulia mizigo kichwani
99.Paka na mkia wake
100.Kizingiti cha mlango
101.Ulimi
www.vitabutanzania.com
102.Nazi
103.Tumbako inaponuswa puani
104.Macho
105.Maziwa
106.Mvua (Taz. 34 juu)
107.Kifo
108.Mlango
109.Jua
110.Kivuli
111.Chawa
112.Saa
113.Mwangwi
114.Taa ya Utambi (Utambi ndio nyoka mkali anayemaliza mafuta ya taa ambayo ni maji
ya kisima Bimpai)
115.Kinywa na meno
116.Mimba
117.Moto
118.Kuku aatamiapo mayai
119.Uyoga
120.Maisha ya binadamu (Mtoto mchanga hutambaa na halafu hutembea na mzee
kutumia mkongojo)
121.Kipara
122.Kisima
123.Mhindi
www.vitabutanzania.com
124.Konokono
125.Jiwe la kusagia
126.Kuska mkeka
127.Nyoka au samaki
128.Nanasi au chungwa
129.Matunda
130.Nafasi kati mdomo na pua (Ulimi hauwezi kugusa pua)
131.Ghala
132.Chongo
133.Mtoto akililia maziwa
134.Watoto wa ng'ombe na mbuzi
135.Mikia ya panya
136.Nguzo za nyumba

L
137.Chunguchungu
138.Debe ama buyu
139.Neno
140.Sindano

M
141.Chungu cha kupikia
142.Nyumba
143.Mafiga
www.vitabutanzania.com
144.Katani
145.Mlango
146.Mchwa
147.Kohozi
148.Mvua (Taz. 34 juu)
149.Moto na mafiga
150.Hindi
151.Inzi
152.Njia
153.Hindi
154.Shimo la mchwa
155.Sima (ugali)
156.Maji
157.Kisogo
158.Sima
159.Nafasi kati yam domo na pua ya ngombe
160.Buibui na utando wake
161.Mkungu wa ndizi
162.Mimba
163.Kichwa na masikio
164.Ngoma na upatu
165.Mwaka
166.Ulimi mdomoni
167.Mawazo
www.vitabutanzania.com
168.Kobe
169.Jiwe
170.Jua
171.Kinyesi na inzi
172.Kunguru
173.Nyuki
174.Shoka (Mwanang'anga ni ndege aliaye mwituni kama shoka.)
175.Tufani
176.Kweme (Tunda la mkweme)
177.Mvua
178.Mvua
179.Siafu
180.Hindi

N
181.Mwiba
182.Njia
183.Tumbo
184.Kinyesi
185.Mate
186.Kivuli
187.Kitanda
188.Kisigino
189.Muwa
www.vitabutanzania.com
190.Matunda ya pua au kwapa
191.Miiba
192.Ulimi (Miiba hapa ni meno)
193.Mbwa
194.Mzinga wa nyuki kwa nje
195.Mzinga wa nyuki
196.Nyota
197.Macho
198.Boga change
199.Mawe mtoni
200.Mijusi
201.Vibuyu
202.Viazi vitamu udongoni
203.Pesa au nyayo
204.Katani
205.Fimbo ya kuchunga
206.Firigisi (tumbo la kuku au ndege)
207.Nyusi (Nywele zinazoota penye sehemu ya uso inayotokeza kwa juu ya macho)
208.Kioo
209.Kivuli majini
210.Mwangwi
211.Popo
212.Utomvu wa papai
213.Puliza kidole wakati unapojikwaa
www.vitabutanzania.com
214.Mwangwi
215.Shoka
216.Majani makavu na mabichi
217.Kivuli
218.Shimo
219.Jicho
220.Umande na jua
221.Mahindi machanga
222.Jani la mgomba la nchani
223.Kupanda mbegu
224.Fuko
225.Mwiba
226.Manyingu
227.Kiazi kikuu
228.Pelele
229.Mzinga wa nyuki
230.Hakuna
231.Ulimi kinywani
232.Chura
233.KIvuli
234.Njia
235.Masikio
236.Mjusi
237.Utomvu
www.vitabutanzania.com
238.Nzige
239.Sauti ya njuga
240.Kivuli
241.Mgomba
242.Kuangua tunda ama nazi
243.Mtego
244.Kivuli
245.Moto
246.Dirisha ama ufa
247.Kata
248.Mimba
249.Nyota
250.Uyoga
251.Ulimi na meno
252.Maisha (Kadiri siku zinavyopita, yaani kukatwa, ndivyo umri unavyoongezeka)
253.Jina
254.Dada (Si kawaida mtu kuoa dada yake)
255.Mke
256.Maziwa
257.Jembe
258.Mdomo
259.Kinywa
260.Kunguru
261. Mafiga
www.vitabutanzania.com
262. Kivuli
263. Jiwe
264. Maji na mkojo (Mkojo unadhaniwa kuwa maji yaliyobadilika rangi baada ya kupita
mwilini)
265. Chungu cha kupikia
266. Kivuli
267. Kichwa
268. Jua ama mwezi
269. Njia ya jua au mwezi angani
270. Kiraka
271. Matendegu
272. Sungura alalapo
273. Kinoo
274. Mkufu
275. Kitanda
276. Mwembe
277. Kichunguu
278. Uyoga
279. Yai
280. Kaburi
281. Konokono (Nyumba yake iko mgongoni wakati wote)

O
282. Mwanamke aliyevunja chungu, mshangao wake
www.vitabutanzania.com
283. Maji ya mfereji

P
284. Mbarika
285. Wa kwanza ni mtoto tumboni mwa mamake, wa pili ni mtoto aliyebebwa mgongoni,
wa tatu ni mama mwenyewe
286. Sima ya ugali
287. Utelezi
288. Kata ya kuchukulia mizigo
289. Macho (Popoo ni tunda la mti uitwao mpopoo)
290. Kivuli

R
291. Uyoga
292. Siafu
293. Maiti

S
294. Nywele kichwani (Nywele zikikatwa, hata kichwa kikubwa namna gani,zafumbatika
kwa kiganja cha mkono.
295. Mkono wa vidole
296. Njia
297. Upepo
298. Nyoka apandavyo mtini
www.vitabutanzania.com
299. Mtoto wangu
300. Miiba (Mtu akichomwa na mwiba husubiri)
301. Maji

T
302. Jua au mwezi
303. Kilemba
304. Makamasi (Tajiri hutumia kitambaa cha mfukoni kupenga makamasi, lakini maskin
hupenga kwa mkono na kutupa)
305. Nyota
306. Mkufu
307. Utando wa buibui
308. Mafiga
309. Mwiba
310. Mhindi ama yai
311. Mbono
312. Jicho
313. Maji
314. Kucha
315. Kinoo
316. Mbingu na nchi
317. Kuezeka nyumba
318. Mpapai
319. Sauti
www.vitabutanzania.com

U
320. Mwangwi
321. Fisi
322. Jua
323. Kinyonga
324. Mwamba
325. Moshi
326. Tundu la sindano
327. Wanyama
328. Kifo
329. Tunda la mbuyu
330. Fimbo ama bakora
331. Kinyonga
332. Kujikwaa
333. Nywele

V
334. Moto

W
335. Vipande vya kweme
336. Nyumba ama kuta zinazoelekeana
337. MAtone ya mvua
www.vitabutanzania.com
338. Nyumba
339. Watu wanaotwanga
340. Mlango
341. Nyota
342. Vipepeo
343. Panya
344. Macho
345. Maboga
346. Fuu
347. Jogoo
348. Vitovu
349. Waliopanda ni vidole vya miguu na mikono,walioona ni macho wawili,waliochuma ni
vidole vitano vya mkono, waliomenya ni vidole vya mikono yote miwili, na aliyelila ni
mdomo.
350. Kuku, katani au mahindi
351. Viroboto
352. Kivuli
353. Kula ugali
354. Mkweme

Y
355. Njia

Z
www.vitabutanzania.com
356. Kingo za mto
357. Chungu jikoni
358. Moto

You might also like