You are on page 1of 9

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA


TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2008

TAARIFA KWA UMMA


KUHUSU TOZO KWENYE SEKTA YA TEHAMA
1.

UTANGULIZI

Katika wiki ya pili ya Februari 2015, baadhi ya watoa huduma za mawasiliano ya


simu za mkononi walianzisha vifurushi vya mawasiliano na bei na kusabababisha
malalamiko kutoka kwa watumiaji na umma kwa ujumla. TCRA, kwa kuzingatia upeo
wa shughuli zake, imechambua hali hiyo na inapenda kutoa maelezo na maagizo
ambayo yatawezesha kuondoa sintofahamu iliyopo na kujenga mustakabali kwa siku
zijazo.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003,
miongoni mwa

kazi za TCRA ni kufuatilia utoaji wa huduma katika sekta

inazozisimamia kwa kuzingatia kiwango cha upatikanaji wa huduma hizo, ubora na


viwango vya huduma, bei ya huduma na kuhimiza ushindani

na ufanisi wa

kiuchumi. Katika kutelekeza majukumu yake, TCRA inawajibika kupitia na


kuchambua, mara kwa mara, utoaji wa huduma katika sekta na kuchukua hatua
dhidi ya chochote kinachotokea kwenye soko, kiwe chanya au hasi.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inaongozwa na Sera za Kisekta, Sheria

ya

Mamlaka ya Mawasilioano Tanzania ya 2003, Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na


Posta

(EPOCA) ya 2010, na Kanuni zake za mwaka 2011 zilizotungwa kwa

kuzingatia matakwa ya EPOCA. Kifungu 6(1) cha Sheria ya TCRA kinaitaka Mamlala
kufuatilia utoaji wa huduma unaofanywa na sekta inazozisimamia ikiwa ni pamoja na
upatikanaji, ubora na viwango vya huduma, gharama za huduma hizo na kufanikisha
ufumbuzi na utatuaji wa malalamiko na migogoro. Hivi karibuni kumekuwa na
malalamiko kuhusu tozo mpya zilizotangazwa na makampuni ya simu za mkononi.

2.

UKUAJI WA SEKTA YA TEHAMA

Kumekukuwepo na kukua na kubadilika kwa haraka kwa soko la mawasiliano


Tanzania katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Mwaka 2005, kwa kuzingatia
mabadiliko ya TEHAMA duniani kote, Tanzania ilianzisha mfumo wa leseni
unaozingatia muingiliano wa tekinolojia. Mfumo huo unajulikana kama converged
licencing framework; kwa kifupi, CLF ambamo, aina nne za leseni zilianzishwa. Hizo
ni leseni inayomwezesha mwekezaji kujenga miundombinu na kutoa huduma; leseni
inayowezesha kutoa huduma ama kwa kutumia miundombinu anayomilki mtoa
huduma au anayokodisha; leseni ya kuwezesha utoaji wa huduma kama vile za
mawasiliano ya intaneti, huduma za kifedha kupitia mtandao na leseni kwa ajili ya
maudhui ya utangazaji wa televisheni na redio.
Soko la TEHAMA limekuwa kwa idadi ya watumiaji wa huduma hizo, kwa aina
mbalimbali za huduma hizo na kwa kuongezeka kwa eneo ambamo huduma
mbalimbali zinapatikana; ingawaje idadi ya watumiaji wa simu za mezani
imepungua. Kuna laini za simu za mkononi zipatazo 31,862,656 sasa ukilinganisha
na laini 2,963,737 mwaka 2005; kama iliyoonyeshwa hapo chini. Idadi ya simu za
mezani ni 151, ukilinganisha na 154, 420 mwaka 2005.

Watumiaji wa intaneti

wameongezake hadi kufikia 11,000,000 Desemba 2014 kutoka 3,563,732 mwaka


2008. Kwa sasa, kuna hamu kubwa ya matumizi ya intaneti na mwelekeo huu
utaendelea; hasa kutakapokuwa na ongezeko la mitandao inayowezesha kutoa
huduma za intaneti; na kuongezeka kwa mitandao ya jamii.

3.

AINA NA MPANGILIO WA TOZO

Watumiaji wa TEHAMA wanapata aina kuu tatu za huduma, ambazo ni:

Huduma za sauti (kuzungumza)


Huduma ya ujumbe mfupi wa meseji, kwa kifupi SMS (Short Message
System)
Intaneti

Wateja walionunua laini au ambao wanatumia huduma za simu kwa kuzungumza


imeongezeka kwa asilimia 91 kutoka milioni tatu (3,000,000) mwaka 2005 hadi
milioni 32 ( 32,000,000) mwaka 2014. Hii imewezesha huduma za simu kufikia
asilimia 97 ya Watanzania ilipofika Desemba 2014; kutoka asimilia 10 mwaka 2005.
Kwa upande mwingine, muda wa kuzungumza kwa simu, ukiwa umepimwa kwa
dakika zinazotumika, umeongezeka sambamba na ongezeko la idadi ya watumiaji.
Umefikia dakika bilioni 41 kutioka dakika milioni 506 mwaka 2005.
Matumizi kwa upande wa meseji, yaani SMS na data pia yameongezeka kwa kiasi
kikubwa kutoka SMS zipatazo milioni 5 mwaka 2005 hadi SMS bilioni 10 mwaka
2014. Watumiaji wa intaneti wanaotumia simu za mkononi sasa wanafikia milioni 10.
Huduma hizi zinatozwa na watoa huduma kwa aina mbili za tozo: Kuna tozo za
msingi na tozo mtumiaji anapojiunga na vifurushi. Gharama za kupiga simu
zinatozwa kwa shilingi kutokana na dakika mtumiaji atakazotumia kuongea,
gharama za kutuma SMS zinatozwa kwa kila ujumbe mfupi unaotumwa na zile za
intaneti na data zinatozwa kwa uniti ambazo mtu anatumia. Uniti hizi zinaitwa
3

bytes, kwa mfano, Megabytes au kwa kifupi MB na Gigabytes ambazo ni MBs


1,024. Hivyo, matumizi ya intaneti yanatozwa kwa MB au GB mtu anazotumia. Hivi
karibuni watoa huduma wametangaza vifurushi vipya ambavyo vimesababisha
malamiko kutoka kwa baadhi ya watumiaji.
3.1 TOZO ZA MSINGI
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kumekuwa na kupungua kwa ujumla kwa
tozo za msingi kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali linalofuata, baada ya
kuzingatia ongezeko la jumla la bei (inflation). Ni vyema ikazingatiwa kwamba
gharama za muingiliano kati ya watoa huduma; yaani kiasi ambacho watoa huduma
wanalipana kwa kuwezesha watumiaji wa mitandao mingine kutumia mitandao yao
kimekuwa kikipungua.

Taarifa hiiinachambua tozo za vifurushi. Iwapo mtumiaji

hatajiunga na kifurushi, tozo za msingi zinatumika.

3.2 AINA NA MPANGILIO WA VIFURUSHI


Watoa huduma za simu kwa kawaida wanatoa mpangilio wa tozo kwa wateja wao
sambamba na tozo za msingi. Vifurushi ni mpangilio ambao mtumiaji anachagua
yeye mwenyewe kwa kupenda. Hata hivyo mpangilio huu umetokea kupendwa sana
na weatumiaji. Kwa kawaida vifurushi vinauzwa kwa huduma za mazungumzo, za
kutuma meseji na za intaneti.
Mtumiaji anaweza kujisajili kutumia kifurushi ama cha siku, wiki au mwezi.
Tutachambua mipangilio hii katika majedwali yanayofuata.
4

3.2.1

VIFURUSHI VYA MAZUNGUMZO, MESEJI NA INTANETI

3.2.1.1
VIFURUSHI
INTANETI

VYA

SIKU

VYA

MAZUNGUMZO,

MESEJI

NA

Jedwali 1: Idadi ya Dakika, Meseji kwa bei za chini na za juu kwa Siku
Kabla

Vodacom
Airtel

Tigo

Bei
(TZS)
399
999
399

Baada

Dakika

SMS

MB

Bei

Dakika

SMS

MB

4
21
5

50
1,000
50
Bila
Kikomo
300
1000

15
100
15

499
999
499

7
20
9

300
1,000
300

8
8
10

250

999

24

1,000

10

30
100

649
999

13
20

450
1,000

8
8

995

40

499
999

7
21

Uchambuzi 1:

Kuna mabadiliko ya bei na idadi ya dakika na idadi ya meseji. Hata


hivyo mabadiko haya sio makubwa.
Kuna upungufu mkubwa wa kiasi cha uniti za data, MBs.

3.2.1.2
VIFURUSHI VYA WIKI VYA MAZUNGUMZO, MESEJI NA
INTANETI
Jedwali 2: Idadi ya dakika, meseji kwa bei za chini na za juu kwa vifurushi
vya Wiki
Kabla

Baada

Bei (TZS)

Dakika

SMS

MB

Bei

Dakika

SMS

MB

1,999

30

500

100

1,999

29

500

60

4,999

90

1,000

300

9,999

190

1000

60

1,995

60

700

175

1,999

34

1,000

70

5,999

200

Bila kikomo

2,000

9,999

200

5,000

70

1,999

40

700

300

4,999

91

2,000

60

9,999

250

5,000

1,024

9,999

190

5,000

60

Vodacom
Airtel
Tigo

Uchambuzi 2:

Kuna mabadiliko ya bei na idadi ya dakika na idadi ya meseji. Hata


hivyo mabadiko haya sio makubwa.
Kuna upungufu mkubwa wa kiasi cha uniti za data,MBs.

3.2.1.3 VIFURUSHI VYA MWEZI VYA MAZUNGUMZO, MESEJI NA INTANETI


Jedwali 3: Idadi ya dakika, meseji kwa bei za chini na za juu kwa
vifurushi vya Wiki
Kabla
Bei
(TZS)
10,999

Vodacom

Dakika

SMS

MB

Bei

Dakika

130

500

300

14,999

230

1200

250

550

2,500

800

49,999

1,000

3,000

250

29,999
Airtel
Tigo

Baada
SMS

MB

9999

175

5,000

400

9,999

175

5,000

300

49,999

1,100

10,000

2048

49,999

1,100

10,000

300

9,999

200

8,000

1,024

19,999

370

8,000

250

49,999

1,200

10,000

4,096

49,999

1,000

10,000

250

Uchambuzi 3:

Kuna mabadiliko ya bei na idadi ya dakika na idadi ya meseji. Hata


hivyo mabadiko haya sio makubwa.
Kuna upungufu mkubwa wa kiasi cha uniti za data,MBs.

3.2.2 VIFURUSHI VYA INTANETI PEKEE.


Kwa ajili ya kulinganisha,vifurushi vya intaneti tu ndivyo vilivyochambuliwa kwa
kuwa ndiyo huduma ambayo inatolewa na watoa huduma wenye leseni za kutoa
huduma za intaneti.
Jedwali 4. Vifurushi vya Intaneti vya mwezi:
Bei (TZS)
Vodacom
2,500
25,000
Airtel
12,500
30,000
Tigo
15,000
25,000
Zantel
6,000
300,000

MBs
100
Bila kikomo
3,000
20,000
1,000
Bila kikomo
600
Bila kikomo

Bei
25
4
2
15
10
-

TTCL
Smile

28,000
10,500

Bila kikomo
500

21

1,450,000

200 GB

Mpangilio huo wa tozo kwa matumizi ya intaneti kwa mwezi unaonyesha kwamba
mtumiaji analipa kidogo anapotumia uniti nyingi zaidi.Kwa hiyo, mpangilio huu
unawafaa zaidi wale wenye matumizi makubwa ya intaneti.
4. HITIMISHO, MAPENDEKEZO NA MAAGIZO:
Kama tulivyoeleza awali kuna aina mbili za toto: Tozo za msingi na tozo za vifurushi.
Malalamiko ya hivi karibuni ya watumiaji yameelekezwa kwenye mpangilio na tozo
za vifurushi. TCRA imechambua mpangilio wa vifurushi tozo za zamani na mpya na
kugundua kwamba ingawaje baadhi ya watoa huduma wamabadilisha bei, kwa
ujumba bei za muda wa kuzungumza na idadi ya meseji hazikubadilika sana. Hata
hivyo, kuna upungufu mkubwa kwa idadi ya uniti za data (MBs).
Kwa hivyo, TCRA inaagiza kama ifuatavyo:
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itachukua hatua stahiki za usimamizi kuhakikisha
kwamba watoa huduma wanazingatia matakwa ya sheria. Kifungu cha 5 cha Kanuni
za tozo (EPOCA Tariff Regulations) za mwaka 2011 kinayataka makampuni ya simu
kuwasilisha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania gharama mpya wanazokusudia
kutoza wateja wao kabla hazijaanza kutumika. Mamlaka itatoa adhabu kila
inavyobidi.

TCRA inaagiza watoa huduma kuzingatia sheria kila wanapobadilisha bei


za bidhaa zao;
(a) Kuziwasilisha kwa Mamlaka kabla hazijaanza kutumika,
(b) Kutoa taarifa za tozo za msingi na vifurushi kwa njia ambayo itaweza
kuwafikia watumiaji wa simu za mkonini,
(c) Kupitia upya bei na tozo mpya kwa kuzingatia mapendekezo haya na
kuwasilisha kwa Mamlaka kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Kanuni
za EPOCA za 2011 kuhusu tozo ( EPOCA (Tariff Regulation of 2011).

TCRA inawaagiza watoa huduma kuhakikisha kwamba mabadiliko


yoyote yanatekelezwa kidogo kidogo na sio ya ghafla ili kuepuka
sintofahamu katika soko;
(a)

TCRA inawaagiza watoa huduma kuwapa wateja wao nafasi

ya kuchagua mpangilio wa vifurushi tofauti kwa huduma wanazohitaji:


Kifurushi cha mazungumzo, Meseji na Intaneti cha siku, siku saba au
mwezi ambacho kinampa mtumiaji uhuru wa kuchagua kiasi ambacho
wako tarari kulipia kwa mazungumzo, meseji na intaneti.
(b)

Vifurushi vya mazungumzo tu: Hivi navyo kwa siku, siku

saba au siku 30 kwa ajili ya watumiaji ambao hawahitaji intaneti na meseji


kwa sababu moja au nyingine na wako tayari kulipia vifurushi vya sauti
pekee;
(c)

Vifurushi cha Meseji (SMS) tu:

Kwa watumiaji ambao

hawahitaji intaneti au muda wa mazungumzo kwa sababu moja au nyingine,


au ambao wanatumia SMS kwa wingi. Hivi nayo viwe kwa siku, siku saba au
siku 30 kwa bei ambazo mtumiaji atachagua.
(d)

Vifurushi vya Intaneti tu: Kwa watumiaji ambao wanatumia

intaneti kwa wingi. Hawa wapewe uhuru wa kuchagua vifurushi vya siku, siku
saba au siku 30.

TCRA inawashauri watumiaji wa huduma za mawasiliano kuchagua


vifurushi na mpangilio wa tozo ambao unafaa kwa matumizi yao.
Watumiaji

wanatakiwa

kudai

taarifa

kamili

kuhusu

huduma

wanazozilipia na waelewe taarifa za watoa huduma kuhusu bei na


tozo, ikiwa ni pamoja na vigezo na masharti ya huduma. Mtumiaji
asiporidhishwa na huduma anayopata anatakiwa alalamike kwanza
kwa mtoa huduma wake, na asiporidhika na ufumbuzi awasilishe
malalamiko yake TCRA.

Watumiaji wanashauriwa kuchukua fursa ya soko huria la mawasiliano


nchini kama nafasi ya kulinganisha huduma na bei za watoa huduma
na vifurushi wanavyouza kabla ya kuamua kujiunga na kifurushi
chochote au huduma yoyote.

Watumiaji wa simu janja zinazowezesha matumizi ya huduma nyingi,


maarufu kama smart phone, kuwa makini wakati wa kuzitumia.
Wahakikishe kwamba wanazima maeneo ambayo yanaweza kutumia
data hata kama wakati huo hawatumii vifurushi vya data walivyonunua
kwenye vifurushi.

Kwa taarifa zaidi, wasiliana na TCRA, Na. 20 Barabara ya Sam Nujoma, Dar Es
Salaam. SL.P 474 Dar Es Salaam 11414. Barua pepe: dg@tcra.go.tz

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
23 Februari 2015

You might also like