You are on page 1of 4

HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

MHESHIMIWA DKT. FENELLA MUKANGARA (MB) WAKATI WA


KUFUNGA MKUTANO NA WASANII TAREHE 27 FEBRUARI, 2015
KATIKA UKUMBI WA UWANJA WA TAIFA, DAR ES SALAM
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Viongozi wa Wasanii wa fani mbalimbali,
Wakurugenzi Wizara ya Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo,
Mtoa Mada,
Waandishi wa Habari
Mabibi na Mabwana
Habari za Mchana,
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kufika
siku ya leo na kuuona mwaka 2015. Niwatakie wote heri ya mwaka
mpya, uwe wa baraka na mafanikio makubwa katika shughuli zenu
za kila siku.
Nichukue nafasi hii kuwashukuru kwa kuitikia mwaliko wetu na
kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Mkutano wa leo pamoja na
majukumu mazito mlionayo.
Ndugu Wasanii,
Napenda kutoa pongezi za dhati kwa kazi kubwa mnayoifanya ya
kueleimsha Jamii katika masuala mbalimbali. Aidha kazi zenu
zimekuwa ni chachu ya kuleta mabadiliko chanya katika Taifa letu
na zimekuwa ni utambulisho wa Utaifa wetu nje ya Tanzania.
Nawapongeza wote mlioshinda tuzo mbalimbali za kitaifa na
kimataifa mmekuwa mstari wa mbele kuitangaza nchi yetu nje ya
mipaka yetu kupitia usanii. Tunajivunia kazi zenu.
Ndugu Wasanii,
Niwahakikishie kuwa siku zote
tupo pamoja na nimekuwa
nikifuatilia kazi zenu mbalimbali, katika Luninga, kusikiliza Nyimbo,

kuona michoro mbalimbali, ubunifu katika mavazi na sanaa


zinginezo. Kwa hakika ubora wa kazi zetu za Sanaa naushuhudia
ukiongezeka siku hadi hadi siku.
Ndugu Wasanii,
Kama mnavyojua mwaka huu 2015, Taifa letu linatarajia kuwa na
matukio makubwa mawili, kura ya maoni ya Katiba
Inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu. Serikali kwa kutambua
umuhimu wenu, imeona ikutane na wadau wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo kwa lengo la kuelimishana na
kukumbushana kuhusu jukumu letu kama Wasanii katika kuelimisha
na kuhamasisha umma katika masuala mbalimbali muhimu kwa
taifa letu.
Katika Mkutano wa leo tutajikita zaidi katika kuelimishana juu ya
wajibu wenu kama Wasanii katika kuielimisha Jamii kuhusu Katiba
Inayopendekezwa na kujadili juu ya nafasi ya Sanaa/ Wasanii
katika katiba inayopendekezwa, ikiwemo haki mbalimbali za
Wasanii.
Ndugu Wasanii,
Taifa linatarajia kuendesha kura ya maoni tarehe 30 Aprili mwaka
huu na ili zoezi hili lifanikiwe kwa kiasi kikubwa taaluma na nafasi
yenu kama wasanii inahitajika kutumika kwa ufasaha na umakini
mkubwa.
Ni ukweli usiopingika kuwa ili wananchi waweze kufanya maamuzi
sahihi wakati utakapowadia ni vyema wakapata elimu kupitia njia
mbalimbali hususan kupitia sanaa juu ya katiba inayopendekezwa,
bila kusahau makundi yenye mahitaji maalum. Tunafahamu kwamba
mna washabiki wengi ambao kupitia Sanaa mnaweza kuwaelimisha
kuhusu mchakato wa upatikanaji wa Katiba Inayopendekezwa na
umuhimu wa ushiriki wao katika kuunga mkono Katiba
Inayopendekezwa.
Ndugu Waasanii
2

Tumeona ni vyema sisi kama Wizara yenye jukumu la msingi la


kuelimisha jamii katika masuala makuu ya kitaifa pamoja na nyinyi
Wasanii tukawa na ufahamu wa kutosha juu ya mategemeo yetu
kwenu katika jambo hili muhimu la Kitaifa. Hasa la kuinadi Katiba
Inayopendekezwa, kuhimiza wananchi kujiandikisha na kujitokeza
kwa wingi kupiga kura ya maoni.
Kama mnavyofahamu na watoa mada walivyowasilisha kwenu
kwamba katika Katiba Inayopendekezwa, yapo mambo mazuri
yanayoendana na wakati uliopo sasa ukilinganisha na Katiba ya
Mwaka 1977. Naamini kabisa baada ya kikao hiki, mmepata uelewa
zaidi na ukweli kuhusu katiba Inayopendekezwa. Tumieni sasa
nafasi yenu kuwafikia wananchi kwa weledi na usahihi. Waifahamu
Katiba Inayopendekezwa, wajiandikishe na kuipigia kura hapo
ifikapo Aprili 30, 2015.
Ni ukweli usiopingika kuwa Katiba
Inayopendekezwa imesheheni haki za makundi mbalimbali bila
kusahau kundi la wasanii na haki zenu zilizofafanuliwa vizuri katika
Ibara ya 59 ya Katiba Inayopendekezwa. Hii inamaanisha kwamba
wasanii kwa mara ya kwanza kilio chenu kuhusu ulinzi na haki zetu
kikatiba umezingatiwa. Hivyo kazi zenu za ubunifu zitaweza
kulindwa kikatiba
Ndugu Wasanii,
Nimeelezwa Mada zilizowasilishwa na kujadiliwa leo, zimetolewa na
mtu mahiri ambaye alishiriki katika Bunge Maalum la Katiba. Hivyo
ni matumaini yangu kwamba kupitia kwake tutaongeza uelewa
wetu juu ya wajibu wetu na umuhimu wa Katiba Inayopendekezwa.
Ni matumaini yangu kwamba tumesikiliza, tumeuliza maswali,
tumejadili na kutoa maoni ambayo yatatusaidia kutoa elimu sahihi
kwa umma.
Hasa kwa kuisemea na kuitangaza Katiba
Inayopendekezwa kwa mlengo wa kuvuka katika kura ya maoni na
wingi wa kura ya Ndiyo.
Ndugu Wasanii,

Kwa mara nyingine nitumie nafasi hii kipekee kuwashukuru na


kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya ya kuelimisha
na kuburudisha Jamii bila kusahau kulitangaza Taifa la Tanzania .
Mwisho nawaomba sana tusaidiane katika kufanikisha hili jambo
muhimu tuweze kuendelea kujipanga vizuri katika kujenga na
kuilinda nchi yetu.
Niwashukuru tena kwa kuja na kushiriki nasi na niwatakie kazi
njema ya kulijenga Taifa letu.
Asanteni!

You might also like