You are on page 1of 3

TANZANIA ROAD SAFETY AMBASSADORS-RSA

(MABALOZI WA USALAMA BARABARANI)

TAMKO LA RSA KUHUSU AJALI NA HALI YA USALAMA BARABARANI


Mwenyekiti Baraza la Taifa la Usalama Barabarani; Watanzania wote kwa ujumla;
Napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya mabalozi wa usalama barabarani,
kuungana nawe na watanzania wote kutoa pole kwa wafiwa na majeruhi wa ajali
ya basi la Majinja Express iliyotokea huko Mafinga mkoani Iringa tarehe
11.03.2014 na kuwapoteza watu 50 na kuacha wengine wengi majeruhi. Ajali hii
ni ya kustua na kusikitisha sana. Poleni majeruhi na Mwenyezi Mungu awajalie
majeruhi uponyaji wa haraka na marehemu awapokee kwenye nuru ya uso wake.
Road Safety Ambasadors(RSA) ni mtandao wa wananchi waliohamasika katika
kusaidiana na kikosi cha usalama barabarani kutii sheria bila shuruti, kuelimisha
umma kuhusu usalama barabarani, na kuripoti matukio mbalimbali barabarani
ikiwa ni pamoja na kufichua mwenendo mbaya wa madereva na askari
barabarani. Tufanya kazi zetu kupitia mtandao wa kijamii wa whatsapp,telegram
(RSA-Kulikoni Barabarani)and facebook-Nenda kwa Usalama Barabarani. Pia
tunatoa elimu kwa umma kupitia redio na televisheni. Ni mtandao wa hiyari
wenye lengo la kupunguza ajali za barabarani na madhara yake kwa jamii.
Kwa miaka mingi sasa ajali za barabarani zimeendelea kukatisha maisha ya
watanzania walio wengi na kuwaachia wengi uyatima na ulemavu. Takwimu
zinaonesha kuongezeka kwa ajali tangu ajali 6410 (1977) hadi kufikia
20618(2008; 23842(2013). Ni mwaka 2014 tu ndipo ajali zilipungua kufikia 14360
zilizosababisha vifo 3750 ukilinganisha na vifo 2905(2008) na vifo 878(2007).
Tunapongeza hatua zilizofanyika kupunguza ajali mwaka 2014 japokuwa idai ya
vifo ilikuwa bado iko juu ukilinganisha na 2008. Hatua mbalimbali zimetangazwa
kuchukuliwa na serikali, lakini ufanisi wa hatua hizo bado umekuwa wenye
mashaka. Mara nyingi kila ajali inapotokea jibu la haraka limekuwa mwendo kasi
wa dereva na tukishatoa salamu za rambi rambi tu tunasahau kabisa bila hata
kujua hatima ya waathirika wa ajali hizo. Hatukatai, ni kweli makosa ya
kibinadamu inasemekana yanachangia sana hizi ajali. Hata hivyo ipo haja ya
kwenda mbali zaidi ya majibu mepesi kuwa ni mwendo kasi tu. Twende mbele
zaidi tufuatilie na kuweka utaratibu mzuri kuhusu haki za waathirika baada ya
ajali. Wengi wamekuwa hawapati haki zao kabisa au hupata kwa kuchelewa
jambo linalopelekea kuwapa machungu zaidi majeruhi na hata yatima na wajane
wanaobaki baada ya ndugu zao kufariki. Ifike hatua tuache kutoa majibu mepesi
kwa maswali magumu na kuchukua hatuia stahiki ili kukabiliana na hali hii.

Sisi kama mtandao wa mabalozi wa usalama barabarani(RSA) tunaitaka serikali


na wadau wanaohusika kuchukua hatua za makusudi kukabiliana na hali hii hasa
zinapotokea ajali kubwa. (Major accidents)
1.

2.

3.

4.

5.

6.

7.

Kuundwa kwa taasisi huru na ya kitaalamu (National Road Accidents


Investigation Board)kuchunguza kwa kina ajali husika ili kubaini chanzo
halisi cha ajali hiyo na vitu vilivyochangia. Katika kuangalia Nini
kilitokea; Namna gani kilitokea; Kwa nini kilitokea; Nini kifanyike kuzuia
kujirudia; na Kipi kifanyike kupunguza athari ya ajali, bodi iangalie
yafuatayo:
(a) Iwapo TANROADS wana program ya ukaguzi wa mara kwa mara wa
barabara na kuzifanyia marekebisho
(b) Iwapo mabasi yanayohusika kwenye ajali yanakuwa na bima sahihi
na inayotosha kufidia wahanga wa ajali hizo
(c) Iwapo kila mamlka ilitekeleza wajibu wake kabla na baada ya
kutokea kwa ajali
(d) Uwepo wa bajeti ya kutosha kufanya matengenezo ya barabara na
kama ipo kwa nini ukarabati haukufanyika kwa wakati
(e) Iwapo wamiliki wa mabasi wana sera na taratibu zozote za
kukabiliana na ajali na nidhamu za watumishi wao
(f) Mafunzo ya dereva husika aliyepata ajali, historia ya maisha yake,
na siku kabla ya ajali au wakati wa ajali hali ya akili yake ilikuwaje.
(g) Nafasi ya hali ya kijiografia katika ajali husika mathalani, uoni,
muundo wa kijiografia wa eneo hilo, hali ya hewa nk
(h) Mwendo wa gari husika na hali ya gari hadi wakati wa ajali
(roadowrthiness)
(i) Abiria kwa kiasi gani walichangia mwendo mbaya kwa kutoripoti na
je iwapo waliripoti ni hatua gani zilichukuliwa dhidi ya dereva au
abiria husika.
Kuwawajibisha wote watakaobainika kwa namna moja ama nyingine
kuchangia kusababisha ajali. Hii ihusishe uwajibikaji wa mamlaka
mbalimbali kama vile Polisi Usalama Barabarani, SUMATRA, TANROADS,
na Wamiliki wa Magari husika.
Bima za magari ya abiria na ya mizigo zichunguzwe ili kuona kama
zinakidhi vihatarishi(risks) vinavyoweza kusababishwa na magari hayo,
uhai na uhalali wa bima hizo na ukubwa fidia zinazotolewa na bima hizo
(coverage)
Shule za udereva na sheria zake ziangaliwe upya ili kuona kama shule
hizo zinakidhi mafunzo ya udereva kulingana na teknolojia ya sasa ya
maendeleo ya magari na hasa mitaala inayotumika.
Mfumo wa upatikanaji leseni uangaliwe kwa kina kuona kama hauna
mianya ya kuwafanya watu wapate leseni bila kupitia mafunzo au
kufuzu vizuri na ikiwezekana mamlaka inayojitegemea ya utoaji leseni
na ukaguzi wa magari ianzishwe kama ilivyoanishwa kwenye sera ya
usalama barabarani, 2009.
Kutungwa kwa sheria ya Mauaji ya bila kukusudia yanayosababishwa na
taasisi (Corporate manslaughter Act) kama ilivyo kule UK ili
kuziwajibisha taasisi zisizojali usalama wa watu.
Kutekeleza kwa vitendo malengo ya sera ya usalama barabarani, 2009,
na kuweka adhabu kali kwa wanaokiuka sheria za usalama barabarani

8.
9.

Kuweka utaratibu mzuri wa kushughulikia malipo ya fidia ya bima kwa


waathirika wa ajali
Kutumia teknolojia ya kisasa ya ufuatiliaji magari ya abiria
barabarani(Real Time Traffic Monitoring System).

Tunaamini kuwa haya yakitekelezwa vyema, tunaweza kupunguza ajali kwa


kiwango kikubwa sana. Sisi kama mabalozi wa usalama barabarani tutaendelea
kutii sheria bila shuruti na kuendelea kwa nguvu zetu zote kutoa elimu ya
usalama barabarani kila siku kupitia mbinu mbalimbali. RSA tunalaani mtu au
taasisi yoyote iliyoshindwa kutekeleza wajibu wake na kupelekea au kuchangia
kwa namna moja au nyingine kutokea kwa ajali hii.
JOHN SEKA
Mwenyekiti-RSA
rsatza@gmail.com
PAMOJA TUNAIMARISHA USALAMA BARABARANI

You might also like