You are on page 1of 3

Magonjwa sugu ya Ini na upandikizaji

Ini pamoja na kuwa chombo kikubwa katika mwili wa binadamu pia ni


kiungo muhimu kwa ajili ya kazi za kimwili kwa maana iyo ni vigumu kwa
mtu kuishi bila Ini. Kutokana na maendeleo katika mbinu za kisasa za
upasuaji, kwa sasa upasuaji unafanyika kwa watu wengi zaidi kuliko miaka
ya nyuma kwa kuwa watu wengi wako tayari kufanyiwa upasuaji kutokana
na kuboreshwa kwa viwango vya mafanikio ya upasuaji. Maradhi sugu ya
Ini yanaweza kusababisha mtu kuhitaji upandikizaji ambao kwa kawaida
unapendekezwa kwa watu walio kwenye hatua ya mwisho za magonjwa
ya Ini (ESLD End Stage Liver Diseases).
Ini linawajibika kwa kazi kadhaa muhimu za mwili kama vile kubadilisha
chakula kuwa nishati na kusafisha damu kutokana na sumu na madawa ya
kulevya. Kiungo hiki pia kina uwezo mkubwa wa kubeba damu, kwa wakati
mmoja ina uwezo wa kua na karibu asilimia 13 ya damu ya mwili.
Miongoni mwa magonjwa yanayoathiri Ini ni pamoja na homa ya manjano,
saratani, ugonjwa sugu wa mirija ya Ini (cirrhosis) ambao pia ni mchangiaji
mkuu katika kusababisha mtu kuitaji upandikizaji. Haya pia ni miongoni
mwa orodha ya magonjwa sugu ambayo hatua kwa hatua yanakuwa
mzigo kwa kiwango cha kimataifa. Kulingana na shirika la afya duniani
inakadiriwa 46% ya magonjwa na 59% ya vifo ni matokeo ya maradhi
sugu. Katika mtazamo mwingine inasemekana kuwa watu milioni 35
wanaokufa kila mwaka ni waathirika wa ugonjwa sugu na takwimu
zinaongezeka.
Kimataifa magonjwa ya Ini yanashika nafasi ya tano kwakusababisha vifo
yakiwa nyuma ya kansa na magonjwa ya moyo, kiharusi na ugonjwa wa
kifua. Hata hivyo watafiti wanasema kuwa tofauti na magonjwa mengine
kiwango cha vifo vya magonjwa ya ini yanaongezeko badala ya kupungua.
Kwa Tanzania miongoni mwa magonjwa ya kuambukiza zaidi ni Homa ya
Manjano A na Homa ya Manjano E (Hepatitis A and Hepatitis E). Yote ni
magonjwa yanaosababishwa na virusi huenea kwa maji machafu au
chakula na kuingilia utendaji kazi wa ini. Virusi pia ni mtesaji mkuu kwa
kiwango cha kimataifa, katika yote Homa sugu ya manjano ni mchangiaji
vifo 1.3million duniani kote takwimu ambazo zinalinganishwa na mzigo wa
TB, VVU / UKIMWI na malaria.
Upandikizaji wa Ini unahusisha kubadilisha Ini lenye ugonjwa na Ini zima
au sehemu ya Ini zima kutoka kwa mtu mwingine. Kwa sasa hakuna
mashine ambayo inaweza kuiga kazi ya Ini utaratibu huu hatari
unafanywa tu kama kuna ukosefu wa tiba nyingine. Pamoja na kiwango
cha mafanikio yake ya hivi karibuni utaratibu huu una uwezekano wa
kusababisha kifo kutokana na matatizo wakati na baada ya tukio hilo.

Dkt. Anand Khakhar Mshauri Mwandamizi wa upandikizaji na


Upasuaji wa Ini na Mkurugenzi Programu ya Kupandikiza Ini
katika Kituo cha Magonjwa ya Ini na Upandikizaji, Hospitali za
Apollo, Chennai, India anasema kwamba "kuna mbinu 3 za upandikizaji
Ini: upandikizaji kutoka kwa maiti, upandikizaji kutoka kwa mtu hai na
upandikizaji aina ya tatu ni upandikizaji wa sehemu ya ini ambao
haitumiki mara kwa mara. Katika upandikizaji kutoka kwa maiti Ini la
mtoaji linachukuliwa kutoka kwa mtu ambaye amegundulika amekufa,
ambaye familia yake imejitolea kuchangia ogani kwa ajili ya upandikizaji.
Watu ambao wanatakiwa kufanyiwa upandikizaji kutoka kwa maiti husubiri
katika orodha ya taasisi/kanda mpaka wapatikane wafadhili wanaofaa."
"Kupandikiza kutoka kwa mtoaji Hai inahusisha mwanafamilia mwenye
afya, kwa kawaida mzazi, ndugu, au mtoto, au mtu wa karibu kihisia,
kama vile mke, kujitolea kuchangia sehemu ya Ini kwa ajili ya upandikizaji.
Mfadhili anatathminiwa kwa makini na timu inahakikisha hakuna madhara
yanayoweza kutokea kwa mfadhili au mpokeaji.
"Upandikizaji wa msaada unahusisha sehemu ya ini ya mtoaji mtu mzima
mwenye afya (hai au maiti) kupandikizwa kwa mpokeaji. Ini la mgonjwa
linabaki kama lilivyo mpaka kipande kisaidizi kinapoanza kufanya kazi. Ini
lenye ugonjwa linaweza sasa kuondolewa."
Mapema mwezi huu timu ya madaktari kutoka Hospitali ya Apollo , Kituo
cha Magonjwa ya Ini na Upandikizaji (CLDT) wakiongozwa na Dkt. Anand
Khakhar na Dr Anil Vaidya wamefanikiwa kufanya Multi-Visceral ya
pili kwa wagonjwa wengi kwa hisani ya maiti ya mtu. Kupandikiza Ini
ambako ni kawaida hufanyika kwa mpokeaji mmoja, lakini mara kadhaa
hugawanywa kusaidia mtu mzima na mtoto, katika tukio hili pia
liligawanyika kwa watu wazima wawili, ushirikiano ambayo ni mara
chache kufaniikisha. Kwa kufanya hivyo hospitali hii inakuwa ya kwanza
kufanya operesheni hiyo nchini India kwa mtu anayeteseka kwa tumbo
kushindwa kufanya kazi vizuri tangu utotoni. Kesi hii pia ilikuwa ya kwanza
ambapo ukuta wa tumbo ulipandikizwa juu na katika matumbo ili kuondoa
tofauti kati ya mtoaji na mpokeaji wa matumbo.
Kuhusu Kitengo cha upandikizaji wa Ini katika Hospitali za Apollo.
Huduma upandikizaji wa Ini katika Hosipitali ya Apollo inalenga kutoa
huduma kwa ufanisi kwa wagonjwa wa ini. Upandikizaji Ini wa mafanikio,
unaotolewa katika hospitali za Apollo ni wa uhakika.
Hospitali za Apollo zina Kitengo kikubwa sana cha upandikizaji wa Ini
nchini India chenye mpango madhubuti wa uhifadhi na upatikanaji wa Ini
kwa ajili ya upandikizaji
Hospitali za Apollo zilizopo Delhi, Chennai, Hyderabad, Kolkata,
Ahmedabad na Bangalore hutoa upasuaji na upandikizaji wa ini na ndivyo
vinavyofanya kuwa mtandao mkubwa wa upandikizaji wa ini nchini India.
Hospitali ya Apollo ya Indraprastha, iliyopo mjini Delhi imefanikiwa
kufanya upandikizaji wa ini kwa wagonjwa 200 kutoka Pakistan Novemba

2011. Kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 90% kupitia mafanikio yake,
Hospitali ya Apollo ya Indraprastha imejijengea historia kubwa katika
ulimwengu wa tiba kwa kuwa hospitali ya kwanza nchini India kutibu
wagonjwa 200 kutoka nchi hiyo moja.
Kwa mafanikio ya zaidi ya asilimia 90% upandikizaji wa Ini zaidi ya 500
umefanyika.
Hospitali za Apollo hufanya zaidi ya upandikizaji 537 wa ini, figo na moyo
katika siku 238 na kufanya hospitali hiyo kuwa ya pili duniani katika
kufanya upandikizaji wa idadi kubwa kwa kipindi kifupi.
Chini ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake, timu katika Idara ya
ugonjwa wa ini na upandikizaji ya hospitali ya Apollo, imefanya
upandikizaji wa ini zaidi ya 100 Juni 2011, na hivyo kujichukulia umaarufu
mkubwa Chennai.
Upandikizaji wa ini wa mafanikio kwa watoto na watu wazima kwa mara
ya kwanza ulifanywa katika Hospitali ya Apollo ya Indraprastha, New Delhi
mwaka 1998. Tangu wakati huo, kumekuwa hakuna kuangalia nyuma, na
leo ni hospitali kubwa inayoongoza katika upandikizajia wa ini Asia ya
Kusini. Baadhi ya mafanikio ya kihistoria yake ni:

Upandikizaji wa mara ya kwanza wa ini kwa watoto -1998

Upandikizaji wa mara ya kwanza wa ini kutoka kwa mtu aliyekufa


-1998

Upandikizaji wa mara ya kwanza wa ini na figo -1999

Upandikizaji wa mara ya kwanza wa ini kwa watoto kutoka kwa


mfadhili aliye hai -1999

Upandikizaji wa mara ya kwanza wa ini kwa mtu aliyekwisha


pandikizwa tayari -2002

Upandikizaji wa mara ya Kwanza wa ini kwa mtoto kutoka kwa mtu


aliyekufa -2007

Upandikizaji mdogo wa ini kufanyika nchini India -2008

Upandikizaji wa Ini na figo zaidi ya 250 ndani ya mwaka ulifanyika


2009.

Timu ya Upandikizaji wa Ini katika Hospitali ya Apollo, Chennai


imefanya upandikizaji wa Ini zaidi ya 200. Na hivi sasa ni ya tatu
kwa ukubwa nchini India.

You might also like