Professional Documents
Culture Documents
Leo hii nchi yetu inaungana na nchi nyingine kote duniani kuadhimisha Siku
ya Maji Duniani, ambayo ndiyo kilele cha Wiki ya Maji kwa hapa nchini.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Maji kwa mwaka huu wa 2015 ni Maji
Kwa Maendeleo Endelevu, ambayo inakwenda sambamba na umuhimu na
mchango wa Sekta ya Maji kwa Maendeleo ya Sekta nyingine za Kiuchumi na
Kijamii.
Tumeanza leo kwa kuweka Jiwe la Msingi katika Mradi mkubwa wa Maji hapa
Mjini Musoma, na mradi huu unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili, 2015 na
utagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 41. Ni mategemeo yetu kuwa Manispaa
ya Musoma itakuwa na maji ya uhakika kwa asilimia 100 baada ya mradi huu
kukamilika. Tena, mafanikio yatakayopatikana kutokana na kukamilika kwa
mradi huu ni pamoja na:
(i)
Kuongezeka kwa uzalishaji wa maji kutoka mita
za ujazo 10,000 za
sasa kwa siku, hadi mita za ujazo 36,000 kwa siku.
(ii)
Kupanua huduma ya maji katika baadhi ya
maeneo ambayo hayana huduma, na maeneo ya mpakani mwa
Manispaa ya Musoma kama vile Bisumwa, Etaro na Nyabange.
(iii)
Ubora
wananchi utaongezeka
magonjwa.
wa
maji yanayosambazwa kwa
na hivyo kupunguza milipuko ya
(iv)
Kuongezeka kwa mapato ya Mamlaka mara
mbili yatakayosaidia kuimarisha na kustawisha huduma endelevu
ya maji kwa wakazi wa Manispaa ya Musoma.
(v)
Kuimarika kwa huduma ya maji kwenye
maeneo yote ya Manispaa ya Musoma na maeneo yaliyokuwa
yanapata maji kwa mgao kama vile Buhare, Kigera Rwamlimi, na
Bweri.
(vi)
Muda wa utoaji wa huduma ya majisaf
utaongezeka kutoka wastani wa saa 22 kwa siku za sasa
hadisaa 24 kwa siku.
Naomba nitoe rai kwa Wananchi wa Manispaa ya Musoma na Mkoa wa Mara
kwa ujumla, tuutunze mradi huu na miradi yote inayoendelea kutekelezwa
ili iendelee kuwasaidia ninyi na vizazi vijavyo.
Ndugu Wananchi;
Ndugu Wananchi;
Takwimu zilizopo zinatia hofu; kati ya mwaka 2000 hadi mwaka 2050,
mahitaji ya maji kidunia yataongezeka kwaasilimia 55. Hali hii itasababisha
kuongezeka kwa migogoro ya matumizi ya maji baina ya watumiaji wa
rasilimali za maji. Nitoe rai kwa Wataalam wa Sekta ya Maji pamoja na Sekta
nyingine zinazohusiana, kuhakikisha kuwa wanatafuta suluhisho la
upatikanaji wa maji, nishati, na uhakika wa chakula na kuwa na mipango
makini, matumizi ya teknolojia sahihi na kubwa zaidi ni ushirikiano wa karibu
baina ya wadau mbalimbali wa maji. Na juu ya haya yote, ni msisitizo katika
utunzaji endelevu wa mazingira yetu ili yaendelee kutuhifadhi. Aidha,
teknolojia za uvunaji wa maji ya mvua na ujenzi wa mabwawa ni maeneo
ambayo yatatuhakikishia kwamba tunakuwa na huduma endelevu ya
rasilimali ya maji.
Ndugu Wananchi;
Ndugu Wananchi;
Mwisho kabisa napenda tena kutoa shukrani kwa Uongozi wa Wizara ya Maji
na Mkoa wa Mara kwa kunialika kushiriki nanyi kwenye Kilele cha
Maadhimisho ya 27 ya Wiki ya Maji Kitaifa. Napenda pia, kuwashukuru wote
walioshiriki kwenye Maonesho ya Wiki ya Maji na kuwapongeza Washindi wa
Maonesho hayo. Niwashukuru pia wale wote waliochangia katika kuandaa
Maadhimisho ya mwaka huu, ikiwa ni pamoja na Wadau wetu wa
Maendeleo. Naipongeza pia Kamati ya Maandalizi kwa kazi yao nzuri
iliyohakikisha maadhimisho yanafanyika katika hali ya usalama na amani.
Baada ya kusema hayo, ninayo furaha sasa kutamka kuwa
Maadhimisho na Maonesho ya 27 ya Wiki ya Maji Kitaifa
yamefungwa rasmi.
ASANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA