You are on page 1of 1

Kaymu yafungua tawi jipya Kariakoo

Dar-es- Salaam 26.03.2015 - Kaymu Tanzania imefungua tawi jipya Kariakoo ambalo litafanya kazi kama
kituo cha kuweka bidhaa kabla hazijasafirishwa kwenda katika maeneo husika. Tawi hilo jipya
linatazamiwa kupunguza usumbufu ambao wauzaji walikumbana nao katika kupata huduma stahiki za
kampuni.
Akiongea wakati wa uzinduzi, Meneja wa Nchi wa Kaymu Erfaan Mojgani alisema tawi hili jipya liko
sambamba na mkakati wa kampuni wa kuleta huduma karibu na wauzaji.
Akiongea kuhusu ofisi hii mpya ya tawi ambayo iko Kariakoo mtaa wa Congo, Erfaan alisema, Hii ni
ishara kubwa wa ukuaji wa biashara hapa Tanzania na ni uwekezaji wa ziada nchini kuhakikisha
mafanikio kwa wanunuzi na wanunuaji.
Aliongeza, Tunajivunia kuwa karibu zaidi na wateja wetu; hii itasaidia sana katika mchakato wa
usafirishaji bidhaa kwa kuwa tupo karibu zaidi na maduka ya wauzaji wengi. Ofisi hii inatazamiwa
kutumika katika huduma za usafirishaji kila siku za kazi na pia katika kutoa huduma nyingine kama kujibu
maswali ya wateja, kutoa mafunzo kwa wauzaji na kuwa na vifaa vya kutolea huduma za upigaji picha
zenye ubora zaidi.
Cha Classic, moja kati ya wauzaji wa Kariakoo alisema, Tumefurahishwa sana na hatua ya Kaymu
kufungua kituo chake hapa Kariakoo. Huu mchakato mpya utatusaidia sana katika kutimiza oda zetu kwa
wingi. Naamini itatusaidia katika kukuza biashara zetu.
Kaymu inafanya kazi na wadau mbalimbali kuhakikisha bidhaa za wanunuaji na wauzaji zinasafirishwa
kwa muda unaotakikana. Uanzishwaji wa ofisi mpya unachangia huduma za uhakika za usafirishaji.
Pia akiongea na vyombo vya habari Bryceson, Afisa Utendaji na Uratibu wa Kaymu Tanzania alisema, Hii
ni njia nyingine ya kuwasaidia wadau wenzetu wa usafirishaji bidhaa, kwa kuwa inawawezesha kuchukua
bidhaa nyingi kwa wakati moja kutoka eneo moja maalum, na hivyo kupunguza ucheleweshwaji katika
usafirishaji bidhaa ama kughairi kushughulikia oda kutokana na maeneo ya wauzaji husika
kutokujulikana

You might also like