You are on page 1of 5

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU KAMPENI YA UGAWAJI WA DAWA ZA KUKINGA NA KUTIBU


MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE KATIKA MKOA
WA MWANZA
Ndugu Wananchi,
Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, hususan Kichocho na Minyoo
ya tumbo yameathiri sehemu kubwa ya jamii katika mkoa wetu wa
Mwanza. Magonjwa haya huleta mahangaiko makubwa kwa wananchi
hasa kwa watoto ikiwemo upungufu wa damu, kuzorotesha ukuaji,
kupunguza mahudhurio ya watoto shuleni na pia kutofanya vizuri katika
masomo yao. Ugonjwa wa Kichocho husababisha Saratani ya Kibofu cha
mkojo ambayo haina tiba hadi sasa. Minyoo ya tumbo inaweza
kusababisha Utumbo kuziba na mtu kulazimika kukatwa utumbo, Minyoo
ikiingia kwenye ubongo huleta dalili kama za kifafa vilevile minyoo huathiri
Ini na

endapo muathirika hatawahi kupata


1

matibabu, dalili zote hizi

husababisha Mauti. Magonjwa haya ni moja kati ya vyanzo vikuu vya


umasikini katika familia, jamii, na taifa kwa ujumla. Aidha, takwimu
zinaonesha kuwa wagonjwa walioathirika kwa saratani ya kibofu cha mkojo
na hasa wakazi wa kanda ya ziwa kwa asilimia kubwa chanzo chake ni
maambukizi ya kichocho.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliridhia tamko la Shirika la
Afya Duniani linalokusudia kudhibiti au kutokomeza magonjwa haya ifikapo
mwaka 2020, na ili kutekeleza azma hiyo. Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii imetengeneza mpango kazi wa miaka mitano wa Utekelezaji wa
shughuli mbalimbali za udhibiti wa magonjwa haya.
Ndugu Wananchi,
Tafiti zilizofanyika mwaka 2005 zimeonyesha uwepo wa maambukizi ya
ugonjwa wa Kichocho mkoani Mwanza yapo juu kuliko maeneo mengine
nchini. Utafiti huo ulionyesha maambukizi ya Kichocho yapo kati ya asilimia
12.7 hadi 87.6 nchini. Utafiti huo unaonesha kwamba ugonjwa wa kichocho
umeenea zaidi maeneo ya kando kando ya ziwa Viktoria na kiwango cha
maambukizo ni zaidi ya 80% na kwa minyoo ya tumbo ni hadi 100%. Na
katika jamii za watoto wenye umri wa kwenda shule, tafiti kwa njia ya
parasitologia, maambukizi ya ugonjwa huu ni zaidi ya 50%. Kwa kiwango
hicho cha maambuzi, kwa mujibu wa tafiti na maelekezo ya kitaalam ya
2

Shirika la Afya Duniani (WHO), jamii inapaswa ipewe dawa za kukinga na


kutibu.
Tangu mwaka 2009 wizara ilizindua mpango wa udhibiti wa magonjwa
yaliyokuwa hayapewi kipaumbele katika mikoa ya mitano kwa kuanzia, na
hadi mwaka 2012 mpango huu tayari ulikuwa umetekelezwa katika mikoa
14 na hadi mwishoni mwa mwaka jana (2014) umekuwa ukitekelezwa
katika mikoa 17 ikiwemo Mwanza iliyoingia katika mpango mwaka 2013.
Hadi sasa, mpango huo unaratibu shughuli zake katika mikoa 21 ikiwemo
Kilimanjaro, Arusha, Simiyu na Geita iliyoingizwa katika mpango mwaka
huu wa 2015. Lengo la mpango kwa sasa ni kuifikia mikoa ya Shinyanga,
Mara na Kagera mapema iwezekanavyo ili kudhibiti magonjwa haya ifikapo
mwaka 2020.
Ndugu Wananchi,
Mkoa unawajulisha wananchi na wakazi wote wa mkoa wa Mwanza
kuwa tarehe 26

na 27 Mei 2015 tutaendesha kampeni ya ugawaji

dawa za kukinga na kutibu magonjwa ya Kichocho na Minyoo ya


Tumbo. Walengwa wa kumeza dawa hizi ni watoto wote wenye umri
wa kuanza shule ya msingi walioandikishwa na wasioandikishwa.
Kampeni hii itaendeshwa na watalaam wa huduma za afya wakishirikiana
na Walimu katika shule zote za msingi waliopatiwa mafunzo maalumu ya
3

ugawaji wa dawa hizi. Kabla ya unywaji wa Dawa hizi Mtoto anatakiwa ale
chakula na katika muda usiozidi masaa 2 baada ya kula awe amepatiwa
dawa hizi; chakula hicho kitaandaliwa shuleni.
Hivyo kila Mzazi katika mkoa wa Mwanza anaombwa amruhusu mtoto
wake aende kumeza dawa hizi muhimu ili ajikinge na kupata tiba ya
magonjwa haya hatari kwani huduma hii ya dawa za kinga tiba inatolewa
bila malipo kwa kila mtoto.
Dawa hizi zimethibitishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa ni
salama, na hazina madhara yoyote kwa afya ya binadamu zinapomezwa
kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na wahudumu wa afya na Walimu
waliopatiwa mafunzo.
Dawa zitakazohusika ni za Praziquantel za kudhibiti Kichocho na
Albendazole za kudhibiti Minyoo ya tumbo ambazo zitatolewa kwa watoto
wote wenye umri wa kwenda shule, walioandikishwa na ambao
hawakuandikishwa.
Ndugu Wananchi,
Ni matumaini yetu

kuwa Wazazi mtawaruhusu watoto wajitokeze kwa

wingi ili kumeza dawa hizi kwa maendeleo ya afya za watoto wetu na Jamii

kwa ujumla. Nawaombeni sana, muendeleze sifa nzuri ya Mkoa wetu kwani
umekuwa ukifanya vizuri miaka yote katika suala zima la chanjo.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.
IMETOLEWA NA OFISI YA MKUU WA MKOA MWANZA

You might also like