You are on page 1of 1

TGNP Mtandao

P.O. Box 8921, Dar es Salaam, TANZANIA; Gender Resource Centre, Mabibo Road,
Tel. 255 022 2443205/2443286/2443450;
Mobile 255 0754 784050, 0715 784050; 0784 784050 Fax 255 022 2443244; Email info@tgnp.org ; web www.tgnp.org

SALAAM ZA RAMBIRAMBI KWA MSIBA WA MHARIRI EDSON KAMUKARA


TGNP Mtandao tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha ghafla cha mwanahabari na
mhariri Edson Kamukara kilichotokea jioni ya Tarehe 25.06.2015 jijini Dar es salaam.Kutoweka kwake ni
huzuni kubwa kwetu, wanahabari na jamii kwa ujumla. Hakika taifa limempoteza mtu makini na
mzalendo.
Kwa muda mrefu, TGNP Mtandao imefanya kazi na marehemuKamukara katika kuihabarisha jamii na
wanawake wa pembezoni wanapata taarifa na kupata nafasi ya kupaaza sauti zao.
Ni dhahiri kuwaKamukara alikuwa mmoja wa wahariri tuliowategemea katika harakati za kumkomboa
mwanamke. Alionesha moyo wa pekee wa kupenda kujitolea kuhakikisha anasaidia kusukuma mbele
harakati za kutetea haki za wanyonge hasa migogoro ya ardhi vijijini, ukatili wa kijinsia na kutetea ajenda
yetu ya kuwezesha wanawake kushika nafasi za uongozi katika ngazi zote.
Marehemu Kamukara alikuwa mwanaharakati, mtetezi wa wanyonge ambaye alijitahidi kuhakikisha sauti
za makundi yaliyoko pemeboni zinasikika hata kwa gharama zake binafsi ili mradi ahakikishe wanawake
na wanaume masikini wanapata fursa ya kumiliki rasilimali zao na kuifurahia keki ya taifa kwa usawa.
Tumemfahamau Edsoni kama mtu aliyechukia kabisa ubaguzi, unyonyaji, uonevu na uporaji wa rasilimali
za wanyonge. Tumeshirikiana nae karibu sana katika kutetea wanawake wa vijini wapate maji salama na
huduma nzuri za afya, makala zake zimejieleza wazi kazi nzuri aliyoifanya. Tutamkumbaka daima kwa
kazi nzuri aliyoiacha.
Sisi tuliobaki hatuna budi kusheherekea mafanikio makubwa ambayo Kamukara aliyafanya kwa
kupigania haki za wananchi na kuetetea demokraisa na haki za binadamu nchini.Tunawaomba wanahabari
waendeleze kazi nzuri aliyoifanya Edson Kamukara wakati wa uhai wake
Tunatoa salamu zetu za rambirambi kwa familia yake , Mke, mtoto mama mzazi, wahariri wote na
wanahabari na ndugu wengine pole sana kwa msiba huu mzito. Tunawaombea faraja katika kipindi hiki
kigumu.
Imetolewa na

...................................
Lilian Liundi
Mkurugenzi wa TGNP Mtandao

You might also like