You are on page 1of 2

FOR IMMEDIATE RELEASE

TAFITI YA HIFADHI BORA ZA TAIFA

Jovago: Tanzania kutambulika na UNESCO kati ya nchi maarufu za


Africa zenye hifadhi bora ni jambo la kujivunia.
DAR ES SALAAM, 5 AUGUST, 2015: Kila mwaka Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) linafanya ukaguzi wa hifadhi za taifa
zinazokidhi viwango vya kungia kwenye hadhi ya kutambulika barani Africa na
Dunia nzima.

Uchaguzi huu unazingatiwa kwa kuangalia iwapo hifadhi husika itakidhi viwango vya
vivutio vya kihistoria au kiutamaduni, mazingira halisi yenye mvuto kijiografia au
vivutio vya uoto asilia .

Kumekuwa na mamia ya hifadhi za Taifa kutoka nchi mbali mbali ikiwemo hifadhi za
taifa kutoka Tunisia, South Africa, Ghana, Alrgeria, Morocco na Kenya, lakini
Tanzania imekuwa ni moja kati ya nchi hizo zinazotambulika na UNESCO kwa
kuongozaa kuwa na hifadhi maarufu duniani.
Ndani ya mwaka 2015, hifadhi saba bora kutoka Tanzania zillingizwa kwenye orodha
ya kutambulika na UNESCO, ambazo ni; Stone town ya Zanzibar, magofu ya Kilwa
Kisiwani na magofu ya Songo Mnara, hifadhi ya Kondoa, hifadhi ya taifa ya mlima
Kilimanjaro, Mbuga za wanyama Selous, hifadhi ya Serengeti na kreta ya
Ngorongoro.

Kutokana na kupanda kwa chati, na ukidhi wa ubora wa hifadhi hizi za kitaifa,


imepelekea kuwa na wimbi kubwa la watalii kutoka nchi mbali mbali hasa kutoka
nchi za bara la Ulaya na baadhi ndani ya bara la Africa.

Andrea Guzzoni, Meneja Mkazi wa Jovago Tanzania amefafanua kwamba kutokana


na utafiti uliofanywa na Jovago hivi karibuni, inaonyesha kwamba Tanzania pamoja
na hifadhi saba zinazotambulika na UNESCO kumekuwa na ongezeko la zaidi ya
hoteli 1000 zilizojiunga na huduma ya jovago.com.Hii ni dalili kwamba hoteli nyingi
hapa Tanzania zimeelewa faida za kuhamia digitali na kutoa huduma zake kupitia
mtandaoni hivyo wageni wanaoingia hapa Tanzania hawapati usumbufu wa kutafuta
mahala salama pa kujiwekeza kupitia kwenye tovuti

Hata hivyo, kupitia tafiti zilizofanywa na Jovago, inaonyesha kuwa Africa ina hifadhi
129 zinazotambulika na UNESCO na Jovago ina zaidi ya hoteli 25,000 hapa Africa
kwenye tovuti yake aliongeza.

Katika sita bora ya nchi zinazoongoza kuwa na hifadhi bora, ni pamoja na Ethiopia
na Morocco ambazo zina hifadhi bora tisa, zikifuatiwa na hifadhi kutoka Tunisia,
Africa ya Kusini, Misri, na Algeria

Kuhusu Jovago
Jovago.com, tovuti inayorahisisha huduma za ku book hoteli kupitia mitandaoni.
Ofisi kuu hapa Africa zipo Lagos (Nigeria), Nairobi kenya, na Dakar (Senegal).
Jovago.com imegunduliwa na kampuni ya Africa Internet Group (AIG) chini ya
udhamini wa MTN na Millicom.
Jovago.com ni tovuti No.1 Inayoongoza katika huduma za ku book hoteli kupitia
mtandaoni pamoja na kutoa huduma nzuri na za haraka kwa ufanisi wa kiwango cha
juu cha urahisi wa matumizi ya tovuti hiyo. Jovago.com inazaidi ya hoteli 25,000
hapa Africa na hoteli 200,000 za dunia nzima kwenye tovuti.

You might also like