You are on page 1of 4

MH: RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

DK.JOHN POMBE MAGUFULI,


IKULU,
P.O.BOX 11400
DAR ES SALAAM,
TANZANIA.
YAH: BARUA YA WAZI KWA MH.RAIS KUTOKA KWA WALIOKUWA
WATUMISHI WA

MUDA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)

Mheshimiwa Rais sisi ni Wafanyakazi tuliokuwa tukiitumikia mamlaka ya


vitambulisho vya Taifa (NIDA). Tumeitumikia mamlaka kwa vipindi tofauti
tofauti kati ya mwaka moja hadi minne na kusitishwa mikataba yetu ya ajira
mnamo tarehe 07/03/2016 baada ya masaa ya kazi kuisha kupitia Televisheni
ya Taifa (TBC). Taarifa hiyo ilitolewa na kaimu Mkurugenzi mkuu wa NIDA Dr.
Modestus Kipilimba ambapo kwa mujibu wake idadi yetu tulikua wafanyakazi
597. Tulipokea kwa masikitiko makubwa

sana, kwasababu taarifa hiyo

ilikuwa ni ya ghafla na ya kushtukiza.Mkurugenzi alishindwa kufuata


utaratibu wa kiofisi na kutumia vyombo vya habari.
Mheshimiwa Rais Tunapenda Umma wa watanzania ujue kuwa usitishwaji
wetu wa ajira haukuwa wa halali, kwa sababu haukufuata sheria, kanuni na
utaratibu za kazi kama inavyoelezwa chini ya kifungu cha sheria ya Ajira na
mahusiano ya kazi ya mwaka 2004.
Taratibu za kusitisha ajira zinatofautiana kutegemea na sababu za kusitishwa
ajira lakini zote zina kipengele cha pamoja ambacho ni haki ya mfanyakazi
kusikilizwa kabla maamuzi ya kusitisha ajira hayajajadiliwa dhidi yake. Mh
Rais tunakubaliana na maamuzi ya mamlaka
umezitoa kwasababu za kiutawala.

na sababu ambazo uongozi

Mheshimiwa Rais baada ya kupokea taarifa hiyo tulichukua hatua zifuatazo:-

1. Tuliomba muajiri wetu atupatie barua ya kuachishwa kazi kwa maandishi,


ilichukua muda kidogo katika utekelezwaji wake lakini baadae mwajiri
alitekeleza ombi letu, lakini barua hiyo ilikuwa na mapungufu yafuatayo:a. Barua

haikueleza

ni

stahiki

gani

na

malimbikizo

gani

tunayostahili kulipwa baada ya kuachishwa kazi, angali mikataba


imesitishwa kabla ya wakati.

b. Barua ile haikutamka wazi kuwa lini tutalipwa stahiki zetu.


c. Pia kuna baadhi ya wenzetu hawakufanikiwa kupata barua kwa madai
yakuwa Ofisi haina kumbukumbu au taarifa zao na wakaomba
waandike barua za kuomba kazi upya sambamba na kupeleka wasifu
wao (CV) ndipo wawaandalie barua ya kusimamishwa kazi, huu sio
utaratibu, ni kukiuka sheria na kanuni za ajira.
d. Barua haikutamka kuwa tuna mafao kiasi gani katika mifuko ya hifadhi
ya jamii ambapo tulikuwa tukichangia kila mwezi kutokana na makato
ya asilimia kumi (10%) katika mishahara yetu.
e. Haikutamka kuhusu makato yetu ya bima ya afya tuliyokuwa
tunakatwa asilimia tatu (3%) kuchangia mfuko wa Taifa wa bima ya
afya(NHIF),lakini hata fomu za kuomba uanachama hazikupelekwa japo
tulikuwa tunakatwa kila mwezi.
2. Tuliomba taarifa fupi kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo tulikuwa
tukichangia na tukabaini yafuatayo:a. Mifuko ya GEPF, PSPF, LAPF, na NSSF mwajiri alipeleka kwa mara ya mwisho
michango yetu mwezi wa saba 2015.Hii ilionyesha kuwa mwajiri wetu hakuwa
anapeleka makato yetu kama ilivyotakiwa. Tunaomba Mheshimiwa Rais
ufuatilie upate kujua ni wapi hasa pesa zetu hizi halali zilipokua zikipelekwa
na ni akina nani hasa walipewa fedha hizi halali zilizotokana na jasho la

watumishi wako na kwa madhumuni gani, na zaid mifuko hio ya hifadhi ya


jamii kwanini na wao walikua kimya kipindi chote hicho ambacho michango
ya wanachama wao ilikua haipelekwi.
Mheshimiwa Rais tunatambua jitihada zako za kutumbua majipu na kuwawajibisha
mafisadi wanaohujumu uchumi wa taifa, mheshimiwa Rais kuna haja ya kutumbua
majipu hapa.
Mheshimiwa Rais, Tuliandika barua kwa msajili wa mifuko ya jamii SSRA, majibu
tuliyoyapata

ndio

yaliyotusukuma

kuandika

barua

hii

kwako

kwasababu

hayakuridhisha.
Tunashindwa kuamini kama leo hii tumekuwa watu wakulilia haki halali inayotokana
na jasho letu ndani ya nchi hii iliyokwisha pata uhuru. Tunatambua kuwa nchi hii
inaendeshwa katika misingi ya sheria na kusimamia haki ya kila mwananchi kama
katiba yetu ya mwaka 1977 ilivyoamuru, lakini Mh. Rais haya yanayoonekana mbele
yetu ni kinyume na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Ujira ni sehemu halali
tunayostahili kulipwa kutokana na jasho letu. Mtu yoyote katika meza yako akinywa
kikombe hiki hatasita kupaza sauti.
Mheshimiwa Rais, sisi tunarudi mtaani kupambana na ule utaratibu wako kuwa
vijana wazururaji wasio na kazi wakamatwe. Tunaomba tilipwe stahiki zetu mapema
tunazodai kutokana na jasho letu halali.
Mheshimiwa Rais, sisi wengi wetu hapa ni vijana tuliohitimu baadhi ya vyuo vikuu
hapa nchini, kazi hii ingetuwezesha kurejesha mikopo tunayodaiwa na bodi ya
mikopo kama sera mpya ya Bodi ya mikopo zinavyoagiza, pia Mheshimiwa Rais
umekua ukisikika kwenye nyumba za ibada na kwenye mikutano mbalimbali
ukisema " Asiyefanya kazi na asile", lakini kwetu sisi imekua ni tofauti, tumefanya
kazi

bila

mishahara

yetu

kuanzia

mwezi

Januari

hadi

Machi

mwaka

huu

tulipositishiwa mikataba yetu.


Mheshimiwa Rais maombi yetu kwako, mateso tunayoyapata kwa sasa ni makali
mno, madhara na athari zimejitokeza kwa baadhi yetu wengine wamepata stroke,
pia wengine wamefukuzwa kwenye nyumba walizokua wamepanga kwa kukosa
kodi, athari nyingine pia zimejitokeza katika familia zetu maana wengi wetu tulikua

tegemezi katika familia zetu, athari za ujauzito kutoka kutokana na jinsi jambo hili
linavyoendeshwa na mengine mengi. Kilio chetu kikubwa ni malimbikizo ya
mishahara yetu ya miezi 3, yaani kuanzia mwezi wa kwanza mpaka mwezi wa tatu
mwaka huu ajira yetu ilipositishwa, pia stahiki zetu zote zinazotamkwa kisheria
katika kifungu cha 44 cha sheria ya Ajira na Mahusiano ya kazi ya mwaka 2004
inayohusu taratibu za kusitisha mikataba ya Ajira.
Mheshimiwa Rais tunaomba uingilie kati swala hili tuweze kulipwa stahiki zetu na
malimbikizo ya mishahara yetu mapema, ili tuweze kuendesha maisha yetu ambayo
yamekuwa magumu mno, pia tukaendeleze sera yako ya kilimo kwa vijana.

Mheshimiwa Rais, tunamtaka Kaimu Mkurugenzi Mkuu Dr. Modestus Kipilimba


atamke wazi ni siku gani hasa atalipa mishahara yetu na mafao yetu tunayodai na
sio

jambo

analolifanya

yeye

pamoja

na

wasaidizi

wake

kueneza

ahadi

zisizotekelezeka kwenye vyombo vya habari ili aaminike anajali wakati ukweli halisi
familia zetu zinashinda njaa na kupitia kipindi kigumu sana.

Tunakupongeza kwa kazi nzuri unayoendelea kufanya katika serikali yako tukufu,
tunatumaini kilio chetu kitakufikia na kuchukua hatua.
Asante.
Imetolewa na sisi

wafanyakazi wakiwa na wanyonge

waliositishiwa mikataba ya ajira


MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA
TAIFA(NIDA).

You might also like