You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425

OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha


Makatibu Tawala wapya kumi aliowateua tarehe 25 Aprili, 2016 na kuwapangia vituo vyao
vya kazi.
Makatibu Tawala hao wameapishwa leo tarehe 27 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam
na kisha wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma, zoezi lililoendeshwa
na Kamishna wa maadili Sekreatieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mheshimiwa Jaji
Salome Kaganda na kushuhudiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Makatibu Tawala walioapishwa ni;
1. Arusha 2. Geita 3. Kagera 4. Kilimanjaro 5. Pwani 6. Shinyanga 7. Singida 8. Simiyu 9. Tabora 10. Tanga -

Richard Kwitega
Selestine Muhochi Gesimba
Armatus C. Msole
Eng. Aisha Amour
Zuberi Mhina Samataba
Albert Gabriel Msovela
Dr. Angelina Mageni Lutambi
Jumanne Abdallah Sagini
Dkt. Thea Medard Ntara
Eng. Zena Said

Makatibu Tawala wengine wa Mikoa ambao hawakuapishwa leo, ni wale waliohamishwa


vituo vya kazi na wale waliobaki katika vituo vya kazi walivyokuwep,o ambao tayari
walishakula kiapo cha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
27 Aprili, 2016

You might also like