Mkataba huu unafanyika leo tarehe ______ Mwezi . 2013
KATI YA Winners Group wa S.L.P.., Dar es Salaam (ambaye hapa ataitwa Mmiliki neno ambalo litamhusu yeye, ndugu, mawakala au warithi wake) kwa upande wa mmoja; NA .., wa S.L.P. .., Dar es Salaam (ambaye hapa ataitwa Mtunzaji neno ambalo litamhusu yeye, ndugu, mawakala au warithi wake) kwa upande wa pili. KWA KUWA Mmiliki wana uhalali wa kumiliki shamba heka 10 lililoko kijiji cha Fukayosi wilaya Bagamoyo mkoa wa Pwani; KWA KUWA Mmiliki wanayo nia ya kumpa mtunzaji mamlaka ya utunzaji wa shamba kwa maelewano na masharti yaliyopo hapa chini; KWAHIYO wote Mmiliki na Mtunzaji wanataka kuweka makubaliano na masharti yao katika mkataba rasmi;. BASI MAKUBALIANO HAYA YANASHUHUDIA KAMA IFUATAVYO: 1. Kwamba Mmiliki atamlipa Mtunzaji kiasi cha Shilingi za Kitanzania . kwa mwezi kwa kutunza shamba tajwa hapo juu. 2. Kwamba mkataba huu utadumu kwa muda wa ambao utaanza tarehe .. na kuishia tarehe .. 3. Kwamba Mtunzaji hatapangisha shamba hilo au sehemu yoyote ya shamba kwa mtu mwingine yeyote yule na endapo kutakuwa na haja ya kufanya hivyo basi Mtunzaji atawajibika kuomba kibali cha maandishi kutoka kwa Mmliki. 4.
Kwamba Mtunzaji atatumia shamba hilo kwa shughuli za Mmiliki tu na
kamwe haitatumika kufanya shughuli za Mtunzaji za binafsi, pamoja na kuangalia mazao yote yaliyopandwa ndani ya shamba hilo, kama ufuta, mananasi, maembe , miti ya mipira nk
5.
Kwamba Mtunzaji atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa shamba
hilo ni safi muda wote na kuiweka katika hali kutengenezeka kwa muda wote wa mkataba huu.
6.
Kwamba Mmiliki anayo haki ya kufika katika shamba hilo muda
wowote kwa madhumuini ya kuangalia, kufanya shughuli yoyote au kukagua hali ya shamba hilo muda wowote bila kutoa taarifa yoyote.
7.
Kwamba Mmiliki ana haki ya kusitisha mkataba huu kwa kumpa
mtunzaji notisi ya wiki moja ambayo ni lazima mtunzaji akubali.
8.
Kwamba endapo kutatokea mgogoro wowote kuhusu mkataba huu,
mgogoro huo utawasilishwa kwa msuluhishi ambaye anakubalika na pande zote mbili na ambaye uamuzi wake utaheshimiwa na kutekelezwa bila masharti. Endapo mgogoro hautasuluhishwa, upande wowote una uhuru wa kuwasilisha mgogoro kwenye vyombo vya sheria. MKATABA HUU umetiwa inavyoonekana hapa chini.
saini
na
pande
zote
MMILIKI kwa niaba ya WINNERS Group:
Jina: _____________________ Cheo:_____________________ Tarehe:____________________ Sahihi:____________________ Jina: ______________________ Cheo:______________________ Tarehe: ____________________ Sahihi:_____________________ MTUNZAJI Jina: ______________________ Cheo:______________________ Tarehe: ____________________ Sahihi:_____________________ Mbele yangu leo hii tarehe, . Mwezi .............. 2013