You are on page 1of 11

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/H/34

23 Januari, 2015

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa


mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki,
pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea
katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 121 za kazi kwa ajili ya Wizara,
Idara zinazojitegemea, Wakala wa serikali na Mamlaka za serikali za mitaa
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili
kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato
cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe
sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja Passport size ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

vii.

viii.
ix.
x.

xi.
xii.
xiii.
xiv.

Testmonials, Provisional Results, Statement of results, hati matokeo za


kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 7 Febuari, 2015
Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
HAURUHUSIWI.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
kupitia posta kwa anuani ifuatayo.

Katibu,
Sekretariati ya Ajira katika
Utumishi wa Umma,
SLP.63100,
Dar es Salaam.
1.0

AU

Secretary,
Public Service Recruitment
Secretariat,
P.O.Box 63100
Dar es Salaam.

AFISA MISITU DARAJA LA II (FOREST OFFICER GRADE II) NAFAS 5


1.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kusimamia upandaji na uhudumiaji wa miti na misitu.
Kusimamia uendelezaji wa misitu ya kupandwa isiyozidi hekta 5,000 au ya asili
isiyozidi hekta 10,000.
Kufanya utafiti wa misitu.
Kutekeleza Sera na Sheria za misitu.
Kuendesha mafunzo ya Wasaidizi Misitu.
Kukusanya takwimu za misitu.
Kufanya ukaguzi wa misitu.
Kupanga na kupima madaraja ya mbao.
Kudhibiti leseni na uvunaji wa miti.
Kutoa ushauri na mafunzo kwa wananchi juu ya uendelezaji na matumizi endelevu
ya miti na kwa wananchi.
Kufanya ukadiriaji wa rasilimali za misitu.
Kupima maeneo na kuchora ramani za misitu.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Misitu kutoka chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine au
Vyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
2.0

MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III NAFASI 7


2.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori
Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali
Kufanya usafi na ulinzi wa kambi
Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi
Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na
kukusanya takwimu zao
Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na nyara nje na ndani ya Nchi
Kudhibiti wanyamapori waharibifu
Kudhibiti moto kwenye hifadhi
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Astashahada au
Astashahada ya awali ya Uhifadhi wa Wanyamapori (Technician or Basic
Technician Certificate in Wildlife Management) kutoka Chuo cha Taaluma ya
Wanyamapori Pasiansi au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B1 kwa mwezi
3.0

AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA III (WARD EXECUTIVE OFFICER


GRADE III) NAFASI 30
3.1 MAJUKUMU YA KAZI
Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika
kata na atashughulikia masuala yote ya kata
Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbali ya uzalishaji,
mali, kuondoa njaa na Umasikini.
Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.
Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na
vitongoji.
Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata
yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibuna kusimamia shughuli za Uchaguzi katika
Kata.

Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo


lake.
Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katika ngazi ya
Kata.
Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na
nakala kwa Katibu Tarafa.
Atakuwa mwenyekiti katika vikao vya vinavyowahusisha wataalamu na watendaji
wa vjiji, na NGOS katika kata yake.
Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji,
vitongoji, na kata yake.

3.2 SIFA ZA MWOMBAJI.


Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne au sita na mwenye cheti cha Mafunzo ya
Stashahada katika fani ya Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii (Sociology), Maendeleo
ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Uchumi na Mipango kutoka chuo cha Serikali za
Mitaa Hombolo Dodoma au chuo chochote kinachotambulika na Serikali.
3.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS C kwa mwezi.
4.0
AFISA KILIMO DARAJA LA II (AGRO OFFICERS) NAFASI 10
4.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuthibiti visumbufu vya mazao na mimea,
Kukusanya takwimu za bei za mazao kila wiki na kila mwezi,
Kukusanya takwimu za upatikanaji wa mazao katika masoko kila wiki/kila mwezi,
Kuendesha mafunzo ya wataalam wa kilimo,
Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya pembejeo na zana,
Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya biashara,
Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya udongo na maji,
Kutoa habari juu ya teknolojia mpya kwa wadau,
Kuandaa/kuandika taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao,
Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji mboga, matunda, maua na mazao
mengine,
Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu bora,
Kuandaa, kutayarisha kufunga na kusambaza mbegu bora,
Kufanya majaribio ya magonjwa kwenye mbegu,
Kufanya ukaguzi wa mbegu mpya kwa kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla ya
kupitishwa,
Kuendesha mafunzo ya kuzalisha mboga, matunda, maua na viungo,
Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani,
Kufanya utafiti mdogo mdogo wa mazao yanayofaa kulimwa katika sehemu ya
kilimo cha umwagiliaji,
Kufanya utafiti wa udongo,
Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya wakulima/wamwagiliaji,

Kuzalisha mbegu za msingi baada ya kuzalishwa na watafiti,


Kuendesha/kusimamaia vishamba vya majaribio vya mbegu na uchunguzi
maabara ili kuondoa utata juu ya mbegu.

4.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya kilimo au shahada ya
sayansi waliojiimarisha katika mchepuo wa kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo
Sokoine au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
4.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D Kwa mwezi.
5.0

AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA II (AGRICULTURAL FIELD OFFICERS)


NAFASI 12
5.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kushirikiana na watafiti kuendesha vishamba vya majaribio,
Kukusanya/kuhifadhi takwimu za majaribio,
Kuwafundisha wakulima mbinu za kilimo bora,
Kuwafikishia wakulima matokeo ya utafiti,
Kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo, matumizi ya mbolea na madawa,
pembejeo za kilimo,
Kukusanya na kutunza takwimu za mazao na bei kwa wiki mwezi, robo na mwaka
ngazi ya halmashauri,
Kukusanya takwimu za mvua,
Kushiriki katika savei za kilimo,
Kushirikiana na vikundi vya wakulima kuhusu matatizo na teknolojia sahihi za
kutumia,
Kupanga mipango ya uzalishaji,
Kupima uotaji wa mbegu na kusimamia taratibu za ukaguzi,
Kutathmini na kusavei maeneo ya vyanzo vya maji kwa ajili ya kuhifadhi,
Kutunza miti mizazi,
Kuwatambua wasambazaji wa pembejeo,
Kutoa mafunzo ya lishe kwa wakulima,
Kufanya vipimo vya ubora, unyevunyevu na uotaji wa mbegu,
Kusimamia taratibu za ukaguzi,
Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea,
Kusimamia shughuli za kila siku za majaribio ya kilimo,
Kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi bora ya udongo na maji,
Kutoa ushauri wa kilimo mseto,
Kuandaa sheria ndogo za hifadhi ya mazingira na
Kutoa taaluma ya uzalishaji wa mboga, matunda, maua na viungo.

5.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha nne au Sita (VI) wenye stashahada (Diploma)
ya kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

5.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C Kwa mwezi.
6.0
MTAKWIMU DARAJA LA II (STATISTICIAN GRADE II) NAFASI 5
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kubuni na kuendeleza mfumo wa kitaifa wa kukusanya na kuratibu takwimu
Kutengeneza utaratibu wa kukusanya takwimu pamoja na ule wa kuchukua
takwimu za mfano/vielelezo (Sampling)
Kukusanya, Kuchambua na kuwasilisha takwimu ngazi za juu.

6.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza katika fani ya Takwimu au Hisabati au sifa
zinazolingana na hizo kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali na wenye
ujuzi wa kutumia Kompyuta.
6.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwe
7.0

AFISA UGAVI MKUU DARAJA LA I - NAFASI 1(INARUDIWA)


Nafasi hizi ni kwa ajili ya Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo (WMA)
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kushauri juu ya Sera ya Ununuzi na Ugavi katika Wakala;
Kushauri juu ya Mfumo wa Mtandao wa Ununuzi na Ugavi kwa kutumia kompyuta,
e-procurement;
Kutathmini taarifa ya vifaa vinavyotumika na Wakala ili kujua aina ya kasi ya vifaa
husika kwa hatua zaidi;
Kusimamia utayarishaji wa Mpango wa manunuzi wa Wakala;
Kusimamia utayarishaji wa makisio ya vifaa vinavyohitajika katika Wakala;
Kusimamia upimaji wa utendaji wa Maafisa Ugavi walio chini yake;
Kumshauri Mtendaji Mkuu kuhusu namna bora kutekeleza majukumu yanayohusu
ununuzi, utunzaji na ugavi katika Wakala;

7.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye Shahada ya Ugavi na Shahada/Stashahada ya Uzamili katika fani
za Biashara au Ugavi kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Bodi ya Taifa ya
Usimamizi wa Vifaa, na uzoefu wa kazi usiopungua miaka kumi na mbili (12).
7.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani WMAS 7 kwa mwezi

8.0
AFISA VIPIMO DARAJA LA II- NAFASI 1 (INARUDIWA)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo (WMA)
1.1.2 MAJUKUMU YA KAZI

Kukagua, kuhakiki na kuvirekebisha vipimo vya wafanyabiashara;


Kutunza na kuhifadhi vifaa vya kitaalamu vitumikavyo katika utendaji wa kazi;
Kutoa ushauri kuhusu masuala ya uhakiki na matumizi ya vipimo;
Kufanya upelelezi kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya vipimo;
Kupokea na kufanyia kazi malalamiko ya wadau na wateja;

1.1.3 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa mwenye Shahada ya kwanza katika fani ya Legal Metrology au Legal


and Industrial Metrology kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. Au
Kuajiriwa mwenye Shahada katika fani ya Uhandisi / Sanyansi ambao wamepata
crash programme in Legal and Industrial Metrology isiyopungua miezi mine (4)
kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. Au
Kuajiriwa mwenye Shahada katika fani ya Uhandisi / Sayansi ambao wamehitimu
Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) katika fani ya Vipimo kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali.
Kuajiriwa mwenye Stashahada ya juu katika fani ya Legal Metrology / Legal and
Industrial Metrology kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

1.1.4 MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani WMAS3 kwa mwezi.

MHANDISI DARAJA LA II (MAJI) WATER RESOURCE ENGINEER


NAFASI 6 (INARUDIWA)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mamlaka za Serikali za
Mitaa.
9.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kushughulikia upembuzi yakinifu, usanifu wa ujenzi, uendeshaji na matengenezo
ya miundombinu midogo midogo ya usambazaji maji na kushiriki shughuli za
upembuzi yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miundombinu
mikubwa ya ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira.
Kufanyia mapitio taarifa za upembuzi yakinifu na sanifu za ujenzi wa miundombinu
ya miradi ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.
Kufanyia ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na utengenezaji wa
miundombinu ya uzalishaji na usambazaji maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya
kupata ubora unaokusudiwa.
Kushiriki katika kazi ya kupendekeza miradi na kupitia mapendekezo ya miradi
(project proposal) ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.
Kufanya uchunguzi kuhusu uharibifu wa miundombinu au ajali zinazojitokeza
wakati wa utekelezaji wa miradi ya maji na usafi wa mazingira.
9.0

Kutayarisha bajeti ya utekelezaji wa shughuli za sekta za maji.


Kusimamia kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na mategenezo
ya miundombinu ya miradi ya maji na usafi wa mazingira.
Kukusanya na kutayarisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za sekta
ya maji kwa ajili ya matumizi ya sekta na kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya
Wahandisi.

9.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya uhandisi wa Maji (Water
Resource Engineering) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.
9.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
10.0

10.1

FUNDI SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI (UMEME) NAFASI 15


(INARUDIWA)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;
Kufunga mfumo wa umeme unaohitajika kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo ya
miradi ya maji na usafi wa mazingira;
Kufunga mota na vifaa vingine vya umeme vya aina mbalimbali vya miradi ya maji
na usafi wa mazingira;
Kufanya usafi na ukaguzi wa mfumo wa umeme, mota na vifaa vingine umeme
vya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu
wa pampu na kuzuia uharibifu;
Kuendesha mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na ya kuzuia uharibifu kwenye
mfumo wa umeme, mota na vifaa vingine umeme kwa kufuata miongozo ya
uendeshaji, na inapohitajika kwa dharura.
Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji
na matengenezo ya mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa
mazingira;
Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.

10.2

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya
mwaka mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na
Serikali ambao wana Cheti cha ufundi Daraja III (Plants Technician Electrical).

10.3

MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.

11.0

FUNDI SANIFU MSAIDIZI (MAJI) (ASISTANT TECHNICIAN - WATER) NAFASI


24 (INARUDIWA)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
11.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kupima uwingi wa maji mtoni
Kusoma kituo cha hali ya hewa
Kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
11.2

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha VI waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachotambuliwa na
Serikali ambao wana cheti cha ufundi Daraja la III katika fani ya maji.

11.3

MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.

12.0
12.1

MHANDISI KILIMO II (IRRIGATION) - 1


MAJUKUMU YA KAZI
Kuandaa programu za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo.
Kushiriki katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana.
Kushiri katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji.
Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafundisha wakulima uendeshaji wa skimu za
umwagiliaji.
Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji.
Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji
pamoja na matumizi ya maji.
Kuandaa mafunzo/maonesha ya matumizi ya zana za kilimo.
Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na
wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta.
Kuwafundisha wakulima jinsi ya ujenzi wa vihenge bora.
Kushughurikia ubora wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezaji
ipasavyo.

12.2

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya
kilimo cha umwagiliaji kutoka chuo kikuu kinachotambuliwa na serikali.

12.3

MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi

13.0
13.1

MHANDISI KILIMO II (MECHANIZATION) 1


MAJUKUMU YA KAZI
Kuandaa programu za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo.
Kushiriki katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana.
Kushiri katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji.
Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafundisha wakulima uendeshaji wa skimu za
umwagiliaji.
Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji.
Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji
pamoja na matumizi ya maji.
Kuandaa mafunzo/maonesha ya matumizi ya zana za kilimo.
Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na
wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta.
Kuwafundisha wakulima jinsi ya ujenzi wa vihenge bora.
Kushughurikia ubora wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezaji
ipasavyo.

13.2

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya
zana za kilimo kutoka chuo kikuu kinachotambuliwa na serikali.

13.3

MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi

14.0
14.1

MHANDISI KILIMO II (LAND USE PLANNING) 1


MAJUKUMU YA KAZI
Kuandaa programu za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo.

Kushiriki katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana.

Kushiri katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji.

Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafundisha wakulima uendeshaji wa skimu za


umwagiliaji.

Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji.

Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji


pamoja na matumizi ya maji.

Kuandaa mafunzo/maonesha ya matumizi ya zana za kilimo.

Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na


wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta.

Kuwafundisha wakulima jinsi ya ujenzi wa vihenge bora.

Kushughurikia ubora wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezaji


ipasavyo.

14.2

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya
matumizi bora ya ardhi (land use planning) kutoka chuo kikuu kinachotambuliwa
na serikali.

14.3

MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E wa mwezi

X.M. DAUDI
Secretary
Public Service Recruitment Secretariat

You might also like