You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

TAARIFA KWA UMMA


Wizara

ya

Afya,

Maendeleo

ya

Jamii,

Jinsia,

Wazee

na

Watoto

inampongeza Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul


Makonda kwa kupiga marufuku matumizi ya Shisha na uvutaji wa Sigara
hadharani kama afua ya kupunguza madhara ya tumbaku na madawa ya
kulevya katika jamii.
Uchunguzi wa kitalaam uliofanyika umebaini kuwa Shisha ina madhara
kwa afya ya watumiaji hasa vijana na watoto. Watumiaji wa Shisha
wanatumia kiwango kikubwa cha tumbaku kwa muda mfupi, hali
inayoongeza madhara yatokanayo na tumbaku kama vile: - Saratani,
Magonjwa ya Mapafu, Kibofu cha mkojo, Tezi dume, Koo, Mdomo na
Kiywa, Ngozi, Ini, Ubongo.
Pia imebainika kwamba matumizi ya Shisha huambatana na kuongezewa
dawa nyingine za kulevya na hivyo hufanya watumiaji wa Shisha kupata
uraibu wa dawa za kulevya. Matumizi ya dawa hizo za kulevya ni kosa la
jinai.
AGIZO
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda
kurejea na kusisitiza agizo lake la tarehe 12 Machi 2015 la kuzuia matumizi
ya sigara na matumizi ya bidhaa za tumbaku katika maeneo ya umma.
Inakumbushwa kwamba agizo hili limezingatia utekelezaji wa Sheria ya
Usimamizi wa Bidhaa za Tumbaku, Sura ya 121 T.L 2002, ya Sheria za
Tanzania kipengele cha 12 (1) ambacho kinakataza matumizi ya Tumbaku
katika Maeneo ya Umma.
MADHUMUNI
Madhumu ya Agizo hili ni kuilinda Jamii kwa ujumla kutokana na
madhara yatokanayo na moshi wa sigara. Wizara inawakumbusha

wananchi wanaotumia bidhaa za tumbaku kupunguza au kuacha kabisa


matumizi ya tumbaku. Aidha, agizo hili linaijumuisha jamii yote katika
kubaini madhara ya tumbaku na umuhimu wa kuzuia matumizi ya
tumbaku katika maeneo ya kazi na maeneo yote ya umma.
WALENGWA
Agizo hili linawahusu wananchi wote nchini wanaopata huduma katika
maeneo ya umma kama ilivyotafsiriwa na sheria husika.
MAENEO HUSIKA
Matumizi ya tumbaku hayaruhusiwi katika maeneo yote ya umma. Maeneo
haya yanajumuisha ofisi zote za Serikali na tasisi zake zote, watu binafsi,
vyuo, vituo vya huduma za Afya zikiwemo Hospitali, vituo vya Afya na
zahanati, vituo vya usafiri wa Anga, Mabasi, bandari na treni, sehemu za
mikutano,

mapumziko,

bustani

na

fuko

za

maji,sherehe,michezo,masoko,maduka makubwa pamoja na sehemu za


kuabudu.Na kwa mtu yeyote anayeendesha shughuli katika maeneo ya
umma analazimika kutenga eneo maalum kwa ajili ya wavuta sigara.
UTEKELEZEJI
Kwa kuwa Mhe. Waziri mwenye dhamana na masuala ya Afya nchini
ameona hatari hii ya Uvutaji wa sigara na utumiaji wa bidhaa za tumbaku
kwa afya ya Wananchi, kuanzia leo tarehe 4/7/2016 matumizi ya Shisha
nchini yamepigwa marufuku kwa wote wanaojihusisha na matumizi hayo,
na kwa wafanyabiashara wote wanaojihusisha na upatikanaji wa Shisha
nchini.
Hivyo basi, kwa agizo hili katika maeneo yote nchini ambako matumizi ya
Shisha hufanyika ni marufuku matumizi hayo kuendelea kutumika.
Aidha vyombo vya Dola na mamlaka husika vinahimizwa kusimamia kwa
ukamilifu katazo hili.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Afya
04/07/2016

You might also like