You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA

TELEGRAMS: POLISI,
TELEPHONE: 2500712
Fax: 2502310
E-mail: mwapol@yahoo.com
rpc.mwanza@tpf.go.tz

OFISI YA
KAMANDA WA POLISI,
MKOA WA MWANZA,
S.L.P. 120,
MWANZA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO


VYA HABARI LEO TAREHE 09.07.2016

MTU MMOJA MWENYE ASILI YA ASIA (HINDU) AMEKUTWA AKIWA


AMEKUFA KIFO CHA MASHAKA NYUMBANI KWAKE WILAYANI
NYAMAGANA.

KWAMBA TAREHE 09.07.2016 MAJIRA YA SAA 10:00 USIKU KATIKA MTAA WA NYERERE ROAD
KATA NA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA ALIYEJULIKANA
KWA JINA LA SURESH NARANJIAN SOMAIYA MIAKA [72] MWENYE ASILI YA ASIA (HINDU)
MENEJA WA SIMBA BISCUIT NA MKAZI WA MTAA WA NYERERE ROAD, ALIKUTWA AKIWA
AMEKUFA KIFO CHA MASHAKA CHOONI HUKU MWILI WAKE UKIWA NA JERAHA DOGO
UPANDE WA BEGA LA KUSHOTO NA KAMBA YA KIATU ILIYOFUNGWA SHINGONI.

AIDHA INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUA AKIISHI NA MDOGO WAKE WAKIUME, SHEMEJI
YAKE, PAMOJA NA MSAIDIZI WA KAZI ZA NDANI MAJINA YAMEHIFADHIWA, KATIKA NYUMBA
HIYO AMBAYO AMEKUTWA AKIWA AMEFARIKI, NDIPO INADAIWA MAJIRA TAJWA HAPO JUU
MDOGO WAKE MAREHEMU WA KIUME AMBAYE ANAISHINAYE HAPO NYUMBANI KWAKE
ALIKWENDA CHOONI NA KUMKUTA KAKA YAKE YAANI MAREHEMU AKIWA AMEANGUKA NA
KUFARIKI DUNIA, NDIPO ALIPOAMUA KUTOA TAARIFA POLISI.

ASKARI WALIWEZA KUFIKA KWA WAKATI KATIKA ENEO LA TUKIO NA KUUKUTA MWILI WA
MAREHEMU UKIWA UMEANGUKA CHOONI. AIDHA UCHUNGUZI WA AWALI ULIONYESHA
MWILI WA MAREHEMU UKIWA NA JERAHA DOGO KWENYE BEGA LA KUSHOTO NA UKIWA
UMEFUNGWA KAMBA YA KIATU SHINGONI, CHANZO CHA KIFO HICHO KINACHUNGUZWA, PIA
HAKUNA MTU YEYOTE ALIYEKAMATWA KUHUSIANA NA KIFO HICHO.

JESHI LA POLISI LIPO KWENYE MAHOJIANO NA NDUGU NA JAMAA WA MAREHEMU


WALIOKUWEPO KATIKA NYUMBA HIYO, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI
YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI, HUKU UCHUNGUZI PAMOJA NA UPELELZI
UKIWA BADO UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI


AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA NDUGU PAMOJA NA JAMAA WA MAREHEMU
AKIWATAKA WATULIE NA KUWAPISHA JESHI LA POLISI LIWEZE KUFANYA KAZI YA
UCHUNGUZI KUHUSIANA NA KIFO HICHO VIZURI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA TAARIFA
KAMILI ITATOLEWA NA IKITHIBITIKA KUNA MTU AU WATU WAMEHUSIKA KATIKA KIFO
HICHO HATUA ZINAZOSTAHILI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO.

IMETOLEWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

You might also like