You are on page 1of 3

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR

TANGAZO LA UFADHILI WA MASOMO YA UZAMIVU KATIKA


FANI YA ELIMU (PHD IN EDUCATION)
CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR (SUZA) KUPITIA MRADI WAKE WA
TRANSLED UNAOFADHILIWA NA SHIRIKA LA NORAD KINATANGAZA UFADHILI WA
MASOMO YA UZAMIVU KATIKA FANI YA ELIMU KATIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES
SALAAM.
MUOMBAJI ATAKAECHAGULIWA KUENDELEA NA MASOMO YA CHUO NA
KUKUBALIWA NA SUZA KUTOKANA NA MAHITAJI ILIYONAYO, MASHARTI YA
MKATABA ATAKAOFUNGA NA SUZA NA MASHARTI YA MRADIATAPATIWA
UFADHILI WA MASOMO IKIWEMO ADA YA MASOMO (TUITION FEES), MALIPO YA
MOJA KWA MOJA (DIRECT COSTS) NA UTAFITI (RESEARCH) KWA MIAKA YOTE YA
MASOMO.
MUOMBAJI ANATAKIWA KUFANYA MAMBO YAFUATAYO:
1. KUJAZA FOMU YA MAOMBI YA ONLINE ILIYOPO KWENYE TOVUTI YA CHUO
KIKUU CHA DAR ES SALAAM AMBAYO NI http://postgraduate.udsm.ac.tz/
2. ATATAKIWA KUCHAGUA PhD IN EDUCATION BY COURSEWORK NA
DISSERTATION. KATIKA SEHEMU YA BARUA YA MWAJIRI SI LAZIMA
KUAMBATANISHA ANDIKA TU NINAYO, NA PIA BARUA YA SPONSOR
ANDIKA TRANSLED PROJECT FUNDED BY NORAD.
3. ATATAKIWA KUTUMA MAOMBI YA UFADHILI AKIAMBATANISHA CHETI CHA
KUZALIWA, VYETI VYOTE VYA MASOMO, NA SABABU NA USHAHIDI WA
YEYE KUPATIWA UFADHILI WA MASOMO NA BARUA YA KUKUBALIWA NA
CHUO (ADMISSION LETTER). BARUA YA MAOMBI YA UFADHILI IANDIKWE
KWA KIINGEREZA NA IPELEKWE KWA MRATIBU MKUU WA MRADI WA
TRANSLED.CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR, P. O. BOX 146,
ZANZIBAR.

MUOMBAJI ATAKAE FADHILIWA NA MRADI ANATAKIWA KUWA NA SIFA


ZIFUATAZO:
1. AWE MZANZIBARI
2. AWE NA DIGRII YA UZAMILI KATIKA FANI YA ELIMU AU NYENGINEYO
INAYOSHABIHIANA.
3. IWAPO HANA DIGRII YA UZAMILI YA FANI YA ELIMU AU INAYOSHABIHIANA
BASI AWE NA DIGRII YA UZAMILI NYENGINE LAKINI AWE ANAYO SHAHADA
YA KWANZA YA FANI YA ELIMU NA SAYANSI (BSC. WITH EDUCATION) AU
ELIMU NA SANAA (B.A. WITH EDUCATION).
WAOMBAJI WATAKAOPEWA KIPAUMBELE:
1. PAMOJA NA SIFA ZILIZOTAJWA WAOMBAJI WATAKAOPEWA KIPAUMBELE
NI WALE WASIO NA UWEZO WA KUJISOMESHA, MAYATIMA, WANAWAKE,
WATU WENYE ULEMAVU, WATU WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA
MAGUMU.

2. WALIOSOMA SHAHADA YA KWANZA AU YA PILI (UZAMILI) KATIKA FANI YA


SAYANSI NA ELIMU (SCIENCE WITH EDUCATION) AMBAO WALICHUKUA
MASOMO YA BIOLOJIA, KEMIA, FIZIKIA NA HESABU. WALIOSOMEA SANAA
NA ELIMU KATIKA MASOMO YA JIOGRAFIA NA HISTORIA WANAWEZA
KUFADHILIWA IKIBIDI.
3. WALIOSOMA FANI YA ELIMU MJUMUISHO (INCLUSIVE EDUCATION), FANI
YA ELIMU AWALI AU AU ELIMU KWA MICHEZO NA SAYANSI YA MICHEZO,
AIDHA KATIKA SHAHADA YA KWANZA AU YA PILI.
ZINGATIA
WATAKAOLETA MAOMBI YA UFADHILI NA VIELELEZO VYOTE IKIWEMO BARUA ZA
KUKUBALIWA NA CHUO (ADMISSION LETTER) KWA MRATIBU WA MRADI WA
TRANSLED MWANZO NA WENYE SIFA ZILIZOTAJWA NDIO WATAKAOPATA

UFADHILI (FIRST COME FIRST SERVED). WATAKAOFADHILIWA NI WAOMBAJI


WATATU TU.
MWISHO WA KUWASILISHA MAOMBI NI ALHAMISI TAREHE 29 SEPTEMBA,
2016.
KWA MAELEZO ZAIDI PIGA SIMU NAMBA 0778000313

You might also like