You are on page 1of 3

Maudhui ya utengano ukizingatia nadharia ya uhalisia.

Utangulizi.
Maudhui hurejelea yaliyomo katika kazi Fulani ya fasihi au jumla ya masuala
yanayozungumziwa na mwandishi au mtunzi katika kazi yake ya kifasihi.Baadhi yay a wahakiki
huyachukua maudhui kama mawazo ya kijumla ya mwandishi.Maudhui ni mada mbalimbali
anazojishughulisha nazo mwandishi.Riwaya ya utengano ni riwaya ambayo imejikita katika
kujadili maudhui mbalimbali kwa mapana na marefu.Maudhui katika riwaya ya utengano
huchangiwa na wahusika wake kwani wao ndio wajenzi wa maudhui mbalimbali.Riwaya ya
utengano imezungumzia masuala mbalimbali yanayoikabili jumuiya ya mwandishi.Baadhi ya
maudhui katika riwaya ya Utengano ni kama Utengano,Visasi,Ufisadi,Uhuru na nafasi ya
mwanamke katika jamii,Ukahaba,Ukoloni-mambo leo,Unafiki na Dhuluma dhidi ya wanawake.

Nadharia ya uhalisia ni msomaji kuvaa sura,matendo na tabia za mhusika mkuu na wasaidizi


wake.Mudhui ya utengano ukizingatia nadharia uhalisia basi ni kuangazia maudhui hayo
ukijiweka katika hali za mhusika mkuu na wasaidizi wake.Maudhui ni kama yafuatayo.

Maudhui ya riwaya ya Utengano.

Utengano.
Maudhui ya Utengano yamefafanuliwa sana katika sehemu nyingi za riwaya yenyewe.Utengano
unajitokeza katika sura mbalimbali.Kuna utengano wa kifamilia unaoshuhudiwa katika familia
ya Bw.Maksudi.Kiini cha utengano huu ni maovu yanayosababishwa na Bw.Maksudi
mwenyewe.Maksudi anatenganishwa na mwanawe Mussa kupitia kisasi cha Bi.Farashuu.Hii ni
kwa sababu Maksudi alikuwa amemtendea ukatili Mwanasururu,mwanawe Farashuu.Aidha
unafiki wa maksudi unasababisha mvurugano kati yake na bintiye Maimuna na mkewe
Tamima.Uovu wa Maksudi pia unfanya yeye kutengana na ndunguye Inspekta Fadhili.Pia
tunapata utengano wa kijinsia.Jamii inaonyesha mapendeleo kwa jinsia ya kiume na kutenga
jinsia ya kike.Hli hii imesababisha utengano kati ya wanaume na wanawake.Wanaume hupewa
nafasi bora katika jamii huku wanawake wakiachiwa kazi za kinyumbani.Utengano wa kitabaka
pia inaonekana katika riwaya hii.Kunayo pengo kubwa kati ya matajiri na maskini katika jamii
husika.Matajiri huishi katika majengo kubwa huku maskini wakijilaza katika vibanda.Uhusiano
kati ya maskini na matajiri umejaa unafiki na usaliti.Matabaka ya matajiri huhusishwa katika
uongozi ambao huwapa fursa ya kuwakandamiza maskini.Hivyo basi kuna haja ya kuwa na
umoja katika wanajamii,katika mataifa yaliyojikomboa kutokana na ukoloni.Utengano
unadidimiza juhudi za kujenga jamii mpya.

Kisasi.
Maudhui ya kisasi yanabainika katika riwaya hii.Mtindo wa kulipa kosa kwa kosa
ummendelezwa sana na mwandishi wa riwaya hii.Whusika wengi wanaonekana wakilipiza kisasi
wanapokosewa.Maudhui ya kisasi ndiyo yanayozingira mgogoro mkuukatika riwaya hii.Kuna
kisasi baina ya Maksudi na Farashuu.Farashuu ana kisasi na Maksudi kwa vile Maksudi
anamtesa na kusababisha kifo cha mwanawe Mwanasururu,kwa sababu hii Farashuu anaamua
kulipiza kisasi kwa Maksudi.Kwanza,anamfumaniza Mussa na Maksudi kwake Kazija.Pili
anamtorosha Maimuna huko Pumziko akaharibike namna mwanawe Mwanasururu
alivyoharibikia huko Bobea baada ya kutalakiwa na kufisidiwa na Maksudi.Mpango huu
unafanikishwa na Biti Kocho,mtumishi wa Maksudi.Kisasi kingine kinaonekana katika mkutano
wa kisiasa katika uwanja wa Uhuru.Hiki ni kisasi cha Umma na viongozi wanafiki na
dhalimu,Zanga na Maksudi.Kazija anapoudokeza unafiki,ukatili,ufisadi na udhalimu wa
Maksudi na Zanga.Mudhui ya kisasi yanadhihirika tena riwayani kupitia uhusiano wa Maimuna
na Shoka.Maimuna anapomkatalia Shoka ombi lake la kimapenzi.Shoka anamtumia Kijakazi ili
kumjazia Maimuna hisia za wivu na pia anachochea vita ili Maimuna wapigane na Kijakazi kisa
na maana anataka ionekane kuwa ni yeye wanayempigania.Hivyo basi si vizuri kwa wanyonge
kujikomboa kwa njia ya kulipiza kisasi kwani kisasi ni itikadi inayoweza kuwapa wanyonge
uwezo wa kujikomboa.

Ufisadi.
Maudhui ya ufisadi yameendelezwa katika sura kadhaa za riwaya hii.Viongozi na asasi za
kitawala kama vile idara ya polisi,ndio wanaoendeleza ufisadi.Ufisadi unajitokeza pale Biti
Kocho anapolazimishwa na karani wa viwanja amlipe shilingi mia mbili ndipo nae amsaidie
kupata kiwanja anachohitaji.Inabidi Biti Kocho kuomba msaada wa pesa kutoka kwa mnyonge
mwenzake Farashuu.Ufisadi pia unajitokeza katika uongozi wa Bw.Maksudi.Akiwa
mkurungenzi wa shirika la Bima la Taifa,Maksudi anakula njama na mzungu
mmoja,Mr.Smith,kulipora shirika hili.Maksuudi anakubali kumlipa Smith fidia asiyo na haki ya
kuipata.Katika njama hii,Maksuudi anakiri kuwa atatumia pesa kuwanyamazisha polisi
wasiifuatilie kesi hiyo.Maksudi pia akiwa katika shirika hili anakabiliwa na kesi mbaya ya
ufisadi na naonekana akiomba msaada wa ndunguye inspekta Fadhili amsaidie kudidimiza kesi
hiyo ili isimharibie kra wakati wa uchaguzi.Katika mazungumzo baina ya Maksuudi na Inspekta
Fadhili tunabaini kuwa polisi huchukua hongo,Maksuudi anasema hivi: Hapo ndipo
ninapokuona mjinga.Wenzio askari kama wewe wanakula mirungura,wewe ni nani hasa
kukataa?.Ufisadi pia unajitokeza katika maelezo ya mtaa wa Tweni na mji wa Pumziko.Mama
Jeni baadhi ya bidhaa za kimagendo alizohodhi katika duka lake.Hizi amezificha katika duka
lake zisionekane na walio karibu na serikali.Ufisadi pale umeelezwa kama kikwazo
kinachodumaza juhudi za serikali na vyombo vya habari kuangamiza biashara haramu.Kuna pia
ufisadi unaotokana na matumizi mabaya yay a mamlaka.Maksuudi anatumia cheo chake kama
mkuu wa wilaya kurithi shamba na nyumba ya Buheti,Mwarabu tajiri huko Via,baada ya nchi
yake kujikomboa na pia tunammwona akiuza sahihi yake kama mkuu wa wilaya kwa shilingi
mia mbili.Ufisadi basi unastahili kukashifiwa vikali kwa maendeleo mema ya uongozi katika
jamii.

Uhuru na nafasi ya mwanamke katika jamii.

You might also like