You are on page 1of 6

Maudhuiyautenganoukizingatianadhariayauhalisia.

Utangulizi.
Maudhuihurejeleayaliyomokatikakazi Fulani yafasihi au
jumlayamasualayanayozungumziwanamwandishi au mtunzikatikakaziyakeyakifasihi.Baadhi yay
a
wahakikihuyachukuamaudhuikamamawazoyakijumlayamwandishi.Maudhuinimadambalimbalia
nazojishughulishanazomwandishi.Riwayayautenganoniriwayaambayoimejikitakatikakujadilimau
dhuimbalimbalikwamapananamarefu.Maudhuikatikariwayayautenganohuchangiwanawahusika
wake
kwaniwaondiowajenziwamaudhuimbalimbali.Riwayayautenganoimezungumziamasualambalimb
aliyanayoikabilijumuiyayamwandishi.BaadhiyamaudhuikatikariwayayaUtenganonikamaUtengan
o,Visasi,Ufisadi,Uhurunanafasiyamwanamkekatikajamii,Ukahaba,Ukoloni-mambo
leo,UnafikinaDhulumadhidiyawanawake.

Nadhariayauhalisianimsomajikuvaasura,matendonatabiazamhusikamkuunawasaidiziwake.Mudh
uiyautenganoukizingatianadhariauhalisiabasinikuangaziamaudhuihayoukijiwekakatikahalizamhu
sikamkuunawasaidiziwake.Maudhuinikamayafuatayo.

MaudhuiyariwayayaUtengano.

Utengano.
MaudhuiyaUtenganoyamefafanuliwasanakatikasehemunyingizariwayayenyewe.Utenganounajito
kezakatikasurambalimbali.KunautenganowakifamiliaunaoshuhudiwakatikafamiliayaBw.Maksudi
.Kiini cha
utenganohuunimaovuyanayosababishwanaBw.Maksudimwenyewe.Maksudianatenganishwanam
wanaweMussakupitiakisasi cha
Bi.Farashuu.HiinikwasababuMaksudialikuwaamemtendeaukatiliMwanasururu,mwanaweFarashu
u.AidhaunafikiwamaksudiunasababishamvuruganokatiyakenabintiyeMaimunanamkeweTamima.
UovuwaMaksudipiaunfanyayeyekutengananandunguyeInspektaFadhili.Piatunapatautenganowaki
jinsia.Jamiiinaonyeshamapendeleokwajinsiayakiumenakutengajinsiayakike.Hlihiiimesababishaut
enganokatiyawanaumenawanawake.Wanaumehupewanafasi bora
katikajamiihukuwanawakewakiachiwakazizakinyumbani.Utenganowakitabakapiainaonekanakati
kariwayahii.Kunayopengokubwakatiyamatajirinamaskinikatikajamiihusika.Matajirihuishikatika
majengokubwahukumaskiniwakijilazakatikavibanda.Uhusianokatiyamaskininamatajiriumejaaun
afikinausaliti.Matabakayamatajirihuhusishwakatikauongoziambaohuwapafursayakuwakandamiz
amaskini.Hivyobasikunahajayakuwanaumojakatikawanajamii,katikamataifayaliyojikomboakutok
ananaukoloni.Utenganounadidimizajuhudizakujengajamiimpya.

Kisasi.
Maudhuiyakisasiyanabainikakatikariwayahii.Mtindowakulipakosakwakosaummendelezwasanan
amwandishiwariwayahii.Whusikawengiwanaonekanawakilipizakisasiwanapokosewa.Maudhuiya
kisasindiyoyanayozingiramgogoromkuukatikariwayahii.KunakisasibainayaMaksudinaFarashuu.
FarashuuanakisasinaMaksudikwa vile Maksudianamtesanakusababishakifo cha
mwanaweMwanasururu,kwasababuhiiFarashuuanaamuakulipizakisasikwaMaksudi.Kwanza,ana
mfumanizaMussanaMaksudikwakeKazija.PilianamtoroshaMaimunahukoPumzikoakaharibikena
mnamwanaweMwanasururualivyoharibikiahukoBobeabaadayakutalakiwanakufisidiwanaMaksud
i.MpangohuuunafanikishwanaBitiKocho,mtumishiwaMaksudi.Kisasikinginekinaonekanakatika
mkutanowakisiasakatikauwanjawaUhuru.Hikinikisasi cha
Ummanaviongoziwanafikinadhalimu,ZanganaMaksudi.Kazijaanapoudokezaunafiki,ukatili,ufisad
inaudhalimuwaMaksudinaZanga.MudhuiyakisasiyanadhihirikatenariwayanikupitiauhusianowaM
aimunanaShoka.MaimunaanapomkataliaShokaombi lake la
kimapenzi.ShokaanamtumiaKijakaziilikumjaziaMaimunahisiazawivunapiaanachochea vita
iliMaimunawapiganenaKijakazikisanamaanaanatakaionekanekuwaniyeyewanayempigania.Hivy
obasisivizurikwawanyongekujikomboakwanjiayakulipizakisasikwanikisasiniitikadiinayowezaku
wapawanyongeuwezowakujikomboa.

Ufisadi.
Maudhuiyaufisadiyameendelezwakatikasurakadhaazariwayahii.Viongozinaasasizakitawalakama
vile idarayapolisi,ndiowanaoendelezaufisadi.Ufisadiunajitokeza pale
BitiKochoanapolazimishwanakaraniwaviwanjaamlipeshilingimiambilindiponaeamsaidiekupataki
wanjaanachohitaji.InabidiBitiKochokuombamsaadawapesakutokakwamnyongemwenzakeFarash
uu.UfisadipiaunajitokezakatikauongoziwaBw.Maksudi.Akiwamkurungenziwashirika la Bima la
Taifa,Maksudianakulanjamanamzungummoja,Mr.Smith,kuliporashirikahili.Maksuudianakubalik
umlipaSmith
fidiaasiyonahakiyakuipata.Katikanjamahii,Maksuudianakirikuwaatatumiapesakuwanyamazishap
olisiwasiifuatiliekesihiyo.Maksudipiaakiwakatikashirikahilianakabiliwanakesimbayayaufisadina
naonekanaakiombamsaadawandunguyeinspektaFadhiliamsaidiekudidimizakesihiyoiliisimharibie
krawakatiwauchaguzi.KatikamazungumzobainayaMaksuudinaInspektaFadhilitunabainikuwapoli
sihuchukuahongo,Maksuudianasemahivi:
Hapondiponinapokuonamjinga.Wenzioaskarikamawewewanakulamirungura,weweninanihasaku
kataa?.UfisadipiaunajitokezakatikamaelezoyamtaawaTweninamjiwaPumziko.MamaJenibaadhiy
abidhaazakimagendoalizohodhikatikadukalake.Hiziamezifichakatikaduka lake
zisionekanenawaliokaribunaserikali.Ufisadi pale
umeelezwakamakikwazokinachodumazajuhudizaserikalinavyombovyahabarikuangamizabiashar
aharamu.Kunapiaufisadiunaotokananamatumizimabaya yay a
mamlaka.MaksuudianatumiacheochakekamamkuuwawilayakurithishambananyumbayaBuheti,M
warabutajirihukoVia,baadayanchiyakekujikomboanapiatunammwonaakiuzasahihiyakekamamku
uwawilayakwashilingimiambili.Ufisadibasiunastahilikukashifiwavikalikwamaendeleomemayauo
ngozikatikajamii.

Uhurunanafasiyamwanamkekatikajamii.
Licha ya kuwa ni jumuiya inayosimuliwa imeondosha minyororo ya utumwa na ukolni bado
mwanamke ni mtumwa wa utamaduni wa jamii yake.Jamii hii imejengeka katika mfumo wa
kuumeni ambao unampa mwanamume mamlaka zaidi kuliko mwanamke.Wanawake katika
riwaya hii wanaonekana kunyimwa uhuru wa kibinafsi.Maksuudi anawatawisha bintiye
Maimuna na mkewe Tamima,hawakurusiwa kutoka nje wala kumruhusu yeyote kuingia huko
bila idhini ya Maksuudi.Tamima ananyimwa uhuru wa kuchagua mkunga atakayemzalisha na pia
haki ya kujifungua hospitalini.Tamima wanapokosana na Maksuudi hana haki ya kukataa talaka
kisheria au kiukoo.Suala la uhuru wa mwanamke ndilo linaloamua hadhi yake katika
jamii.Ukosefu wa uhuru unamfanya mwanamke kukosa elimu,kazi bora na haki katika jamii
anamoishi.Katika riwaya hii wanawake wanasawiriwa kama viumbe wasio na ukomavu wa
kiakil.Maimuna anapata uhuru wa kufanya atakavyo pale ambapo anatoroka kwao nyumbani
lakini uhuru anaopata Maimuna sio halisi kwani anapata uhuru asiotarajia.Anaishi kuwa kahaba
wa Mama jeni na Biti Sururu.Mwandishi anadhamiria kuonyesha,mwanamke anaponyimwa
uhuru kunamfanya kuwa mtegemezi na anpojipatia uhuru huo anakuwa mhitaji na hii ndiyo
sababu Kazija ,Maimuna,Dora,Kijakazi na wengine wanakuwa makahaba.Wanawake wengine
pia wanajipata wakifanya biashara duni kamakuendesha madanguro,kuoka mandazi, na kupika
pombe ya kienyeji huku wanaume wakiwa vingozi,madaktari,madereva,wenye maduka
makubwa.Selume anateswa na mumewe huku Maksuudi akiwatesa wake zake.Hata hivyo
tunawaona wanawake wakipigania uhuru wao kama Kzija,Biti Kocho,Farashuu na
Maimuna.Serikali pia inaweza kusaidia katika ukombozi wa wanawake.Mwandishi anasema
hivi: 'Serikali itafanya kampeni kubwa kuwaelimisha wanawake vijijini....kunatakikana
maendeleo ya haraka vijijini na maendeleo ya wanawake ni maendeleo ya jamii nzima,ni
ukombozi wa jamii nzima.

Ukoloni mambo leo.


Ukoloni mambo leo ni kati ya maudhui yaliyorejelewa na mwandishi katika riwaya ya
utengano.Licha ya jamii kujitoa katika minyororo ya ukoloni viongozi fulani wanachukua
hatamu na kuendeleza ukoloni uleule wa mkoloni wa awali.Maksuudi anfuata mienendo ya
wakoloni ,anatumia cheo chake kunyanganya na kuwadhulumu wanyonge,baada ya kuchaguliwa
kuliongoza wilaya Maksuudi anarithi nyumba ya tajiri mmoja mwarabu.Ple ambapo Maksuudi
anawatawisha Maimuna na Tamima ni ishara ya ukoloni aliyokuwa akitenda
Maksuudi.Maksuudi akiwa mkurungezi wa shirika la bima la Taifa,anaonekana akishirikiana na
wazungu kulipora shirika hilo,anamlipa Mr.Smith fidia asiyostahiki.Kwake nyumbani kwa
Maksuudi anamiliki Samani mbalimbali kutoka nchi za ulaya,jambo hili linachangia kudorora
kwa uchumi wa nchi yake.Katika maelezo ya Shoka pia tunapata ukoloni mambo leo,huu ni
wakati Shoka anamshawishi Maimuna kuyapokea malipo duni ili wafanye mapenzi,Shoka
anatetea unyonge wake hivi:"wewe unafikiria pesa tuzipatazo sisi wachukuzi au wakulima au
wafanyakazi za sulubu ni pesa za mchezo?Mkulima anachuwana na jembe,nguvu zake huishia
wapi? Umarekani,Ujerumani au Ujapani wao ndio wanaopanga bei za mazao yetu,na
wafanyakazi wa karakana wanafanyia nani kazi,ukitazama sana wanamfanyia mkoloni mambo
leo; nasi;wapangazi bandarani tunampakilia nani bidhaa una.. unafikiria? Mabeberu bado,bado
hatuna uhuru kamili,hatujaudhibiti uchumi".Hivyo basi mataifa yaliyostawi yanazorotesha ukuaji
wa uchumi wa mataifa yanayoendelea kama Afrika.Ukoloni mambo leo pia unadhihirika katika
biashara zinazoendeshwa huko Pumziko,inavyobainika,mali nyingi ya magendo inaingizwa pale
kutoka nchi za nje.Hatimaye mtaa wa Toweni unaonekana kumilikiwa na matajiri kutoka
nje.Hwa ndio wanaingiza mali ya nje katika mji wa Pumziko.

Mabadiliko.
Maudhui ya mabadiliko yamechukua nafasi kubwa katika riwaya hii.Mabadiliko yanadhihirika
kaika familia ya Maksuudi iliyokuwa na mshikamano wa kifamilia,Utengano wa kifamilia
unashuhudiwa pale Mussa,Miamuna na mama yao Tamima wote wanatenganishwa,kila mmoja
kaienda njia zake.Maksuudi anaachwa na kitoto kichanga kilichozaliwa usiku ule wa utengano
lakini kinaaga dunia.
Ktika enzi za ukoloni,Maksuudi alikuwa mtetezi wa wanyonge na wapiginiaji wa uhuru,hii pia ni
maudhui ya mabadiliko.Lakini kujitolea kwake kulikuwa nia ya kibinafsi.Nchi iliponyakua
uhuru,aliaminiwa na kuteuliwa mkuu wa wilaya,hapo ndipo udhalimu wake
unadhihiri.Anabadilika na kuwa mkoloni-mamboleo,mkatili na kiongozi asiyejali wanyonge
katika jamii.Licha ya kudai ucha-mungu,Maksuudi anatenda kinyume na dini na hata kuwa na
wake nje ya ndoa.Badiliko la maisha ya Maksuudi linamsababishia kufungwa jela miaka
miwili.Hata hivyo mwandishi amedhihirisha kwamba kinchoweza kudumu maishani ni
mabadiliko tu.Inabidi Maksuudi abadilike.Maisha ya mjini na ya hadhi anayaacha na kurudi
shambani.Utengano anaojenga baina yake na wanyonge anauziba.Anaonekana akitangamana na
wafanyakazi wake Mabruki na Haji.Anatimuliwa kwa kazi anayojivunia.Juu ya haya anajaribu
kuziba utengano anaousababisha nyumbani kwake.Afya yake pia inadhoofika licha ya kuwa mtu
mwenye afya nzuri.Maksuudi pia anapokonywa mali aliyowapokonya watu hapo
awali.Mwandishi anaonyesha namna mabadiliko yanavyoweza kuwarudi viongozi katika jamii.
Mabadiliko pia yanadhihirika kupitia mhusika Mussa.Mussa alikuwa mkware na mlevi lakini
baaada ya kufumaniwa na babake anamakinika katika masoma yake ya chuo na kufuzu na kuwa
daktari.Pia anaona si haba na kufuta yaliyojiri baina yake na babake.Maudhui ya mabadiliko pia
yanajitokeza kwa uhusiano baina ya familia ya Farashuu na familia yake Maksuudi.Ingawa
Farashuu anaweka kisasi dhidi ya familia ya Maksuudi,hata kuitnganisha,hatimaye ndoa ya
Maimuna na Kabi inaondosha kisasi chake.Farashuu anaonekana akiwajibika kama mpatanishi
baina ya familia hizi mbili.Hata anasaidia kupatana kwa Mussa,Tamima na Maimuna.
Mabadiliko yamedhihirishwa hata na Maimuna.Maimuna ni mtoto aliyelelewa akaelekea kupitia
kutawishwa ili asije akachafuliwa na ulimwengu,hata hivyo anatoroka utawa na kuenda
kujitafutia uhuru anaotamani.Utoro wake unamgeuza mhitaji huku akiwa akiukimbia ukwasi
mkubwa.Anaanza maisha ya ukahaba ambayo yanambadilisha hata na urembo wake lakini
hatimaye anaurudia ustaarabu wake pamoja na afya baada ya kuolewa na Kabi.Maudhui ya
mabadiliko yamechangia sana katika kuleta uhalisia katika riwaya hii.Kupitia hali hii wahusika
mbalimbali wamesawiriwa katika mabadiliko ama kwa wema au uovu.Ni kupitia mabadiliko
ambapo vingozi kama Maksuudi wameonjeshwa maisha ya mafukara na wanyonge,aidha
mabadiliko ndiyo matumaini ya wanyonge kwamba hali zinazowadhalilisha haziwezi kudumu
milele.Hili linawapa hamasaisho na hamasa kuendelea kupigania hali bora maishani.Hii ndyo
sababu ya mwandishi kutochorea taswira ya upatanisho mwishoni mwa riwaya na kuondosha
Maksuudi,ambaye ni kielelezo cha udhalimu na kikwazo kwa ujenzi wa jamii mpya.
Ukahaba.

You might also like