You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Simu: +255-22-2112035/40 9 Barabaraya Ohio


Nukushi: +255-2122617/2120486 S.L.P. 9223
Baruapepe: ps@moha.go.tz 11483 DAR ES SALAAM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendeleza jitihada zake za


kuliboresha na kuondoa changamoto mbalimbali zinazolikabili Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji hapa nchini, kwa kutenga kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa
sare za askari wa Jeshi hilo katika Bajeti yake ya mwaka wa fedha 2017/ 2018.

Hatua ya Serikali kutenga fedha hizo itasaidia kupunguza mapungufu ya sare za askari
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyokuwa yakilikabili Jeshi hilo na hivyo kuwafanya
askari wake kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye amesema


kwa mwaka huu mpya wa fedha, Serikali imeendelea kutatua changamoto za uhaba wa
vitendea kazi ndani ya Jeshi hilo kama vile magari na madawa ya kuzima moto ambapo
imetenga kiasi cha shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kununua magari ongezeko ambalo ni
mara dufu ya kiasi kilichotolewa mwaka wa fedha uliopita.

Kamishna Jenerali Andengenye amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita
wa 2016/2017 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitenga pia kiasi cha
shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ununuzi wa magari ya kuzima moto, jitihada hizi za Serikali
zinalenga kuondoa changamoto ya uhaba wa vitendea kazi na hivyo kurahisisha
utendaji kazi wa jeshi hilo.

You might also like