You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
Simu Na: +255 (026) 2963630 Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Nukushi: +255 (026) 2963629 na Utawala Bora,
Barua Pepe: ps@utumishi.go.tz Jengo la Taaluma Na. 1,
Tovuti: http://www.utumishi.go.tz Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria,
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
Barabara ya Mkalama,
S.L.P. 670,
40404 DODOMA.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SERIKALI HAIJAFUTA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA UMMA

Serikali haijafuta mafunzo kwa watumishi wa umma ambapo Taasisi za


Serikali zimeelekezwa kuandaa Mpango wa Mafunzo kwa watumishi kwa njia
ya uwazi na shirikishi ili kuepuka malalamiko kutoka kwa baadhi ya watumishi
wa umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala


Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na
Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, jijini Dar es
Salaam.

Mhe. Kairuki amesema mwajiri anapoandaa Mpango wa Mafunzo kwa


watumishi wake ni vyema mpango huo ukawa shirikisha kwa watumishi wote ili
kujua mpangilio wake, ikiwa ni pamoja na kuandaa orodha ya ziada ya
watumishi watakaochukua nafasi za wale waliopangwa kushiriki mafunzo lakini
wakashindwa.
Napokea malalamiko mengi sana kuhusiana na upendeleo katika suala la
mafunzo, napenda kuwasisitiza waajiri tuandae Mpango wa Mafunzo ambao ni
shirikishi kwa watumishi wote kuepuka haya, wengine wanapangwa na
hawashiriki mafunzo, Mhe. Kairuki amesema na kuongeza baadhi ya
watumishi wa umma wanapangwa kushiriki mafunzo na hawaendi kwa sababu
mbalimbali, lakini fursa ya nafasi hizo hawapangiwi wengine ili kuendana na
mpango.

Mhe. Kairuki ameongeza kuwa Mpango wa Mafunzo shirikishi pamoja na


kuondoa malalamiko, utasaidia pia kutorudisha fedha zilizobaki kwa watumishi
wa umma ambao walipangwa lakini wakashindwa kuhudhuria mafunzo kwa
sababu mbalimbali.

Aidha, Mhe. Kairuki amesema kwa sababu ya kutoshirikishwa wapo


wanaopotosha kuwa Serikali imefuta Mpango wa Mafunzo. Napenda
kuwaambia kuwa Serikali haijafuta mafunzo, ili mtumishi wa umma aweze
kufanya kazi zake kwa weledi ni lazima ahudhurie mafunzo, Mhe. Kairuki
amesema na kusisitiza Serikali inajali mafunzo kwa rasilimaliwatu kwa
matokeo bora.

Mhe. Kairuki yupo katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es salaama
ambapo leo ni siku ya nane akiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
kwa kukutana na watumishi wa umma wa kada zote katika vikao kazi.

Lengo la kukutana na watumishi wa umma ni kusikiliza malalamiko, ushauri na


changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia

2
kazi na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini ili kufikia malengo
yaliyopangwa na Serikali.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI


OFISI YA RAIS-UTUMISHI
19.07.2017

You might also like