You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
Simu Na: +255 (026) 2963630 Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Nukushi: +255 (026) 2963629 na Utawala Bora,
Barua Pepe: ps@utumishi.go.tz Jengo la Taaluma Na. 1,
Tovuti: http://www.utumishi.go.tz Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria,
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
Barabara ya Mkalama,
S.L.P. 670,
40404 DODOMA.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UHAMISHO WA WATUMISHI WA UMMA UFANYIKE KWA MAKINI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amezitaka Taasisi za Serikali kuratibu
suala la uhamisho wa watumishi wa umma kwa makini pale inapohitajika
kufanya hivyo Ili kuepuka kero na usumbufu kwa watumishi.

Waziri Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa
Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala eneo la Segerea, jijini Dar es
Salaam.

Mhe. Kairuki amesema uhamisho lazima ufanyike kwa mtumishi wa umma


endapo kukiwa na sababu za msingi sana. Naomba ieleweke kuwa uhamisho
una taratibu zake hivyo kila mwajiri ni mwajiri akazifuata. Mhe. Kairuki
alisisitiza.

Ameongeza kuwa imebainika wapo baadhi ya watumishi wa umma


wanawasilisha sababu mbalimbali kwa waajiri kuomba kuhama wakiwa na nia
ya kukwepa kukaguliwa sifa zao za elimu.
Waziri Kairuki amesisitiza kuwa uhamisho usifanyike kwa mtumishi ambaye
anaonekana kuwa na matatizo.

Baadhi ya waajiri wamekuwa na tabia ya kuwahamisha watumishi wa umma


ambao wameonekana kuwa na tatizo na kuwahamishia sehemu nyingine,
uhamisho wa namna hii haukubaliki, tatizo la mtumishi linatakiwa kufanyiwa
kazi kwenye kituo chake cha kazi na sio kupeleka tatizo sehemu nyingine.
Mhe. Kairuki ameongeza.

Mhe. Kairuki yupo katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es salaama
ambapo leo ni siku ya tisa akiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala-
Segerea kwa kukutana na watumishi wa umma wa kada zote katika vikao kazi.

Waziri Kairuki katika vikao kazi amehimiza watumishi wa umma nchini kubadili
mtindo wa maisha, kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi, kujiepusha na
ugonjwa wa UKIMWI, na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa (MSY).

Lengo la kukutana na watumishi wa umma ni kusikiliza malalamiko, ushauri na


changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia
kazi na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini ili kufikia malengo
yaliyopangwa na Serikali.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI


OFISI YA RAIS-UTUMISHI
20.07.2017

You might also like