You are on page 1of 1

Mchakato wa Uanzishaji Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi Waanza.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano - Sekta ya


Mawasiliano, Injinia Angelina Madete amesema uanzishaji wa Taasisi ya Teknolojia ya
Ufundi (ICoT), utasaidia kupunguza pengo lililopo sasa baina ya wahandisi, mafundi
sanifu na mafundi mchundo hapa nchini.

Akifungua warsha ya wataalam washauri na wadau wa Taasisi ya Teknolojia ya Ufundi


Jijini Dar es salaam leo, Mhandisi Madete amewataka wataalam hao kufanya
uchambuzi wa kina ili kuwezesha taasisi hiyo mpya kukidhi mahitaji ya mafundi sanifu
na mchundo na hivyo kukidhi uwiano wa kimataifa unaotaka mhandisi mmoja, fundi
sanifu watano na mafundi mchundo 25.

Tunataka kuwa nchi ya viwanda vya kati ifikapo mwaka 2025, hivyo ni lazima tuwe
na wahandisi, mafundi sanifu na mafundi mchundo wa kutosha watakaofanyakazi kwa
weledi na kumudu ushindani katika soko la ajira, amebainisha Injinia Madete.

Mhandisi Madete amesema kuwa pengo la wahandisi, mafundi sanifu na mafundi


mchundo limeongezeka kutokana na vyuo vingi vya kati kutoa shahada hivyo uwepo
wa ICoT utakabiliana na kumaliza changamoto hiyo.

Aidha amezungumzia umuhimu wa taasisi hiyo mpya kuanzisha kozi ya waendesha


mitambo ambayo mahitaji yake ni makubwa hapa nchini na kwa sasa hakuna chuo
kinachotoa kozi hiyo.

Hakikisheni taasisi hii inapata ithibati ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE),
ili kuwawezesha wahitimu wote wa ICoT kupata fursa za kujiendeleza na elimu ya juu.

Naye mratibu wa wataalam wa uanzishaji ICoT Profesa Peter Chonjo amesema


wamejipanga kuhakikisha taasisi hiyo ya teknolojia ya ujenzi inakuwa ya mfano hapa
nchini kwa kuwa itawezesha wataalam wengi wa ujenzi kuwa na weledi unaokubalika
na kuibua uwezo wa ushindani katika soko la ajira na hivyo kuwezesha Tanzania
kufikia malengo yake ya kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Tanzania inakadiriwa kuwa na mtandao wa barabara wenye zaidi ya kilometa elfu 87


na kati ya hizo elfu 35 ni barabara za kitaifa na elfu 52 ni barabara za Wilaya ambazo
ujenzi wake unahitaji wataalam wa kutosha katika fani ya ujenzi na uendeshaji wa
mitambo.

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na


Mawasiliano.

You might also like