You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


IDARA YA UHAMIAJI

OFISI YA KAMISHNA JENERALI WA


ANUANI YA SIMU: UHAMIAJI UHAMIAJI,

TELEFAX: +255 22 2850595 S .L . P. 512,


+255 22 2850584
Dar-es-salaam.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Idara ya Uhamiaji imesema jukumu la Udhibiti wa Uingiaji na Utokaji wa raia wa


kigeni nchini, linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 (Rejeo la
2016) na wala haiwalengi wafanyakazi wa Kampuni ya Madini ya Acacia peke yake.

Ni hitajio la kisheria kwa kila raia wa kigeni anayeingia na kutoka nchini kukaguliwa
ili kujiridhisha iwapo hakuna dosari zozote za Uhamiaji, Ulinzi na Usalama.

Sheria ya Uhamiaji inaitaka Idara ya Uhamiaji kumhoji mtu yeyote awe raia wa
Tanzania au kigeni bila kujali anafanya kazi kwenye Kampuni au Shirika gani, pale
inapotaka kujiridhisha juu ya uhalali wa ukaazi wake hapa nchini na ikijiridhisha kuwa
mtu huyu hana dosari zozote inamwachia huru kama ilivyofanyika kwa wafanyakazi
wa Kampuni ya Madini ya Acacia waliohojiwa na kuruhusiwa kuendelea na safari yao
hivi karibuni.

Idara ya Uhamiaji inapenda kuuarifu Umma kuwa hakuna sababu zozote nje ya
matakwa ya Sheria ya Uhamiaji zinazopelekea Idara ya Uhamiaji kuweka kizuizi cha
kuja au kutoka kwa wafanyakazi wa kigeni wa Acacia.

Tunapenda kuujulisha Umma kuwa ni muhimu kwa watanzania na raia wa kigeni


wanaokusudia kuingia na kutoka nchini kuhakikisha wanafuata Sheria za Uhamiaji ili
kutimiza hitajio la kisheria.

Imetolewa na
Ally M. Mtanda
Msemaji wa Idara ya Uhamiaji
29 Julai 2017

You might also like