You are on page 1of 1

1

STATE HOUSE ZANZIBAR


OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE
Zanzibar 17 . 08 .201 7

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed


Shein , amewahakikishia wananach i wa Zanzibar kuwa Serikali anayoiongoza
itahakikisha inaimaarisha huduma za afya kwa wananchi wake kutambua kuwa
afya haina mbadala.

Dk. Shein aliyasema hay o leo kwa nyakati tofauti katika ziara yake katika Wilaya ya
Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.

Katik a maelezo yake Dk. Shein mara baada ya kuweka jiwe la msingi la nyumba ya
Madaktari na familia mbili huko Kajengwa Makunduchi, alieleza kuwa amekwenda
kijijini hapo kutekeleza ahadi aliyowaahidi wananchi wakati alipokwenda kuzindua
kituo cha afya.

Dk. She in aliahidi je ngo hilo kulimaliza kwa kuliezeka, kulitia milango na madirisha
huku akieleza kuwa huduma za afya katika kipindi hichi zimeimarika kwa kiasi
kikubwa ikilinganishwa na hapo siku za nyuma katika kijiji hicho cha Makunduchi.

Alisema kuwa huduma za afya hasa Makunduchi zimeimarika kwa kiasi kikubwa na
kueleza kuwa hivi karibuni juhudi zilifanyika katika kuchangia ili hospitali hiyo izidi
kuimarika na iwe ya Mkoa kwa kuimarisha majengo na huduma nyengine

Alieleza kuwa mara baada ya kumalizika kwa jengo hilo huduma hizo zitaimarika zaidi
kwani madaktari watapata fursa za kuishi hapo hapo katika eneo la kituo cha afya
huku akieleza kuwa Mkoa huo umepata bahati ya kujengwa hospitali ya rufaa huko
Binguni, Wilaya ya Kati Unguja.

Aliongeza kuwa ni uwa muzi wa Serikali ya Ma pinduzi ya Zanzibar kuimarisha huduma


za afya na kusisitiza kuwa Serikali hii inapenda watu wake na iko makini katika
kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora.

Aieleza kuwa hivi karibuni

You might also like