You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

Tele: +255 026 2322761-5 Ofisi ya Bunge


Fax No. +255 026 2324218 S.L.P. 941
E-mail: info@bunge.go.tz DODOMA.


TAARIFA KWA UMMA
__________

Ofisi ya Bunge inapenda kuutaarifu Umma kuwa Kiongozi wa Kambi ya Rasmi


ya Upinzani Bungeni Mheshimiwa Freeman Mbowe hajanyanganywa gari
kama ambavyo inapotoshwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kilichotokea ni kwamba gari hiyo imerudishwa Nchini ili dereva wa gari hilo
afuate taratibu za kupata kibali cha kusafiri nje ya nchi. Ni vema ieleweke
kuwa ni kweli gari yenye Na. STL. 4587 Aina ya Toyota Prado imetengwa
maalum kwa ajili ya kumuhudumia Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni katika kutekeleza Majukumu yake ya kikazi na binafsi hapa Nchini.

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni aliomba gari ikamhudumie


Mjini Nairobi Nchini Kenya ambapo Ofisi ya Bunge iliridhia ombi hilo na
kuomba taratibu zizingatiwe. Hata hivyo, Ofisi iligundua kwamba gari
ilikwenda Nairobi na dereva hakupata kibali cha kusafiri nje ya Nchi
ambacho kila mtumishi wa Umma anayesafiri nje ya Nchi lazima apate
kibali hicho kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi (Chief Secretary).

Hivyo basi, kwa kuwa tarartibu zilikuwa hazijakamilika, dereva aliambiwa


alirejeshe gari hilo Nchini na kuliegesha katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Arusha hadi taratibu nyingine zitakapokamilika. Dereva yupo Dodoma
anakamilisha taratibu ili ofisi iweze kumuombea kibali Ikulu ndipo anaweza
kurejea Nchini Kenya kwa ajili ya kuendelea kumhudumia Kiongozi wa
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Ni dhamira ya Ofisi ya Bunge kuendelea kumhudumia Kiongozi wa Kambi


Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa kufuata misingi na kanuni za Utumishi wa
Umma na zile za Bunge bila kuchanganya na siasa.
Ofisi ya Bunge inauhakikishia Umma kuwa taratibu zikishakamilika Kiongozi
wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ataendelea kuhudumiwa popote
atakapokuwa.

Imetolewana:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
DODOMA

28 Septemba, 2017.

You might also like