You are on page 1of 2

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE

Anuani ya simu: Muhimbili Anuani ya Posta:


Simu: +255-22-2151379 S. L. P. 65141
Nukushi: +255-22-2150534 DAR ES SALAAM
Baruapepe: info@jkci.or.tz Tanzania

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MATOKEO YA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO WAKATI WA


MAADHIMISHO YA SIKU YA MOYO DUNIANI
Jumla ya wananchi 600 wameshiriki katika zoezi la upimaji wa magonjwa ya
Moyo ambao ulienda sambamba na utoaji wa elimu ya lishe bora kwa afya
bora ya Moyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani iliyofanyika
tarehe 29/09/2017 katika viwanja vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.

Wananchi walioshiriki katika zoezi hilo walipimwa urefu, uzito, shinikizo la


damu (BP), sukari na kupewa ushauri. Asilimia 80 ya wananchi waliopimwa
siku hiyo walikutwa na matatizo ya shinikizo la juu la damu na wengine
walikutwa na matatizo mengine ya Moyo.

Aidha wagonjwa 400 waliokutwa na matatizo ya moyo walipewa dawa na


baadhi yao walianzishiwa kliniki ili wataalamu wetu waweze kufuatilia
maendeleo ya afya zao kwa ukaribu na kuweza kupata huduma ya matibabu
kwa ukaribu zaidi.

Kwa namna ya kipekee tunazishukuru sana kampuni zinazotengeneza dawa za


binadamu za Tata Africa Holdings (T) LTD, Reddys, na Phillips ambazo ziligawa
dawa bure kwa wananchi waliokutwa na matatizo ya Moyo.

Tunawaomba wananchi wajenge tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii
itawasaidia kujuwa kama wanamatatizo ya moyo au la na hivyo kuanza
matibabu mapema. Asilimia kubwa ya wagonjwa tunaowapokea katika kliniki
zetu baada ya kuwafanyiwa vipimo tunawakuta mioyo yao haiko katika hali
nzuri. Hii inaonyesha kuwa wana matatizo ya Moyo pasipo kujifahamu.

Imetolewa na :

Kitengo cha Uhusiano na Masoko


Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
04/10/2017

You might also like