You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
Simu Na: +255 (026) 2963630 Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Nukushi: +255 (026) 2963629 na Utawala Bora,
Barua Pepe: ps@utumishi.go.tz Jengo la Taaluma Na. 1,
Tovuti:http://www.utumishi.go.tz Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria,
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
Barabara ya Mkalama,
S.L.P. 670,
40404 DODOMA.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MHE. MKUCHIKA AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUTEKELEZA


MAJUKUMU KWA KASI NA KUZINGATIA WELEDI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na


Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu), Mhe. George H. Mkuchika (Mb)
amewataka Watumishi wa Umma kutekeleza majukumu yao kwa kasi;
kuzingatia weledi pamoja na Sheria, Kanuni na taratibu za Utumishi wa
Umma nchini ili kuwa na utendaji bora wenye matokeo.

Mhe. Mkuchika (Mb) amesema hayo leo alipofanya ziara ya kikazi katika
taasisi anazoziongoza za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na
Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mkuchika amesema moja ya majukumu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti


ya Umma na Utawala Bora ni pamoja na kusimamia na kuimarisha utawala
bora katika uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa kubuni Sera, Sheria,
Kanuni na Taratibu za Uendeshaji na Usimamizi wa shughuli za utumishi
wa umma. Hivyo, ni muhimu watumishi wa umma walio katika ofisi hiyo
kuzingatia hayo ili kuwa mfano kwa wengine.

Ofisi yetu ni kioo ambacho watu wote wanakitazama, hivyo watumishi


wake hawana budi kuzingatia maadili katika utendaji kazi ili kuonyesha
mfano kwa wengine, Mhe. Mkuchika (Mb) amesema na kusisitiza
1
watumishi wa umma kutenda haki, kutobagua na kuepukana na suala la
rushwa au ushawishi wanapowahudumia Watanzania.

Aidha, Mhe. Mkuchika (Mb) ameomba watumishi wa umma katika eneo


lake na wengine kumpa ushirikiano wa kutosha na wa dhati katika utendaji
kazi wake ili kurahisisha utendaji kazi na kuleta matokeo mazuri katika
Utumishi wa Umma nchini.

Mimi ni mgeni, nimekuja kwenu kujitambulisha na kujifunza, hivyo nitahitaji


ushirikiano wa kutosha kutoka kwenu ili kurahisha utendaji kazi katika
kuwahudumia wananchi, Mhe. Mkuchika amesisitiza na kuongeza
mtendaji yoyote atakayeshindwa kutekeleza maelekezo yake, na kupata
taarifa za huduma mbaya kutoka kwa wananchi atamfuata katika eneo lake
la kazi kubaini ukweli.

Mhe. Mkuchika (Mb) ameanza ziara ya kikazi leo katika taasisi zilizo chini
ya Ofisi yake kwa lengo la kujitambulisha na kuzifahamu shughuli
mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi hizo ikiwemo kuchukua changamoto
za kufanyia kazi.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,
OFISI YA RAIS-MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA.
TAREHE 16 OKTOBA, 2017

You might also like