You are on page 1of 1

1

STATE HOUSE ZANZIBAR


OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE
Zanzibar 19.10.2017

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed


Shein leo amemuapisha Kapteni Khamis Simba Khamis kuwa Naibu Mkuu wa
Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM).

Kapteni Khamis Simba Khamis aliteuliwa hivi karibuni na Rais wa Zanzibar na


Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kushika wadhifa huo.

Hafla hiyo,ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar ambayo imehudhuri na viongozi mbali mbali
wa Serikali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Mawaziri wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan
Said, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya
Mzee.

Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Mufti


Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Hassan Othman Ngwali, Wakuu wa Vikosi vya SMZ, Washauri wa Rais wa Zanzibar,
Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib pamoja na viongozi
wengine wa Serikali.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar


Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

You might also like