You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


Simu Na.255-26-2963341/2963342/2963346 Chuo Kikuu cha Dodoma,
Nukushi: 255-26-2963348 Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya
Barua Pepe: ps@communitydevelopment.go.tz Maendeleo ya Jamii,
Tovuti:www.mcdgc.go.tz Jengo Namba 11,
S.L.P 573,
40478 DODOMA.

PONGEZI KWA WATOTO WALIOPATA UFAULU WA JUU NA


KUSHIKA NAFASI KUMI BORA KITAIFA KATIKA MATOKEO YA
MTIHANI WA DARASA LA SABA 2017

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatoa pongezi za dhati kwa
watoto wote waliopata ufaulu wa juu na kushika nafasi 10 bora kitaifa katika matokeo ya mtihani
wa Darasa la Saba kwa mwaka 2017.

Aidha, kwa namna ya pekee Wizara inawapongeza wanafunzi 4 wa kike waliopata ufaulu wa juu
na kuingia kwenye ushindani wa nafasi kumi bora kwa mwaka huu wa 2017, ukilinganisha na
mwanafunzi 1 tu wa kike aliyengara katika nafasi hizo kwa mwaka 2016.

Wizara imetambua juhudi binafsi zilizofanywa na mwanafunzi wa kike Hadija A. Ally kutoka
Shule ya Msingi Sir John ya jijini Tanga, ambaye ameshika nafasi ya kwanza kati ya wanafunzi
10 hodari kitaifa. Aidha, Wizara inampongeza mwanafunzi aliyeshika nafasi ya pili, Naseem K.
Said (Sir John, Tanga), nafasi ya sita ikishikiliwa na Insiya Kalimuddin (Sir John Tanga), na
nafasi ya saba ikishikilikiwa na Colletha Masungwa wa St. Achileus, ya mkoani Kagera.

Kadhalika, Wizara inawapongeza wanafunzi wa kike na wakiume ambao wameonesha jitihada


katika kutekeleza wajibu wao masomoni. Hii inaonesha dhahiri walikuwa wasikivu kwa walimu
wao, wazazi na walezi wao hivyo kuweza kupata matokeo mazuri.

Taarifa ya TECTA inaonesha kuwa ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 70.3 ya mwaka 2016
hadi asilimia 72.76 kwa mwaka 2017, sawa na ongezeko la asilimia 2.4; huu ni ushuhuda thabiti
kuwa wadau wa watoto wameshirikiana na Serikali katika kuimarisha na kuboresha mazingira ya
watoto kupata haki ya kuendelezwa na kumwezesha Mtoto wa kike na wa kiume kutimiza ndoto
zake.

Juhudi zilizooneshwa na watoto hawa wa kike ni ishara ya matokeo mazuri ya utekelezaji wa


azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kutoa fursa sawa kwa watoto wa kike na wa kiume
katika kupata haki ya elimu. Wakati tukiendelea na utekelezaji wa kampeni ya Mimi
Msichana, Najitambua; Elimu ndio Mpango Mzima, Wizara inatoa rai kwa watoto wote wa
kike kutafakari matokeo ya mwaka ya huu ili kuwa chachu ya kujitambua na kukataa mimba za
utotoni. Kama wanafunzi wa kike watajitambua na kujilinda, wataweza kusoma kwa ari kubwa
kwa manufaa yao na kutumikia Taifa kwa uzalendo wa dhati.

1
Wizara inawataka watoto wote wa kike na wa kiume waelewe kuwa wamehitimu daraja moja, na
bado wanalojukumu la kujiendeleza zaidi katika masomo ya sekondari na kwa wale ambao
hawakupata ufaulu unaotosheleza wanayo nafasi ya kujiendeleza kupitia taaluma mbalimbali na
stadi za maisha ili kupata maarifa yatakayowawezesha kutoa mchango katika juhudi za kufikia
uchumi wa kati na wa viwanda.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,
JINSIA, WAZEE NA WATOTO
25/10/2017

You might also like