You are on page 1of 2

TEMESA NA TBA ZATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KASI NA VIWANGO

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa amezitaka taasisi za Wizara ya Ujenzi,


Uchukuzi na Mawasiliano Mkoani Dodoma kufanya kazi kwa kasi, viwango na ufanisi ili
kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya tano yenye kauli mbiu ya Hapa Kazi tu.

Akizungumza wakati wa kikao kazi na wafanyakazi wa Taasisi ya Wakala wa Ufundi na


Umeme (TEMESA) na Wakala wa Majengo (TBA) amesema ni wakati sasa wa taasisi hizo
kuja na mwarobaini wa changamoto zilizopo na kubuni fursa za kuongeza kasi ya
maendeleo kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ya mji.

“Utendaji wenye weledi kwenye taasisi hususani katika utekelezaji wa miradi ya


miundombinu, ufundi na ujenzi utakidhi mahitaji ya watumishi wa Serikali kwa kuwapa
nyumba na ofisi zenye viwango ambazo zitakuwa za mfano kwa Makao Makuu ya
Serikali", amesema Kwandikwa.

Naibu Waziri Kwandikwa amesisitiza umuhimu wa taasisi hizo kuzingatia thamani ya


fedha kwa kuwekeza kwenye miradi yenye tija na faida ili kwenda na wakati na
teknolojia iliyopo.

Baada ya kukagua nyumba zinazomilikiwa na TBA, Naibu Waziri Kwandikwa, amesema


ni wakati muafaka wakala huo kuitazama upya mikataba iliyoingia na wapangaji wa
nyumba hizo ili kurekebisha vipengele vyote vyenye changamoto kwa lengo la kuweka
mazingira wezeshi kwa nyumba hizo ili zitunzwe na kudumu.

“Tazameni upya mikataba mliyoingia na wapangaji, haiwezekani nyumba zinachakaa na


takataka zinatupwa ovyo ovyo bila kuzingatia utaratibu, ifike mahala sasa mikataba
ieleze bayana, utaratibu wa utunzaji wa nyumba lakini pia uelekeze namna bora ya
kutunza mazingira", amesisitiza Kwandikwa.

Ameongeza kuwa ni wajibu wa wakala huo kupitia nyumba hizo kila wakati ili kufahamu
nyumba chakavu na kuweka mikakati ya kuzikarabati ili kuokoa fedha nyingi ambazo
zinatumika katika ukarabati wa mara moja kwa nyumba nyingi.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TBA, Steven Simba, amemuhakikishia Naibu Waziri
Kwandikwa kuwa TBA imejipanga kuhakikisha kuwa nyumba za Serikali zinajengwa kwa
kuzingatia viwango kulingana na mahitaji.

Awali akitoa taarifa kwa Naibu Waziri Kwandikwa amemueleza kuwa mwanzoni
walikua na nyumba mia nne, lakini sasa wameongezewa nyumba nyingine mia nne
kutoka CDA na pia kuna miradi inaendelea ya ujenzi wa nyumba nyingine, hivyo uwepo
wa nyumba hizo utapunguza changamoto ya makazi kwa watumishi wanaohamia
mkoani humo.

Naibu Waziri Kwandikwa amekagua karakana ya TEMESA, nyumba zaidi ya 800 za


watumishi na viongozi na maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na


Mawasiliano.

You might also like