You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
Simu Na: +255 (026) 2963630 Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Nukushi: +255 (026) 2963629 na Utawala Bora,
Barua Pepe: ps@utumishi.go.tz Jengo la Taaluma Na. 1,
Tovuti:http://www.utumishi.go.tz Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria,
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
18 Barabara ya Mkalama,
S.L.P. 670,
40404 DODOMA.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SERIKALI YA TANZANIA YAISHUKURU SERIKALI YA USWISS KWA USHIRIKIANO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala


Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) ameishukuru Serikali ya
Uswiss kwa ushirikiano wake katika sekta mbalimbali ikiwamo masuala ya
utawala bora.

Mhe. Mkuchika amesema hayo leo katika kikao na Balozi wa Uswiss nchini
Tanzania na Zambia, Mhe. Florence Tinguely Mattli kilichofanyika ofisini kwake
jijini Dodoma.

Mhe. Mkuchika amesema, Serikali ya Uswiss imekuwa ikitoa ushirikiano


mkubwa kwa Tanzania katika masuala ya utawala bora ambayo wafadhili
wengi hawayapi kipaumbele.

Amezitaja nchi nyingine zinazoshirikiana na Serikali ya Tanzania katika


masuala ya utawala bora kuwa ni Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo
la DfID na Marekani kupitia Shirika lake la Misaada la USAID.

Aidha, Mhe. Mkuchika amesema, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa


Tanzania chini ya Uongozi wa Rais wake, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
inahakikisha suala la utawala bora linazingatiwa katika utekelezaji wa
majukumu mbalimbali.

Kwa upande wake, Balozi wa Uswiss nchini Tanzania na Zambia, Mhe.


Florence Tinguely Mattli ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada
wanazozifanya katika utekelezaji wa masuala ya utawala bora na ameahidi
kuendeleza ushirikiano.

IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,
OFISI YA RAIS - UTUMISHI
15 MEI, 2018

You might also like