You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu: 255-22-2114512, 2116898 OFISI YA RAIS,
E-mail: press@ikulu.go.tz IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
Tovuti : www.ikulu.go.tz
11400 DAR ES SALAAM.
Faksi: 255-22-2113425
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ikulu, Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
amemteua Prof. Siza Donald Tumbo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utawala
ya Chuo cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College – ATC).

Prof. Tumbo ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Zana za Kilimo na


Teknolojia Vijijini (Center for Agricultural Mechanization and Rural
Technology – CAMARTEC).
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Mussa Iyombe
kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni kwa
Watumishi wa Umma (Public Service Social Security Fund - PSSSF).

Uteuzi huu wa wenyeviti wa bodi umeanza tarehe 13 Mei, 2018.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
14 Mei, 2018

You might also like