You are on page 1of 2

08th Juni 2018

TAARIFA KWA UMMA

USAWA KATIKA ULIPAJI WA KODI NA MANUFAA YAKE KATIKA KUBORESHA


HUDUMA ZA UMMA.

Katika mkutano wa vyama vya wafanyakazi, asasi za kiraia makundi ya


wanafunzi na vijana uliofanyika tarehe 07 hadi 08 mwezi Juni mwaka 2018
ulikuwa na ujumbe usemao “Kukabiliana na ukosefu wa usawa katika ulipaji
wa kodi” iliadhimiwa kwamba, Tanzania haiwezi kuendelea kupoteza fedha
za kodi zinazotokana na ukwepaji wa kulipa kodi na misahama isiyo na tija.
Washiriki wa warsha hii wametoa mapendekezo kwa serikali yetu tukufu ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ifuatavyo:

1. Kupitia upya misamaha na mikataba yote ya kodi na kuhakikisha


kunakuwepo na uwazi wa umiliki faida wanazopata makampuni
mbalimbali na kiwango cha kodi wanachotoa.
2. Serikali ya Tanzania inaombwa kuiongezea uwezo mamlaka ya
mapato Tanzania (TRA) ili iweze kukusanya mapato zaidi na fedha hizo
ziweze kujenga na kuboresha miundo mbinu pamoja na kutoa huduma
bora kwa umma.

Washiriki wa warsha hii walibaini kuwa katika miaka ya hivi karibuni


kumekuwa na makusanyo hafifu ya kodi inayotokana na makampuni ya nje
wakati makusanyo kutoka kwa wanachi mmoja mmoja yameongezeka
katika nyanja za kitaifa na kimataifa. Pia Tanzania inapoteza kiwango
kikubwa cha fedha kutokana na misamaha ya kodi kwa makampuni ya nje
isiyo na tija na mtiririko haramu wa fedha (illicitly financial flow of funds).

1
Kwa mfano inakadiriwa kwamba Tanzania inapoteza takribani dola za
kimarekani milioni 531.5 kila mwaka kutokanana misamaha ya kodi.
Aidha warsha hii ilibaini kuwa baadhi ya mikataba mbalimbali ya kodi ina
vifungu ambavyo vinainyima uwezo serikali yetu kukusanya kodi kwa
makampuni ya nje chini sheria ya kodi ya mwaka 2004.

Pia warsha hii ilibaini kuwa wananchi hawana uelewa wa kutosha kuhusu
kodi zinazotozwa kwa makampuni ya nje yanayofanya kazi Tanzania, na hii
inachangiwa zaidi na changamoto za usiri katika maswala ya fedha. Pia
imeshauriwa kwamba mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) iwengezewe
uwezo ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi katika kukusanya
kodi .

Washiriki wa warsha hii wanaamini kuwa Tanzania inaweza kukusanya


mapato mengi kwa kupunguza misamaha ya kodi isiyo na ulazima kwa
makampuni ya nje. Hii itasaidia kuondokana na changamoto ya upungufu
wa fedha kwa ajili ya uboreshaji wa miundo mbinu ya huduma mbalimbali
za umma na kuboresha maslahi ya wafanyakazi. Pia tunaamini kuwa vita ya
serikali dhidi ya mtiririko wa fedha haramu itafanikiwa endapo kutakuwa na
ushirikiano thabiti wa wadau mbalimbali vikiwemo vyama vya wafanyakazi,
asasi za kiraia na makundi mbalimbali katika jamii

Tamko hili limeandaliwa na washiriki wa warsha hii ambao wametoka;


Vyama Shiriki vya Public Services International (PSI) Tanzania; ( TALGWU,
TUGHE, RAAWU and TUICO), Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi Tanzania
(TUCTA), East African Trade Union Confederation (EATUC), Civil Society
Organizations such as Open Mind Tanzania (OMT), Tanzania Coalition on
Debt and Development (TCDD), Inter University Tax Justice Network Forum
(IUTJNF) and Pan African Center for Policy Studies (PACPS)

You might also like