You are on page 1of 7

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu: 255-22-2114512, 2116898 OFISI YA RAIS,
E-mail: press@ikulu.go.tz IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
Tovuti : www.ikulu.go.tz
11400 DAR ES SALAAM.
Faksi: 255-22-2113425
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ikulu, Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
leo tarehe 13 Agosti, 2018 amefanya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya 1,
Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji 41, na
amewahamisha vituo vya kazi Mkuu wa Wilaya 1 na Wakurugenzi wa Wilaya,
Miji, Manispaa na Majiji 19.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 13 Agosti, 2018 na Katibu Mkuu Kiongozi


Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Mhe. Dkt.
Magufuli amemteua Bi. Senyi Simon Ngaga kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Kwimba Mkoa wa Mwanza.

Bi. Senyi Simon Ngaga amechukua nafasi ya Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon
ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato
Mkoani Geita, baada ya Mkuu wa Wilaya ya Geita aliyeteuliwa hivi karibuni
Kanali Patrick Norbert Songea kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi nje ya
nchi.

Uteuzi wa Bi. Senyi Simon Ngaga unaanza leo tarehe 13 Agosti, 2018 na
Wakuu wa Wilaya wote wawili wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi
mara moja.

AIDHA, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi na uhamisho wa Wakurugenzi


wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji, kufuatia baadhi ya
Wakurugenzi waliokuwa katika nafasi hizo kustaafu, kupangiwa kazi nyingine,
kuhamishwa na wengine kuondolewa katika nafasi za ukurugenzi kama
ifuatavyo;

1
1. Mkoa wa Arusha.
i. Jiji la Arusha – Dr. Maulid Suleiman Madeni.
ii. Halmashauri ya Wilaya ya Meru – Bw. Emanuel Mkongo.

2. Mkoa wa Dar es Salaam.


i. Manispaa ya Temeke – Bw. Lusubilo Mwakabibi
(Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Mkoani Kigoma).
ii. Manispaa ya Ubungo – Bi. Beatrice Dominic Kwai
(Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya
Mtwara).
iii. Manispaa ya Ilala – Bw. Jumanne Kiango Shauri
(Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe).
iv. Manispaa ya Kigamboni – Bw. Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija
(Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa).

3. Mkoa wa Dodoma.
i. Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa – Bw. Mustafa S. Yusuph.
ii. Halmashauri ya Mji wa Kondoa – Ndg. Msoleni Juma Dakawa.
iii. Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa – Bw. Paul Mamba Sweya.
iv. Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa – Dkt. Omary A. Nkullo.

4. Mkoa wa Geita.
i. Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale – Bi. Mariam Khatib
Chaurembo.
ii. Halmashauri ya Wilaya ya Chato – Bw. Eliud Leonard
Mwaiteleke (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya
ya Misungwi).

5. Mkoa wa Iringa.
i. Halmashauri ya Manispaa ya Iringa – Bw. Hamid Ahmed Njovu
(amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya
Sumbawanga).
6. Mkoa wa Kagera.

2
i. Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi – Bw. Innocent Mbandwa
Mukandala.
ii. Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba – Bw. Limbe Bernard
Maurice (amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya
Misenyi).
iii. Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba – Bw. Solomon O. Kimilike.

7. Mkoa wa Katavi.
i. Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo – Bw. Ramadhan Mohamed.

8. Mkoa wa Kigoma.
ii. Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma – Ndg. Mwailwa Smith
Pangani (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya
Nsimbo).
iii. Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko – Ndg. Masumbuko
Stephano Magang’hila.
iv. Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma – Bi. Upendo Erick Mangali.

9. Mkoa wa Kilimanjaro.
i. Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga – Ndg. Zefrin Kimolo
Lubuva.
ii. Halmashauri ya Wilaya ya Moshi – Tatu Selemani Kikwete
(Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha).

10. Mkoa wa Lindi


i. Halmashauri ya Wilaya ya Liwale – Bw. Nassib Bakari Mmbaga
(Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya
Temeke).
ii. Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa – Bw. Renatus Blas Mchau.

11. Mkoa wa Mara.

3
i. Halmashauri ya Wilaya ya Musoma – Bw. Kayombo Lipesi John
(Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya
Ubungo).
ii. Halmashauri ya Wilaya ya Butiama – Ndg. Magori Mgalani
Alphonce.

12. Mkoa wa Mbeya.


i. Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya – Bw. Stephan Edward
Katemba (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa
ya Kigamboni).
ii. Halmashauri ya Jiji la Mbeya – Mrakibu Mwandamizi wa
Polisi James Cola Kasusura.
iii. Halmashauri ya Wilaya ya Kyela – Bi. Lucy L. Mganga.

13. Mkoa wa Morogoro.


i. Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero – Mhandisi Stephano
Bulili Kaliwa.
ii. Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro – Ndg. Kayombe Masoud
Lyoba.
iii. Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi – Bw. Mussa Elias Mnyeti.
iv. Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa – Asajile Lucas
Mwambambale.

14. Mkoa wa Mtwara.


i. Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara – Kanali Emmanuel Hally
Mwaigobeko.

15. Mkoa wa Mwanza.


ii. Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi – Ndg. Kisena Magena
Mabuba.
iii. Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe – Bi. Ester Anania Chaula.

4
16. Mkoa wa Njombe.
i. Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe – Ndg. Edes Philip
Lukoa (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya
Chalinze).
ii. Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa – Ndg. Sunday Deogratius
George.

17. Mkoa wa Pwani.


i. Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze – Bi. Amina Mohamed
Kiwanuka (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya
Wanging’ombe).
ii. Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha – Ndg. Butamo Nuru
Ndalahwa (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya
Moshi).

18. Mkoa wa Rukwa.


i. Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi – Bw. Engelus Wilbard
Kamugisha.
ii. Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo – Ndg. Msongela Nitu
Palela (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala).
iii. Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga – Bw. Jacob James
Mtalitinya (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya
Nzega).

19. Mkoa wa Ruvuma.


i. Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga – Bw. Juma Ally Mnwele.
ii. Halmashauri ya Mji wa Mbinga – Bi. Grace Stephen Quintine.
iii. Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo – Bw. Evans
Nachimbinya.
iv. Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru – Bw. Gasper Zahoro
Balyomi.

5
20. Mkoa wa Shinyanga.
i. Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga – Mrakibu Msaidizi wa
Uhamiaji Hoja Mahiba.

21. Mkoa wa Simiyu.


i. Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi – Mrakibu Msaidizi wa
Zimamoto James Marco John Mtembelea.

22. Mkoa wa Singida.


i. Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi – Bw. Justice K. Lawrence

23. Mkoa wa Songwe.


i. Halmashauri ya Wilaya ya Tunduma – Mhandisi Mussa Natty.
ii. Halmashauri ya Wilaya ya Songwe – Bi. Fauzia Hamidu.
iii. Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi – Ndg. Kazimbaya Makwega.
Adeladius (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya
Lushoto).

24. Mkoa wa Tabora.


i. Halmashauri ya Wilaya ya Nzega – Ndg. Sekiete Seleman
Yahaya.
ii. Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge – Bi. Martha Daudi Luleka.

25. Mkoa wa Tanga.


i. Halmashauri ya Mji wa Korogwe – Bw. Nicodemus John Bee.
ii. Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi – Ndg. Gracia Max Makota.
iii. Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli – Bw. George Haule.
iv. Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe – Ndg. Kwame Andrew
Daftari.
v. Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto – Mrakibu Mwandamizi
wa Uhamiaji Ikupa Harrison Mwasyoge.
Wakurugenzi ambao katika mabadiliko haya wamebadilishiwa vituo vya kazi
wanapaswa kwenda kuripoti katika vituo vyao vipya vya kazi mara moja, na
Wakurugenzi ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wanatakiwa kuripoti

6
kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Jijini Dodoma siku ya Jumatano tarehe 15 Agosti, 2018 kwa ajili
ya kupata maelekezo zaidi kuhusu majukumu yao na kula kiapo cha uadilifu
kwa viongozi wa umma.

Wakurugenzi wateule wanaokwenda TAMISEMI Jijini Dodoma wanapaswa


kuwa na vyeti vyao halisi (Originals), pamoja na nakala za vyeti hivyo
zilizothibitishwa kisheria (Certified Copies) vinavyoonesha matokeo ya
kumaliza elimu ya kidato cha nne, kidato cha sita na elimu ya taaluma
walizosomea.

Wakurugenzi ambao vituo vyao vya kazi havikutajwa katika mabadiliko haya
wanaendelea na nyadhifa zao katika vituo walivyopo.

WAKATI HUO HUO, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi


wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Huruma Mkuchika amemteua
Ndg. Mnkondo Yesaya Bendera kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Rungwe
ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Moses Maurus Mashaka ambaye
amepangiwa kazi nyingine.

Bw. Bendera anatakiwa kuripoti kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jijini Dodoma Jumatano tarehe 15
Agosti, 2018 kwa maelezo zaidi, akiwa na vyeti vyake halisi (Originals) vya
elimu ya Sekondari na vya elimu yay a taaluma alizosomea.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
13 Agosti, 2018

You might also like