You are on page 1of 2

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI-27 JUNE 2019

MAPITIO YA SERA YA KILIMO MWAKA 2019


Jukwaa huru la Wadau wa Kilimo (ANSAF) kwa kushirikiana na baadhi ya mashirika
wawakilishi wa wanachama wake wamekutana kupitia na kujadili sera ya kilimo ya
mwaka 2013 ambayo inafanyiwa maboresho na serikali kupitia Wizara ya Kilimo.
Lengo mahsusi la kikao kazi hiki ni kuitikia wito wa serikali kwa wadau mbalimbali
kutoa maoni kwenye sera ya kilimo ya mwaka 2013. Hivyo basi, kama Jukwaa huru la
Wadau wa Kilimo, ANSAF imefanya mapitio na majadiliano kuhusu sera ya mwaka
2013 na kuja na mapendekezo kuboresha sera hii.
Kwanza tunapenda kuishukuru na kuipongeza serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara
ya kilimo kwa kuwashirikisha Wadau wa kilimo kwa mapana yake katika kutoa maoni
kwenye mchakato huu wa kupitia na kuboresha sera ya kilimo ya mwaka 2013.
Tunaamini, ushirikishwaji huu utaongeza na kuchochea ushiriki wa Wadau katika
utekelezaji wa sera hii.
Pia tunaipongeza serikali kwa jitihada mbalimbali katika kukuza na kuendeleza sekta ya
kilimo hasa kupitia mpango wa maendeleo ya kilimo wa awamu ya pili (ASDPII)
uliozinduliwa mwaka 2018. Pia tunapongeza juhudi za serikali kuboresha mazingiza ya
biashara na uwekezaji nchini kupitia BLUEPRINT. Tunatambua pia nia na mikakati
mbali mbali kama vile kutunga sheria ya kilimo na bima ya kilimo katika juhudi za
kuleta maendeleo chanya kwenye kilimo nchini.
Kuelekea mapitio ya sera ya kilimo ya mwaka 2013, tunapendekeza yafuatayo;
1. UPOTEVU WA MAZAO baada ya kuvuna ni changamoto inayohitaji kufanyiwa
kazi katika sera ya Kilimo. Tunashauri sera ihimize serikali na wadau waweke mkazo
katika kutekeleza mkakati wa kitaifa wa kupunguza upotevu wa mazao kwenye
mnyororo wa thamani. Vipaumbele viwekwe katika kuhimiza upatikanaji wa elimu
kwa wadau, teknolojia za uhifadhi, miundombinu ya uhifadhi (maghala, vihenge),
usafirishaji, masoko na kuongeza thamani.

2. Sera ya Kilimo inatambua umuhimu wa upatikanaji wa takwimu sahihi za kilimo na


uwepo wa wadau mbalimbali. Ni muhimu, kuwa na mipango madhubuti ya
utekelezaji, uratibu na ufuatiliaji wa sera kwa ushirikiano na wadau wa sekta.
Kuboresha dawati la sekta binafsi, ni muhimu kuunda dawati maalumu la
vikundi/vyama vya wakulima na ushirika kwa maendeleo ya kilimo.

1
3. Kunahitajika msukumo zaidi kwenye upatikanaji na matumizi bora ya MBEGU na
PEMBEJEO muhimu za kilimo, HUDUMA za UGANI na TAFITI, na matumizi bora
na endelevu ya udongo kwa mazao mbalimbali ili kuongeza tija katika uzalishaji.

4. Tunaunga mkono dhumuni la serikali la kutunga sheria ya kulinda ARDHI YA


KILIMO. Pia tunahimiza kutambua na kuheshimu maeneo yaliyotengwa mahsusi
kwa shughuli za kilimo nchini. Sheria hii iendane na mipango ya matumizi bora ya
ardhi, hati miliki, mazao ya kipaumbele na mabadiliko ya tabia nchi.

5. Sera ya Kilimo inasisitiza upatikanaji wa mazao mengi na bora, ili kuhakikisha


usalama wa chakula na lishe kwa taifa na kaya. Maboresho ya sera ya kilimo
yamelenga kuchochea maendeleo ya VIWANDA nchini. Uwepo wa viwanda vya
ndani vinakuza soko la mazao ya wakulima. Hivyo basi, ni muhimu sera hii kuweka
mazingira rafiki yatakayohakikisha uwepo na ukuaji wa viwanda vya ndani kama
ilivyoainishwa kwenye mpango wa maendelo ya kilimo (ASDPII) na muongozo wa
kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini (BLUEPRINT).

6. Sera ya Kilimo inatambua na kuhimiza ushiriki wa VIJANA katika kilimo.


Tunahimiza maboresho haya yatambue na kuongeza nguvu kwenye mpango wa
utekelezaji wa mkakakati wa kushirikisha vijana kwenye kilimo biashara.

7. Sera ya Kilimo inatambua umuhimu wa kuongeza BAJETI ya kilimo na BIMA ya


mazao. Ili tifikie malengo ya maendeleo ya kilimo nchini, tunashauri serikali itoe
asilimi 10 ya bajeti iende kwenye kilimo kama yalivyo makubaliano ya MALABO.
Pia, tunahimiza kuharakisha uanzishwaji wa bima ya mazao.

8. Sera ya Kilimo inatambua umuhimu wa MIUNDOMBINU katika maendelo ya


kilimo. Ili kukuza kilimo kunahitajika kuwekeza kwenye miundombinu ya nishati,
umwagiliaji, usafirishaji wa mazao vijijini, masoko na hifadhi ya mazao.

Mashirika
1. Agricultural Non-State Actors Forum (ANSAF)
2. Tandahimba Farmers Association (TAFA)
3. AMSHA Institute of Rural Entrepreneurship
4. Action Aid Tanzania
5. Katani Ltd.
6. Tanzania Horticultural Association (TAHA)
7. Action for Democracy and Local Governance (ADLG)
8. Maasai Pastoralist development organization –Lareto (MPDO-Lareto)
9. Mwanasatu Development Organisation (MWADO)
10. Arusha NGOs Network (ANGONET)

You might also like